Kwani Mpendazoe bado yupo?Sio kama, ndio ukweli wenyewe!, kama ilivyo kwa Ubungo nako wanatoka mkoa fulani.
My Take.
Mtatiro anachagulika zaidi kuliko Mpendazoe!.
Mtatiro ni born and breed in opposition, Mpendazoe ni CCM aliyepotezwa maboya na CCJ, akajiunga Chadema because he had no option!, na amino nawaambie saa hizi anajuta!, anatamani kurudi zake CCM, ndio maana hasikiki kabisa katika harakati!, hivyo kama ni kweli bado ana nia na opposition, ashauriwe aende Kishapu. Jimbo la Segerea ni la Mtatiro!.
Kwa majimbo ya Dar es Salaam, karibu yote yatakwenda UKAWA isipokuwa Ilala! na Kigamboni!.
Pasco.
Kwa vile siku hizi wanasiasa wana hama kwa kujitangaza, Mpendazoe bado yupo Chadema kwa vile hajatangaza vinginevyo!, ila ukimya wake tuu ndio unanishangaza na kunipa maswali bila majibu!.Kwani Mpendazoe bado yupo?
Julius Mtatiro
Umeandika mambo ya msingi sana isipokuwa moja tu la idadi ya mitaa tuliyoshinda UKAWA uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kwa majimbo ya UKONGA na SEGEREA.
Kumbukumbu nilizo nazo zinaonyesha kama ifuatavyo:
UKONGA:
CHADEMA MITAA 10 (WENYEVITI)
CUF MITAA 4 (WENYEVITI)
SEGEREA:
CHADEMA MITAA 16 (WENYEVITI)
CUF MITAA 11 (WENYEVITI)
Kwa Majimbo yote mawili msimamo upo hivi:
CHADEMA MITAA 26
CUF MITAA 15
Sasa hiyo mitaa 33 unayoisema sijui umeipata wapi kiongozi na kwamba cuf ndiyo ina mitaa mingi kuliko Chadema nalo sio kweli hata kidogo.
Ni muhimu ukapitia upya kumbukumbu zako ili kuondosha mkanganyiko na upotoshaji uliotokea ktk mabandiko yako.
Hapo sasa unatetea kwa uongo ili uonekane ukweli,Segerea CDM ilipata viti vingi vya mitaa uchaguzi uluopita kuliko CUF. Tetea wewe kuwa na sifa za kuteuliwa kupitia UKAWA,lakini usitake kutaguta sifa kwa kusema uongo ilhali hata kwenye uchaguzi wenyewe hukushiriki hata kwenye harakati kusaidia kupata hivyo viti vya serikali za mitaa.Ndugu yangu JAKACKSERU,
Hata hiyo UKONGA ina wagombea wazuri tu wa CHADEMA akiwemo Kamanda Mwita Waitara, ngoja tusubiri kujua UKAWA inagawanaje majimbo ndipo tutahitimisha masuala haya. Lakini kwa namna nilivyojipanga sitakuwa na kinyongo kumuunga mkono mgombea yeyote wa UKAWA ikiwa atapitishwa kugombea Segerea.
Sina tabia ya kupigania madaraka kwa sababu najua kuna masuala mengi ya kufanya kuliko kuongoza. Jambo la msingi ni kuwa UKAWA itapata mgombea imara SEGEREA. Wana Segerea wameichoka CCM na wanahitaji kiongozi imara zaidi, ukiongea nao wanakueleza hawachagui chama, watahitaji kuwa na kiongozi imara kutoka chama chochote kati ya vyama vyetu na kwamba huyo ndiyo chaguo lao. Mimi ni mmoja wa watu wanaohitaji ridhaa hiyo na wapo wenzangu, sote tutapimwa, atakayepitishwa tutampigania.
Na jambo la mwisho unalopaswa kujua ni kuwa vyama vya CHADEMA na CUF vinahitajiana mno UKONGA na ukiangalia hata matokeo ya serikali za mitaa utagundua kuwa kati ya mitaa takribani 33 ya UKAWA, CUF ndiyo ina mitaa mingi. Hii ndo hali ya kisissa ya sasa. Lakini CUF kuwa na mitaa mingi SEGEREA mwaka 2014 au CHADEMA kupata kura nyingi za ubunge mwaka 2010 siyo hoja ya vyama hivi viwili kuweka u-vyama wao mbele na kusahau ushirikiano.
UKAWA ikiweka mgombea mmoja Segerea itashinda kwa kishindo. Ikivurugana na kila chama kikajiwekea mgombea sote tutaanguka.
Ni hayo tu.
J. Mtatiro.
NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.
Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.
Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.
Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.
Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.
Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.
Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0
Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com
Mmeanza kunyukana mapema na sasa mnabishana nani ana mitaa mingi na nani hana, mwisho wa siku kila mmoja atataka kusimama kivyake na huo ndio utakuwa mwisho wenu.
Kwa majimbo yote CCM imeshinda kwa % ngapi vs UKAWA?
Hiyo profile kama inanihisu, ila Mtatiro hapawezi segerea inamfaa Mpendazoe
hivi kawaidsa yake ndo ikoje...kurun away na wasanduku ya kura?Unajisumbua bure. Ccm kisiki cha mpingo itachukua jimbo hilo kama kawaida yake
Hakuna minyukano yoyote hapa, kinachotokea ni kuwekana sawa tu ili kila mmoja afahamu na kutambua nani ni nani katika majimbo haya mawili ya Segerea na Ukonga.
Lakini pia hii ni kumsaidia ili apate takwimu sahihi mapema ili ikitokea amekabidhiwa kijiti cha UKAWA awe anafahamu ni kwa kiwango gani Ukawa ina support ya wananchi katika jimbo husika.
Kwani kuna mtu wa CDM kajitokeza kugombea Segerea?