Furaha yakweli na pumziko la kweli linapatikana kwa Yesu kristo pekee wala hakunamwingine awezaye kukupa furaha. ili upate furaha hii unapaswa kwanza kutambuakila mwanadamu kwa kuzaliwa na kutenda nikiwemo na mimi, sisi ni wenye dhambi,(zbr 58.3, 51.5), Warumi 3.23, 5.12). Biblia inasema hakuna mwenye haki hatammoja hivyo sisi wote ni wenye dhambi kwa kuzaliwa na kutenda? tujiulize sotemtoto mdogo unakuta ana wivu, chuki, hasira, choyo, hucheza dansi/muziki bilakufundishwa kwann? hii yote hutokana na dhambi ya asili. Baada ya mtu kuzaliwana kupata akili ndipo anaanza kufanya dhambi zingine kama wizi, uzinzi,uasherati, utukanaji, ulevi, uchawi,uganga wa kienyeji n.k.
Lazima tujue na tukubaliane kuwa hakuna mwanadamu hata mmoja aliyewahi kuishiduniani bila kufanya dhambi isipokuwa YESU KRISTO PEKEE, ndiyo maana sehemunyingi Yesu aliwauliza watu aliowahi kuishi nao na wale aliokuwa nao je ni nanianayenishuhudia kuwa mimi ni mwenye dhambi, hakuna hata mmoja wao aliyewezakunyoosha kidole kuwa alifanya dhambi yoyote katika maisha yake.
Tukijua kweli hii tujue Yesu kristo aliteswa, kusulubiwa na kufa kwa ajiliyetu, damu yake iliyomwagika msalabani inatosha kabisa kutusafisha dhambi zetutukiamini. Cha msingi tuache kujihesabia haki kuwa sisi ni wema sana natumefanya hili na lile (kusali sana, kutoa sadaka nyingi, kujenga majengo yaibada n.k.) tukumbuke wokovu unakuja kwetu kwa neema tu yaani kwa upendeleowala si kwa matendo yetu. Wewe jiulize tunao viongozi wengi wa dini na watuwote wana dini lakini je wana uwezo wa kushinda dhambi? mbona bado tunamajambazi, wazinzi, waasherati, watukanaji na waovu wa kila aina pamoja na kuwatuna dini. katika hili tunajifunza hakuna dini yoyote hata ya kuzaliwa iliwahikumpa mtu uwezo wa kushinda dhambi isipokuwa Yesu Kristo pekee. Ndugu yangutena watu wa dini ni wabaya sana na ndio waliomkamata Yesu kristo, wakampiga,wakamtemea mate, wakamdhihaki, wakamsulubisha na kumtundika pale juu msalabani.Naamini ndugu yangu hata wewe una dini lakini jiulize mwenyewe je una uwezo wa kushindadhambi? jibu ni hapana kwa herufi kubwa
Ndugu yangu ili tupate wokovu tunapaswa kuiamini kazi aliyoifanya Yesu Kristopale juu msalabani na kuamini kuwa damu yake inatosha kutusafisha dhambi zetu.kisha tunatakiwa tutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha ndipo tutapatawokovu au rehema(mithali 28.13). Tukishatubu dhambi zetu kwa kumaanishakuziacha tunasamehewa dhambi zetu na kuoshwa kwa damu ya Yesu kristo nakufanyika kuwa watoto wa Mungu(luka 1.77, Luka 10.19, mathayo 1.21, Yohana1.12). Tukishafanyika kuwa watoto wa Mungu tunapewa uwezo wa kushinda dhambizote ndiyo maana hata watu wanaokujua watakushangaa na kuona mbona si yulewaliyemjua na waliyeongea naye jana. Je uko tayari kuokoka? najua uko tayarikuokoka? Basi nakusihi ufuatishe sala hii kwa dhati kabisa kutoka moyoni- MunguBaba, nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi kwa kuzaliwa na kutenda, natubu dhambizangu zote kwa kumaanisha kuziacha, naomba ulifute jina langu katika kitabu chahukumu na kuliandika katika kitabu cha uzima mbinguni, nipe uwezo wa kushindadhambi na kufanyika mtoto wako, nioshe kwa damu ya Yesu kristo dhambi zanguzote, asante kwa kunisamehe na kunifanya kuwa mtoto wako katika jina la YesuKristo,Amen.
Nami ninakuombea-Mungu wangu ninakusihi na kukuomba umsamehe mtu huyu dhambizake zote za kuzaliwa na kutenda, msafishe kwa damu ya Yesu Kristo na umpeuwezo wa kushinda dhambi na kumfanya kuwa mtoto wako, ulifute jina lake katikakitabu cha hukumu na uliandike kaika kitabu cha uzima, asante kwa kumsamehe nakumpa uwezo wa kushinda dahmbi katika jina la Yesu Kristo, Amen.
Ndugu yangu hongera kwa uamuzi wako mzuri ambao hautaujutia,Hongera kwa kuwakama umeifuatisha sala hii kwa dhati kabisa kutoka moyoni tayari umeokoka nakufanyika kuwa mtoto wa Mungu, Mbinguni kuna furaha kuu kwa uamuzi wako waBusara wa kuokoka kwani umeushinda uongo wa shetani anaoutumia kuwadanganyawatu kuwa haiwezekani kuokoka duniani wakati wanaimba kila siku katika ibadazao kuwa usinipite mwokozi na hata Yesu Kristo alipoingia nyumbani kwa Zakayoakiwa duniani alimwambia zakayo leo hivi wokovu umefika nyumbani mwako (mathayo1.21, Yohana 8.44, luka 10.19). Ili uweze kukua katika wokovu na imani,ninakushauri utafute kanisa linalohubiri wokovu upate kujiunga na kusali pamojanao, watakufundisha jinsi ya kuenenda katika mapenzi ya Mungu na hatimaye uwena nafasi ya kuingia mbinguni(zaburi 119.6,9). Mungu wa Milima na Tambarareakubariki kwa uamuzi wako wa busara na kukufanikisha katika kila jambo kadriunavyoitii sauti yake
Mungu akubariki