Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,399
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
 
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
 
Yaani umekopeshwa badala ya kujipeleka mwenyewe ukalipe deni la watu unamgeuzia kibao aliyekukopesha eti kwa nini hakuja kukudai.

Hizi tabia watanzania wengi wanazo ndio maana hata taasisi za fedha hukataa kukopesha watu na wakikopesha hulipisha riba kubwa za kuua mtu sababu ya usumbufu wa watu kama huyu mleta mada.Mkopo ukipewa unatakiwa uulipe bila shuruti wala kumsumbua mkopeshaji.Hiyo kesi umeshindwa kabla hata ya kuipeleka mahakamani.Na hapa umejianika kuwa ni mkopaji jeuri usishangae ukienda kukopa taasisi za fedha wakakugomea kukupa mkopo hata wa shilingi mia.
 
waburuze tu,maana hawajielewi..wanachukua majina mfukoni ili kumridhisha mkuu wa kaya..wanawaacha wahusika na kuwaandika wasiohusika
 
kUNA jAMAA NIKO ANAKATWA NA BODI WAKATI HATA HIYO BODI HAIJAWAHI KUMPA HATA BUKU
 
Kwahiyo unalalamika kwanini hawakukati? Kwanini hawajatoa jina lako?

Lakini si utaulizwa ulichukua hatua gani ulipogundua haukatwi tangu 2012?

Halafu hilo jukwaa la walimu na wanafunzi ndiyo nalisikia leo.

Ila nenda kwa wanasheria/ mawakili wanaweza wakakuonesha katika hilo swala lako kama una locus stand au ndiyo utakua case study Tanzania nzima.
 
Hata mimi ntawaburuza mahakamani. Mi nlikopeshwa na wizara ya elimu ya juu sayansi na teknolojia.... bodi ya mikopo haijawahi kunikopesha.

Ntamlipaje mtu ambaye hajanikopesha?? Hakuna makubaliano yoyote tuliyongia na hii bodi. Bodi imeanzishwa mi nikiwa uraiani tayari nakula vya kwangu.

Naombeni namba za Tundu Lissu
 
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
Ni jukumu la Nani kufatilia wanaodaiwa na bodi ?
 
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016

Tumekusikia ila lipa kwanza deni mtoto Wada jarani yangu asome nae.

Ulikuwa wapi kwenda kuwaambia hayo miaka yote
 
deo umehamia jf??!!

kwa wasiemjua kafatilieni post zake kule fb halafu mtajua mnapaswa kujibu nini.
 
Serikali ndo imeniajiri na wao ndo wananilipaaa mishahara yangu inapitia kwao

Kwann wasichukue hela yao??

Mbona kuna watu wamekatwa directly bila kupeleka taarifa zao??

Halafu wanapiga watu penalty hovyo kabisa,
 
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
Mhhh Ha ha ha haaaaa Deogratius Kisandu acha mbwembwe, haina haja ya kutueleza hayo, ww nenda mahakamani fungua mashtaka, sisi inatusaidia nini?
 
Back
Top Bottom