Nitaweza kujenga nyumba kwa Milioni tatu?

Nitaweza kujenga nyumba kwa Milioni tatu?

3m kwa room mbili,sebule na choo cha master jumlisha na public,hela inatosha..ila utaweka vyumba vidogo angalau 8kwa 10,na sebule 8 kwa tisa jiko 8kwa 8fut.
Ila haitamaliza angalao itakufikisha kwenye madirisha..then unapumzika kidogo unatafuta hela kidogo inapiga mpaka lenta unapumzika then unapiga mpaka kumalizia kupaua unapumzika unatafuta hela..then unakuja kupaua na mabati ya bei rahisi 32g,unapiga nyavu za mbu...floor chumba kimoja unahamia.In three years unakua umemaliza nyumba mkuu...three year si mingi mkuu....*JIFUNZE KUWEKEZAATERIALS KWENYE HARDWERE KUBWA*

Sent using Nokia ya Torch
Kweli tena akiijenga vizuri akaweka na system za maji ,siku akija kuweka maji ni rahisi maji yanakuwepo mpaka ndani,ataweka na vioo vya alminum mbona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa anataka madilisha ya vioo! Jumla vyumba vitatu self, bado haitatosha wewe mama wewe. Kama ni kule kwetu igoma sawa lakini itabidi apige Ziggy zaggy chini

Ushanfahamu vizuri (in mussa hussein voice)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi naamini akiweka madirisha ya dril kisha akaweka nyavu ya kuzuia mbu tu vioo ataweka baadae

Mi mwaka huu lazima nijenge wallah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan kaka tena ukitaka usinunue tofali tafuta mtu muajili akufyatulie tofali azichome

Weka msingi mzuri wa kawaida ,vyumba visiwe vikubwa viwe wastani tu hasa chumba chako ndio kiwe kikubwa kiasi na sebule,kila kitu ufanye wastani utaniua nyumba utaezeka

Au weka msingi kwanza nyanyua boma mpaka kwenye lenta kisha ezeka bati,vingine fanya taratibu kama pesa itaishaa
Unaweza weka mlango mzuri wa mbao na ule wa drili mmoja ule wa kutokea nje vyumba vingine milango utaweka pole pole,mi naamini unaweza

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji7][emoji848] feeling encouraged!! Namim kamoyo kangu hakana haraka wala pupa, asanteeee tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mfano ukiwa na million 10 nyumba ya kawaida inaweza kufikia wapi kwenye ujenzi.
Kwa kweli mimi nikiwa na milioni kumi najenga nyumba ya vyumba vitatu self container,jiko,inaisha vizuri finishing yotee hadi na kuvuta maji au kuweka umeme,lakin ukitaka kasiri milioni kumi haitoshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3m labda ujenge ya miti juu weke nyasi, halafu fundi uwe mwenyewe na msaidizi mkeo!
  1. Ebu fikilia Chumba kimoja self container tofali 600 @ 1100/= 660000/=
  2. cement kujenga hadi plaster 10bags @ 14500/= 145000
  3. Mchanga fuso 200000/=
  4. nondo 4@ 20000/= 80000/=
  5. Ring beam 30@500
  6. kokoto 100000/=
  7. maji 50000/=
  8. madirisha mawili grill na aluminum 800000/=
  9. mlango frem na top 600000/=
  10. mlango chooni 400000/=
  11. Bati 15 @ 22000/= 330000/=
  12. Kenji mbao 2*2 na 2*4 pc 15/10 =130000/=
  13. misumali = 15000/=
  14. Blandaring mbao 15pc = 45000/=
  15. gypsum board PC 5 = 60000/=
  16. mikanda 6@4000= 24000/=
  17. rangi ndoo 30000/=
  18. gypsum powder 2bags = 30000/=
  19. white cement 1 bags 30000/=
  20. Tailizi 30square Mita = 900000/=
  21. Sinki la choo 30000/=
  22. septiki tank kuchimba na kujenga 600000/=
  23. bomba na chember moja 40000/=
  24. wirering Umeme vikorokoro vyote mainswitch,wire,switch,box,socket,bomba,breka,e/rod n.k =3000000/=
  25. kuingiza Umeme TANESCO …...…...
  26. maji dawasco........
  • MALIPO YA UFUNDI boma 450000/=
  • mbao za rinta kukodi 8@2000/= 16000/=
  • kupaua 300000/=
  • plaster na skimming 300000/=
  • fitting za Umeme 200000/=
  • FUNDI tailiz 150000/=
UKIJUMLISHA HIZO GHARAMA PAMOJA NA BALANCE YA USAFILI WA MATERIAL HADI SITE! KWA CHUMBA KIMOJA NA CHOO TU ndipo utaelewa pesa yako inatosha au haitoshi
Aisee umechambua vzr sana, nadhan akipata hyo hela akakutafuta kwa kazi kama ww ni fundi hakika hatojutia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote huwa nawashauri watu kuwa ujenzi sio kama kununua kitu dukani ambako mwenye duka anakutaka ulipie bidhaa kwa wakati mwafaka.

Una milioni tatu yako na eneo (uwanja) unao basi anza ujenzi wako hadi pale utakapoishia kisha unajikusanya tena unaendeleza kidogo kidogo hadi utafika wakati utamaliza tu.

Jambo la msingi sana hasa kwa nyakati hizi ni kuhakikisha unaanza kujenga nyumba ambayo una uhakika inaendana na kipato chako
 
Back
Top Bottom