Nitakuwa tofauti na Mh. Spika kuhusu hili la Bandari ya Bagamoyo

Bagamoyo lazima ijengwe.Hatuwezi kuwa wajinga tena.Mnaomshabikia mwendazake jamazeni.Someni ripoti ya CAG jinsi mabilioni yalivyopotea.Ndugai yupo sahihi kabisa.KUMBUKENI HII NI AWAMU YA SITA.

Kwa nini ujenge mradi usio na faida?
 
Kwa hali ilivyo sasa mtu pekee wa kutuepusha na "mihemuko" ya baadhi ya viongozi ni Rais wetu Mama Samia Suluhu

Kwa sasa asilimia kubwa ya viongozi wetu ni Kama wanaanza kupumua! Ni kama walikuwa na fundo limewakaba sasa wanalitoa

Hakuna ubishi kwamba awamu iliyopita Mambo mengi aliyekuwa na uwezo wa kuamua kipi kifanyike na kipi kisifanyike alikuwa ni Magufuri (RIP). Si baraza la Mawaziri wala wataalum wengine walikuwa na uwezo wa kufanya maamuzi labda wale aliowapenda yeye

Ni kweli kabisa kwamba katika aina hiyo ya maamuzi Kuna mengi yatakuwa yalienda ndivyo sivyo na wasadizi wake hawakuwa na la kufanya

Hata hivyo, pamoja na yote hayo Kama nchi hakuna sababu ya kuanza kwenda kwa pupa katika miradi mikubwa aliyoikataa kana kwamba bahari inakauka leo

Bandari ya Bagamoyo inayopigiwa chapuo na Wachina, inaweza kuwa nzuri sana!

Pamoja na uzuri huo tusibeze kasoro alizoziona mwendazake kwani hata wakati wa majadiliano alikuwepo kwenye baraza la Mawaziri Kama waziri kamili

Niimani yangu kuwa tangu akiwa waziri hakuona Kama ni kipaumbele cha kwenda nacho Kama nchi lakini kwa vile hakuwa msemaji wa mwisho alishindwa kuzuia Kama wengine walivyoshindwa kumshawishi aendelee na huo mradi baada ya kupata madaraka ya u Rais

Inawezekana ni hulka ya viongozi wetu wa ki afrika kuvutia miradi mikubwa maeneo wanayotoka hivyo tukatumia kigezo cha kutaka kumkomoa mtangulizi wake kwasababu tunaona juhudi zilizokuwa zinaelekezwa Chato, lakini hili hatutakiwi kuliweka mbele moja kwa moja tunapoangalia maslahi ya Taifa

Tunapoingia mikataba na mataifa makubwa hatuna budi kurejea history ya "establishment of colonialism in Africa" ya kidato cha tatu!

Mikataba mikubwa na mataifa makubwa yanavyoviashiria vyote vya elements of colonialism vilivyokuwepo tangu enzi hizo za wakoloni wa zamani

Kinachobadilika kwasasa ni kwamba hawa colonialists wa sasa wanakuja kisomi kwasababu wanajua hata sisi tumepiga hatua kubwa kwenye elimu

Waweke masharti wanapoanzisha mradi lakini na sisi tusiwe wanyonge kuweka masharti yetu kwasababu tunawahitaji lakini na wao wanatuhitaji pia

Tusiwe wanyonge wa kukubali kila wanachotaka wao huku wao wakikataa kila tunachotaka sisi!

Kwenye bandari ya Bagamoyo nasema tuvute subri kwanza hasa kipindi hiki ambacho viongozi wanaonekana kupumua !

Tujipe muda, tujitafakari Kama ina uharaka kiasi hicho?. Tujadili kwa pamoja Kama tuna ulazima wa bandari mpya au tuendeleze zilizopo kwanza?. Baada ya kupata majibu turudi kuangalia wao wanataka nini na kipi hakiko sawa?
 
Je, tunao ushahidi au ni propaganda kuwa Wachina wanakamata mali za nchi eti kwa kuwa nchi hiyo imeshindwa kulipa deni? Wanakamata bila makubaliano, bila matakwa ya mkataba? Leteni hiyo rasimu ya mkataba wa Bagamoyo nasi tuichambue. Kama kweli ni mbaya sisi si wajinga tutaona na tutakataa. Tusiukatae mradi kwa kuwa ni wa Bagamoyo, au ulioasisiwa na akina Kikwete, huku tukisingizia yasiyoonekana
Watu wana exaggerate. Tofauti na nchi nyingine, huu mradi hawatukopeshi bali wanajenga mradi wao nchini kwetu kwa kumsaidia a na Oman. Sasa cha kujiuliza ni jinsi gani tutafaidika.... Opportunity cost or what is the catch?

By the way, CCM Kila Siku wanadai kuwa China ni marafiki zetu... Sasa mbona hstumuamini huyu Rafiki tena?
 
Na Thadei Ole Mushi.

Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma...
Hivi hawa, mbona wanajitoa ufahamu namna hii! Kama hatuwezi kujenga wenyewe basi ni heri tusijenge kabisa, ujinga uliofanywa Zambia kamwe tusiuruhusu kwetu, ninetumiwa hizi clip mpaka nimetokwa machozi kuzitazama👇




 
Na Thadei Ole Mushi.

Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma....
Tafadhali sana Mama Samia auone huu uzi
 
Na Thadei Ole Mushi.

Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma...
Bandari ilikuwa inajengwa kwa ubia wa tati China,Oman na Tanzania wabia hawa wao wangefund pesa sisi tungetoa ardhi.baada ya mradi kukamilika kungeundwa chombo maarumu kwaajiri ya kukusanya mapato ambayo yangegawanywa kwa usawa kwa wabia wote.

Sema mwendazake kuna uwezekano alidanganywa.au majasusi wa nchi jirani walifanikiwa kuingilia kati this mission lakini kama taifa tunahitaji sana bandari ya bagamoyo before standard gauge.
 
Sawa !!Acha hawa wachina wawekeze kwenye sgr na kwenye bwawa la umeme rufiji kama alivyokwisha kuamua mwendazake magufuli maana miradi hii yote miwili hatunayo tanzania mpaka sasa."Lakini sio kuwekeza kwenye bandari ya bagamoyo maana at least tayari tunazo bandari zetu za DSM, Tanga, Mtwara.

Ujenzi wa bandari Bagamoyo utaleta ushindani usiokuwa wa lazima kwa bandari zetu zilizopo."Upigaji huu wa debe"Wa mh.Ndungai kuhusu ujenzi wa bandari bagamoyo naupinga kwa asilimia zaidi ya 500.
 
Bandari ilikuwa inajengwa kwa ubia wa tati China,Oman na Tanzania wabia hawa wao wangefund pesa sisi tungetoa ardhi.baada ya mradi kukamilika kungeundwa chombo maarumu kwaajiri ya kukusanya mapato ambayo yangegawanywa kwa usawa kwa wabia wote.sema mwendazake kuna uwezekano alidanganywa.au majasusi wa nchi jirani walifanikiwa kuingilia kati this mission lakini kama taifa tunahitaji sana bandari ya bagamoyo before standard gauge.
Kuhusu mapato kugawanywa sawa nadhani Tanzania tutapigwa tu
Kwanza ardhi kuitoa ndo kosa la kwanza
 
Kama Wschina wana Uchungu sana na Tanzania basi wawekeze kwenye Bandari ya Lindi. Kujenga bandari Bagamoyo wakati Serikali inapanua bandari ya Dar es Salaam ni dhahiri kwamba kuna jambo limejificha nyuma yake
Mkuu ulipotea sana, sijakuona kipindi kirefu kwenye platform hii. Hili la bandari limekuja kwa kasi hatari, yawezekana Msoga et al, at work. Hii remote control italitesa tena taifa, na tutarejea hukohuko kwenye miradi ya upigaji
 
Hivi mbona tunasahau ushenzi wa ndugai mapema! Huyu Matonya sii ndiyo aliyemtaka CAG Prof. Assad kwenda Dodoma kohojiwa la sivyo atapelekwa Dodoma kwa kafungwa pingu kwa kauli yake kuwa Bunge halifanyi kazi ripoti za CAG? How can we trust him.
 
Bagamoyo yetu itakuwa sasa.

Nitafurahi Sana nikiona bandari ya Bagamoyo ikijengwa.
Lazima ufurahi kwa sababu unayempigia chapuo atakupa kitu kidogo. Ngugai anatia aibu. Nafikiri tumuite bendera fuata upepo. sasa hivi anajidai kutofautiana na marehemu, wakati wakati huo angeombwa chochote na marehemu angetoa. it pains to see opportunists like Ndugai.
 
Acha WIVU na bagamoyo.
Lazima ufurahi kwa sababu unayempigia chapuo atakupa kitu kidogo. Ngugai anatia aibu. Nafikiri tumuite bendera fuata upepo. sasa hivi anajidai kutofautiana na marehemu, wakati wakati huo angeombwa chochote na marehemu angetoa. it pains to see opportunists like Ndugai.
 
Mjadala huu ungenoga zaidi kama huo mkataba mzima ungewekwa katika tovuti ili kila anayependa ausome; kisha tufanye debate sisi wazalendo tunaopinga huu mradi na wale wanaounga mkono huu mradi.

Inasikitisha mradi mbovu kama huu ambao naamini pengine hata chifu Mangungu asingeukubali lakini leo hii unatetewa na watu ambao ni wasomi! Hivi nini kifanyike ili somo la uzakendo liwaingie watanzania wote?
Hapa umeongea la msingi sana maana sasa hivi imekua ngumu sana kuamini maneno ya wanasiasa baada ya report ya CAG
 
Sijawahi kumuona huyo jamaa kama ni smart...sijui why anashikilia ofisi kubwa hivi...I don know
 
Muda umefika wauweke wazi mkataba nasi tuusome..tuweze kutoa maamuzi..sio kuwasikia wao KILA siku
Mkataba huja baada ya makubaliano. Kilichopo sasa ni mapendekezo ya mwekezaji na majibu ya serikali. Ukitaka mkataba subiri pale watakapowekeana sahihi.
 
Back
Top Bottom