Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia petroli

Edzone

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Messages
745
Points
500

Edzone

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2017
745 500
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler. Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through parttime activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu. Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto repair shop. Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.

Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.

Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.
Niambie kuhusiana na engine ya Premio 7A 1760 CC
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,538
Points
2,000

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,538 2,000
ni Original mkuu
Kuna original na genuine...
Hata za kichina huwa na original kutokana na standard zao..

Genuine ni kama iliyotoka na gari....hakuna tofauti na inafanana mpaka part number na sometimes inasoma mpaka chasis number..

Part kuandikwa tu Toyota au Nissan haitoshi kuifanya iwe genuine bali yaweza kuwa original huko ilipitengenezwa..
 
ilogelo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
649
Points
1,000

ilogelo

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
649 1,000

Sasa utaitambuaje boss
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,538
Points
2,000

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,538 2,000
gari yangu nikiendesha kwa muda taa ya check engine inawaka nikitoa terminal na kurudishia gari inawaka na taa inazima. ni tatizo gani?
Kuna sensor imekufa...
Fanya diagnosis kujua kama ni MAF, O2 au sensors nyinginezo.....au ikute MAF sensor ni chafu sana.

Unapochomoa terminal ya battery unafanya reset ya computer ya gari na kudelete error code..
Ila ukiwasha gari na kutembea computer bado inakutana na taarifa za sensor mbovu, inadetect error code, wewe unaona check engine light..

Kuchomoa betri ni njia ya kureset check engine light endapo error ilitokea kimakosa..

Lakini kama sensor ni mbovu. erro itaendelea kujitokeza mpaka utakapobadilisha sensor husika.
 
Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Messages
1,538
Points
2,000

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2018
1,538 2,000
Sasa utaitambuaje boss
Mara nyingi genuine parts huhitaji kubeba sample..

Muuzaji ukimpa details za gari mfano

AIR FILTER

Make..NISSAN
Model..TIIDA
Year....2005
CHASIS NO....DBA E11

Details hizo akiingia nazo kwenye computer au stoo analeta spea yenye namba ile ile iliyokuja na gari..

Kwa makanjanja hawawezi kukuhudumia kwa kutumia deatails....watakudai sample ya spea iliyokufa....

Hakikisha namba za part unayonunua zinafanana na part unayotoa
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,516
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,516 2,000
gari yangu nikiendesha kwa muda taa ya check engine inawaka nikitoa terminal na kurudishia gari inawaka na taa inazima. ni tatizo gani?
Kafanye computer diagnosis mara moja usije ukajuta; usipoziba ufa utajenga ukuta! Kuondoa betri ni kufanya computer reset, lakini hakuondoi tatizo. Kuna matatizo mengine huwa ni madogo sana lakini yakiachwa kwa muda yanazaa matatizo makubwa zaidi.
 
Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Messages
8,516
Points
2,000

Kichuguu

Platinum Member
Joined Oct 11, 2006
8,516 2,000
Ninakushukru sana mkuu kwa maelekezo mrua.
Nilishabadili air cleaner tu.
Kuna fundi nilimshirikisha akanambia huenda ikawa ni fuel pump, nozzle, mounting na oxygen sensor.

Na gari ina km 200.000 kwa sasa, unashauri nibadilishe kitu gani ili liendelee kubaki kwenye hali yake?

Pia naomba kujua ni mafuta gani ya kuzibulia injector na wapi naweza yapata? Na kuna wakati ac inachelewa kufanya kazi hasa ninapokuwa nimepaki kwenye jua kwa muda mrefu.

Ngoja nifanyie kazi ushauri ulonipa kisha nilete mrejesho.
Fuel pump haisababishi matatizo unayosema; inaonekana kama vile injini haiunguzi mafuta vizuri, kwa hiyo ama haipati hewa ya kutosha au fuel pressure regulator haifanyi kazi sawasawa. Iwapo fuel pressure regulator imeshalegea, basi haiweki pressure ya kutosha kwenye injector na kufanya injectors zishindwe kuatomize mafuta ila zinadondosha matone ya kwenye cylinder mafuta na kusababisha yaungue kwa fujo. Lakini vile vile angalia sensor zako hasa ya aif flow sensor.

Niliwahi kupost huko nyuma kuhusu mafuta hayo ya kusafishia injectors, nasikia yanapatikana kwenye vituo vingi vya mafuta kama Total.
1571676647160.png

Kuhusu AC, je inachelewa kupooza au inachelewa kustart?
 
ilogelo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
649
Points
1,000

ilogelo

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
649 1,000
Fuel pump haisababishi matatizo unayosema; inaonekana kama vile injini haiunguzi mafuta vizuri, kwa hiyo ama haipati hewa ya kutosha au fuel pressure regulator haifanyi kazi sawasawa. Iwapo fuel pressure regulator imeshalegea, basi haiweki pressure ya kutosha kwenye injector na kufanya injectors zishindwe kuatomize mafuta ila zinadondosha matone ya kwenye cylinder mafuta na kusababisha yaungue kwa fujo. Lakini vile vile angalia sensor zako hasa ya aif flow sensor.

Niliwahi kupost huko nyuma kuhusu mafuta hayo ya kusafishia injectors, nasikia yanapatikana kwenye vituo vingi vya mafuta kama Total.
View attachment 1240323

Kuhusu AC, je inachelewa kupooza au inachelewa kustart?
ac inachelewa kupoza mkuu. Samahani mkuu, naomba kujua kama una ofisi ya ufundi hususani kwa dar.
 
ilogelo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
649
Points
1,000

ilogelo

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
649 1,000
Mara nyingi genuine parts huhitaji kubeba sample..

Muuzaji ukimpa details za gari mfano

AIR FILTER

Make..NISSAN
Model..TIIDA
Year....2005
CHASIS NO....DBA E11

Details hizo akiingia nazo kwenye computer au stoo analeta spea yenye namba ile ile iliyokuja na gari..

Kwa makanjanja hawawezi kukuhudumia kwa kutumia deatails....watakudai sample ya spea iliyokufa....

Hakikisha namba za part unayonunua zinafanana na part unayotoa
Shukrani mkuu
 
mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
19,076
Points
2,000

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
19,076 2,000
Mkuu mim nina Toyota mark 2 Gx 110,aisee linabwia mafuta,nimeweka mafuta ya 30,000 nimetoka nayo makumbusho mpaka tazara narud makumbusho taa ua mafuta inawaka
Ungesema hio safari nzima ni Km ngapi na mafuta ya elfu 30 unapata lita ngapi ingekua rahisi watu kujua gari yako inakula Km ngapi per litre maana sio kila mtu anapajua dar.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
19,076
Points
2,000

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
19,076 2,000
Mara nyingi genuine parts huhitaji kubeba sample..

Muuzaji ukimpa details za gari mfano

AIR FILTER

Make..NISSAN
Model..TIIDA
Year....2005
CHASIS NO....DBA E11

Details hizo akiingia nazo kwenye computer au stoo analeta spea yenye namba ile ile iliyokuja na gari..

Kwa makanjanja hawawezi kukuhudumia kwa kutumia deatails....watakudai sample ya spea iliyokufa....

Hakikisha namba za part unayonunua zinafanana na part unayotoa
Arusha nilipata tabu saana,nilikua natafuta clutch pressure plate ya bimmer 3 series, so nikawa napima nikitaka kujua hili ni duka la makanjanja naambiwa njoo na sample lkn nikiambiwa tutajie VIN Ya gari yako najua hawa wanajua wanachokifanya.
 
mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
19,076
Points
2,000

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
19,076 2,000
Fuel pump haisababishi matatizo unayosema; inaonekana kama vile injini haiunguzi mafuta vizuri, kwa hiyo ama haipati hewa ya kutosha au fuel pressure regulator haifanyi kazi sawasawa. Iwapo fuel pressure regulator imeshalegea, basi haiweki pressure ya kutosha kwenye injector na kufanya injectors zishindwe kuatomize mafuta ila zinadondosha matone ya kwenye cylinder mafuta na kusababisha yaungue kwa fujo. Lakini vile vile angalia sensor zako hasa ya aif flow sensor.

Niliwahi kupost huko nyuma kuhusu mafuta hayo ya kusafishia injectors, nasikia yanapatikana kwenye vituo vingi vya mafuta kama Total.
View attachment 1240323

Kuhusu AC, je inachelewa kupooza au inachelewa kustart?
Mkuu ninavyofahamu namna bora ya kusafisha injectors ni Ultrasonically.

Hayo mafuta ya kusafishia injectors si yanachukua uchafu kwny tank yanapeleka kwny injectors then ule uchafu unaelekea wapi mkuu?
 
WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Messages
835
Points
500

WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2015
835 500
Mkuu habari na hongera kwa kazi nzuri.

Nina shida na engine ya IZZ. Muungurumo wake umekuwa juu na pia kunakuwa na mlio wa kkkkkkk.

Fuel consuption imeongezeka tofauti na kawaida. Nimebadili plug lakini shida haijaisha bado.

Pia kunakuwa na vibration sana.
Ni mambo gani natakiwa kufanya na tatizo linaweza kuwa ni nini?
Pia check coil kama zote zinafanya kazi kama inavyotakiwa.
 
Forum statistics

Threads 1,364,506
Members 520,767
Posts 33,318,570
Top