AGITATOR
JF-Expert Member
- Apr 7, 2019
- 4,933
- 6,179
"Siku Moja mtanikumbuka, najua mtanikumbuka kwa mazuri sio kwa mabaya, kwa maana na sacrifice maisha yangu kwa ajili ya watanzania masikini". Mchina ni mkoloni ajaye hapa Africa, anatafuta kila jinsi aweke miguu yake kwa kisingizio cha kutusaidia kuwekeza. Hawana huruma kiasi hicho, kwa mwendo huu nchi hii itakuwa kama Enzi za mzee ruksa aka shamba la Bibi. RIP JPM.Na Thadei Ole Mushi.
Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma.
Wachina wana hamu na ujenzi wa Bandari hiyo kuliko hata watanzania wenyewe. Je ni kweli wachina wanatupenda kiasi hicho?
Fact
Mwaka juzi China ilianza kushikilia mashirika muhimu ya Zambia baada ya Zambia kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na China.
China ilishikilia Shirika la Utangazaji la nchi hiyo pamoja na Shirika la Umeme la Zambia (ZESCO) na bado wataendelea kutaifisha mashirika mengine kadri muda utakavyokwenda.
Huko Sri-Lanka nako wameshikilia Bandari ya nchi hiyo kwa Lengo lile lile la kulipa madeni ya China.
John Perkins kupitia kitabu chake Confession of an Economic Hit man anatufunulia jinsi sera ya Conspiracy inavyofanya kazi.
Perkins anaelezea kazi aliyokuwa akiifanya bila yeye kujua kwenye Kampuni la MAIN (Consulting and engineering Company)
Aliajiriwa kama mfanyakazi kwenye kampuni hilo ambalo ni Kampuni binafsi ila shughuli zake ziliathiriwa na mkono wa Serikali (Ujasusi) bila yeye kujua.
Kazi yake kubwa ilikuwa ni kushawishi nchi maskini zikope mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa katika nchi zao. Miradi kama vile ujenzi wa miundombinu ya Reli,Ujenzi ya Umeme ambayo utasaidiwa kukopeshwa aidha na World bank, IMF au USAID.
Perkins alikuja kugundua kuwa njia hii ya kukopesha mikopo mikubwa ambayo hailipiki ni njia mojawapo ya Taifa la Marekani kuendelea kupata maeneo ya kunyonya katika nchi maskini.
Perkins anatoa mifano jinsi alivyofanikisha kuingiza Indonesia kwenye Mtego huo na nchi nyingine nyingi.
Kwa nchi ambazo zinaendelea na zenye rasilimali kama Gesi, Madini na mafuta Marekani huwa hawalali kwenye kuhakikisha inatafuta kuwakopesha.
China nayo imeaanza kunufaika na Sera hii ya conspiracy kila mahali wanajenga ushawishi mkubwa kutoa mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa. Wanajua mikopo hii hailipiki hivyo wanaweza kunufaika wao.
Bandari ya Bagamoyo ikikamilika inafunika zote Afrika Mashariki, hivyo wateja wengi watahamia Bagamoyo ambayo itakuwa inaendeshwa na mchina baada ya sisi kukosa fedha za kumlipa mchina. Najiuliza Je China inaweza kutupenda kwa kiasi hicho? Je tunaweza kumlipa mchina?
Ole Mushi
0712702602
View attachment 1746890