Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

Nitaiburuza bodi ya mikopo mahakamani

Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
Anatafuta kiki tu hapa, mda wote tangu amalize wakati anaona anadaiwa kwa nini hakuitaarifu bodi ya mikopo waanze kumkata hela yao
 
Hahahaa... mie nilidhani ataiburuza bodi mahakamani kwa kumwita mdaiwa sugu wakati hawajawahi kumkopesha.

acha mbwembwe za kutafta kiki... we kalipe tu deni lao.
 
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
Ndio uone akili za mawakala wenu
 
Tumekujua, ngoja tukufate hukohuko utueleze kwanini hujalipa deni hadi sahivi mpuuzi mmoja wewe
 
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe
Kbsa Mkuu,nilifikiri unataka kasema wanakukata kimakosa,km wafanyakazi baadhi wanakatwa kwa makosa
 
Yaani umekopeshwa badala ya kujipeleka mwenyewe ukalipe deni la watu unamgeuzia kibao aliyekukopesha eti kwa nini hakuja kukudai.

Hizi tabia watanzania wengi wanazo ndio maana hata taasisi za fedha hukataa kukopesha watu na wakikopesha hulipisha riba kubwa za kuua mtu sababu ya usumbufu wa watu kama huyu mleta mada.Mkopo ukipewa unatakiwa uulipe bila shuruti wala kumsumbua mkopeshaji.Hiyo kesi umeshindwa kabla hata ya kuipeleka mahakamani.Na hapa umejianika kuwa ni mkopaji jeuri usishangae ukienda kukopa taasisi za fedha wakakugomea kukupa mkopo hata wa shilingi mia.
Hoja yako iko wapi sasa? Huoni kwamba kitendo chako cha kukaa kimya bila kuitaarifu bodi ni kosa kisheria? Yaani ukienda tu Mahakamani basi ujue umejimaliza mwenyewe

Sina hakika kama hata mnaelewa namna haya mambo yalivyo.

Ngoja nijaribu kuwaelewesha;

1. Kwanza mtoa hoja yuko sahihi na akienda mahakamani wala hatakuwa amejinyonga (Lizaboni)

2. Utaratibu tangu kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu ni kuwa unakopeshwa kugharamia elimu yako na baadae ukiingia ktk soko la ajira basi, sheria inamwelekeza aliyekuajiri kuhakikisha inamkata sehemu ya mshahara huyu mtumishi kulipia deni la mkopo wake wa elimu. Kwa sheria ya sasa iliyopitishwa juzi inasema ni 15% ya mshahara utakaokuwa unapata.

3. Mechanism ya kulitekeleza hili ni mara uajiriwapo aidha taasisi binafsi ama ya umma, sharti ujaze fomu za mkataba wa ajira na ndani kuna kipengere kinachokutaka ueleze iwapo wewe ni mnufaika wa mkopo wa Elimu ya juu.

Hii maana yake ni kumfanya mwajiri wako aanze kukata makato ya huo mkopo na kupeleka kwa mwenyewe i.e HESLB

4. Hii inaweza kuwa ni kosa tu kwa mwajiriwa kama atatoa taarifa ya uongo (kumdanganya mwajiri) kwamba hawajawahi kunufaika na mkopo wa HSELB wakati ukweli ni mnufaika.

Katika hili nina hakika Deogratius Kisandu aliliweka wazi na ndiyo maana anapata guts za kwenda kuishitaki bodi ya mikopo. Na hapa si tu bodi ina shida bali mwajiri wake atakuwa na matatizo iwapo mlalamikaji atathibitisha kuwa hakuwahi kukana kuwa ni mnufaika wa mikopo ya Elimu ya juu!!

6. Nadhani Kisandu haendi mahakamani kwa sababu tu anataka aanze kulipa mkopo wake, bali lengo lake ni kukumbusha watu na taasisi mbalimbali i.e bodi yenyewe na waajiri kutekeleza kwa ufasaha na kwa wakati majukumu yao waliyopewa kufanya!!
 
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
Jina lako halipo ktk orodha iliyotolewa kwa hiyo kinachokuwasha ni nini.Kesi hii haikuhusu kabisa.
 
Huyu Jamaa kaweka vyeti vyake vyote kuanzia vya clinic mpaka vya chuo kule FB. eti anawathibitishia bodi..sijui anathibitisha nini sasa.
nafikiri atakuwa amerukwa na akili.
mimi nimemsikitikia tu.
 
6. Nadhani Kisandu haendi mahakamani kwa sababu tu anataka aanze kulipa mkopo wake, bali lengo lake ni kukumbusha watu na taasisi mbalimbali i.e bodi yenyewe na waajiri kutekeleza kwa ufasaha na kwa wakati majukumu yao waliyopewa kufanya!!

Kazi ya kufuatilia deni kama limekatwa na limefika bodi kwenye akaunti ya mhusika ni la muhusika mwenyewe.Alitakiwa yeye kama mnufaika wa mkopo aangalia pay slip yake kama deni linakatwa.Kuona hakatwi miaka yote na akakaa kimya ina maana yeye binafsi na mwajiri wake walikula njama za pamoja za kutokulipa hilo deni.Kama ni kesi wote wawili wana kesi ya kujibu.Mwajiri na mwajiriwa.
 
Jina lako halipo ktk orodha iliyotolewa kwa hiyo kinachokuwasha ni nini.Kesi hii haikuhusu kabisa.

Tatizo lako umeona "kuwashwa" kwa jamaa tu bila kuona mantiki (logic) iliyomo ndani ya kusudio lake hilo!

Mimi nimeiona. Nisome hapo juu ktk quatation yangu kwa Lizaboni & Yehodaya unaweza kuelewa kitu.
 
Kazi ya kufuatilia deni kama limekatwa na limefika bodi kwenye akaunti ya mhusika ni la muhusika mwenyewe.Alitakiwa yeye kama mnufaika wa mkopo aangalia pay slip yake kama deni linakatwa.Kuona hakatwi miaka yote na akakaa kimya ina maana yeye binafsi na mwajiri wake walikula njama za pamoja za kutokulipa hilo deni.Kama ni kesi wote wawili wana kesi ya kujibu.Mwajiri na mwajiriwa.

Hapana, mnufaika hana kosa lolote kwani aliliweka clear ktk mkataba wake wa ajira.

Unless tukubaliane tu kwamba mwajiri ndiye mwenye makosa kwa kushindwa kutekeleza anayopaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa sheria!

Who knows? Inawezekana labda walikuwa hawajaamua kuanza kukata fedha zao ambayo mimi (mwajiriwa) kwa maandishi ya mkataba nilishatoa idhini waanze kuchukua za kwao....
 
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
Nasikitikia jukwaa unaloongoza. .. Duniani mambo yamejizingira katika vitu viwili, namely haki na wajibu... Ulikuwa na haki ya kupata mkopo so unawajibika kuulipa.. Katika form ya mkataba ulisoma popote kuwa utafuatwa ili kurudisha mkopo? Kama jirani anakudai na hajakufuata huwezi kupeleka malipo mwenye... Um sorry for our kids kama walimu mnathink along those lines
 
Tatizo lako umeona "kuwashwa" kwa jamaa tu bila kuona mantiki (logic) iliyomo ndani ya kusudio lake hilo!

Mimi nimeiona. Nisome hapo juu ktk quatation yangu kwa Lizaboni & Yehodaya unaweza kuelewa kitu.
Issue ya accountability kwa Taasisi ni moja na kuhakikisha kuwa mkopo unalipwa Bodi ya mikopo toka kwa mkopeshwaji ni mbili.

Kwenda mahakamani sijui ni kufungua shauri gani?
 
Unless tukubaliane tu kwamba mwajiri ndiye mwenye makosa kwa kushindwa kutekeleza anayopaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa sheria!

Mwajiri na bodi ya mikopo hawajawahi sainiana mkataba popote.Bodi inayemtambua ni yule waliyesaini naye mkopo ambaye ni mkopaji.Ndio maana bodi inasema itawaburuza mahakamani wakopaji kwani ndio ilioingia nao mkataba.Huyo mwajiri wanajuana naye wenyewe.Na si wote wanapeleka pesa zao za kulipa deni kupitia mwajiri wengine hupeleka wenyewe kwani wamejiajiri au wameamua tu kulipa wenyewe.

Bodi haina mahali imesaini na waajiri mkataba.Mkataba ni kati ya bodi na mkopaji.
 
Wewe ndio maana ulifukuzwa kwenye chama chetu, ukienda mahakamani kama mimi ndio jaji/hakimu nakuitia polisi wakusweke lupango maana sheria ya bodi ya mikopo inasema kabisa ukipata kazi ni lazima utoe taarifa bodi ili waanze utaratibu wa kukukata.
 
tehe tehe tehe kweli HELSB wameleta kizaazaa
 
mkuu ina onekana unalipwa pesa mingi subiri Magu akupunguzie unajisifia mtumishi wa umma utakatwa hadi kodi ya kuendesha gari kwenye barabara za lami
 
wa
NITAIBURUZA MAHAKAMANI BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KWA UZEMBE WA KUTONIKATA MAKATO YA MAREJESHO YA SHAHADA NILIYOSOMA

Mimi Deogratius Kisandu, nasema kuwa; Yai ukililea vizuri litazaa Kuku lakini yaani Ukililea vibaya litazaa yai vinza. Kwanza kabisa natumia fursa hii kumshukru Mungu kusoma kwa miaka mitatu Shahada ya Elimu Maalum katika Chuo Kikuu Kishirki cha Sebastian Kolowa, Chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (Sekuco), kwasasa kinaitwa Sebastian Kolowa Memorial University(Sekomu). Kwa kipindi chote cha masomo nimelipiwa na Bodi ya Mikopo elimu ya juu, nikipewa mkopo kwa 70% kipindi chote cha masomo kuanzia mwaka wa masomo 2009/2010 mpaka 2011/2012 ambapo nilihitimu huko Lushoto, Tanga.

Chakushangaza kila aliyeingia kwenye ajira alianza kukatwa mara moja na wengine walichelewa baada ya mwaka mmoja walianza kukatwa na hata Salary Slip zao zinaonesha kuwa wanakatwa tena hii ilikuwa ni automatic bila hata kupewa taarifa. Leo tunashangaa kutangaziwa kuwa tujisalimishe, kivipi ili hali kwasisi ambao ni watumishi wa Umma tayari majina yetu yapo kwenye system ya Utumishi na kwa mantiki hiyo, sisi hatuhusiki bali mwajiri wetu ndio anawajibika kwa kutokutoa taarifa ya watumishi wake kila mwaka katika bodi ya mikopo.

Mimi nachoshangaa, jina langu hata kwenye Orodha ya wadaiwa Sugu halimo na ilihali ninadaiwa na sijaanza kukatwa tangu nimalize chuo mwaka 2012, lakini wenzangu wanakatwa makato ya kurejesha mkopo bila hata kupewa taarifa yoyote. Kwanini jina langu lisionekane na wakati natakiwa kulipa mkopo au mnasubiri nikikaribia kustaafu ndio mtoe jina langu ili mje mnikate vizuri kwenye mafao ya kustaafia? Kwa hili natangaza rasmi kuishitaki Bodi ya Mikopo elimu ya juu mahakamani. Mimi sitajisalimisha Ofisi zao bali bodi itajisalimisha mahakamani, naendelea kutafta msaada wa kisheria zaidi ili kuweka mambo sawa. Namba yangu ya Chuo ni Sek/BedSN/130/09-KISANDU DEOGRATIUS PIO.

Kwa niaba ya wahangaa wenzangu nimejitoa sadaka kutetea Utu wa Watumishi wa Umma wanyonge tulionyongwa kifikra.

Deogratius Kisandu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

17/11/2016
wacha kujishebedua. kwa nini hujawas hitaki hadi wao wameanza kutoa orodha ya wadaiwa sugu. wee jisalimishe ulipe
 
Back
Top Bottom