Pombe si kitu kibaya ila binadamu wanaitumia vibaya. Pombe inaburudisha baada ya kazi ngumu. Raha ya pombe ni kunywa kiasi kidogo tu. Kama ni bia, moja au mbili zinatosha. Unasikiaje raha baada ya bia 5 au 7?
Mwanzo wa Wazungu kuanzisha Public Houses au Pub ilikuwa ni sehemu ya wanaume kukutana na kubadilisha a mawazo. Kutokana na hali ya uchumi wanaume wengi wa ujira wa chini walimudu bia moja au mbili.
Siku hizi watu wanakunywa benefit yote. Matokeo yake ni kuongezeka kwa magonjwa yatokanayo na Pombe.