Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
UUNGWANA NI MATENDO; PALE ULIPOONA MWAJIRI HAKUKATI KAMA USEMAYO YANATOKA MOYONI, BASI ULITAKIWA KUMKUMBUSHA tena kwa maandishi. hiyo labda mdio ingelikuwa salama kwako huko mahakani unakotaka kuenda. kinyume chake wewe kama wale,.
 
Rudi ukasome mkataba wako, kama kuna kipengele kinasema kudaiwa kuna ukomo ....nenda mahakamani, lakini kama hakuna, jikusanye ulipe.
 
Mhhh Ha ha ha haaaaa Deogratius Kisandu acha mbwembwe, haina haja ya kutueleza hayo, ww nenda mahakamani fungua mashtaka, sisi inatusaidia nini?
Kama haikusaiidii kitu na hainafaida kwako ume comment ili iweje kama sio kiherehere, uniona haikufai pita kimyakimya. Au unataka na wewe uonekane upon?
 
Yaani umekopeshwa badala ya kujipeleka mwenyewe ukalipe deni la watu unamgeuzia kibao aliyekukopesha eti kwa nini hakuja kukudai.

Hizi tabia watanzania wengi wanazo ndio maana hata taasisi za fedha hukataa kukopesha watu na wakikopesha hulipisha riba kubwa za kuua mtu sababu ya usumbufu wa watu kama huyu mleta mada.Mkopo ukipewa unatakiwa uulipe bila shuruti wala kumsumbua mkopeshaji.Hiyo kesi umeshindwa kabla hata ya kuipeleka mahakamani.Na hapa umejianika kuwa ni mkopaji jeuri usishangae ukienda kukopa taasisi za fedha wakakugomea kukupa mkopo hata wa shilingi mia.
Sio sawa!
watu wote waliokuwa wakikatwa na bodi kupitia mishahara hawakujisalimisha!
hata contract ya bodi na mwanafunzi haikuwa na kipengele hicho!
nadhani serikali ina hamu ya kulipa fine tu kwa haya makusanyo yao!
kuna mtu anaaiingiza cha kike, labda wamepanga deal!
katika mikopo huwa kuna grace period, lkn hata mikopo hii contract yake ilitaka akatwe mtu mwenye ajira, hata hao sugu unaweza ukakuta kuwa nao ni wakosa ajira sugu!
 
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
Uzuri kesi za madai hazina kifungo ........ hata hawa Bodi ya mikopo wanahangaika kutisha watu tu!!

Badala ya kutishia wahamasishe watu!!
 
Back
Top Bottom