Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

hilo jimbo ni laini kama maini
ukishidwa hapo tena basi
 
Kwahyo chadema hawataki wanaUKAWA wa vyama vengine wajitokeze? mana ukweli ni kwamba wamemmind mtatiro kujitokeza.
 
Segerea ni ngome ya chadema sasa CUF inakuaje tena???? CUF wakumbuke maazimio ya UKAWA.
 
Pamoja sana Mkuu...Mtatiro...Naweza kusema jambo moja Inatakiwa HEKIMA yakutosha kwa Viongozi wa UKAWA kwasababu kwenye kupitisha wagombea Kutakuwa na changamoto kubwa sana hasa maeneo ambayo miongoni mwa vyama vimeweka mizizi...
 
Safi sana hapo upele umepata mkunaji nina hakika sasa yule mwizi wa masanduku hato rudi tena.
 
Sasa ninaanza kuamini kwamba kweli huu MUUNGANO wa UKAWA hautafika popote kabla ya kuvunjika na kusambaratika kwasababu ya UROHO wa madaraka!

Kama Viongozi wa juu wa vyama kama huyu Julius Mtatiro hawajui hata makubaliano yanayounda umoja wa UKAWA kuhusu kuachiana majimbo, Je wanachama wengine hali itakuwaje?!

Nitataja makubaliano mawili tu ya UKAWA kuachiana majimbo, ambayo nilikuwa nafikiri yatakuwa kwenye finger tips za Julius Mtatiro. Make no mistake I have nothing against Mtatiro, lakini ninasimamia principles.

Makubaliano No 1. Majimbo yote yanayongozwa na chama kinachounda UKAWA. Chama hicho ndiyo kitakuwa na jukumu la kumteua mgombea atakayepeperusha bendera ya UKAWA. Maana yake nini? Majimbo ya Ubungo, Kawe CHADEMA ndiyo kitakuwa na jukumu la kumteua mgombea atakayepeperusha bendera ya UKAWA. Vivyo hivyo kwa Kasulu NCCR Mageuzi, Wawi CUF etc

Makubaliano no 2. Majimbo ambayo yanaongozwa na CCM, ambapo 2010 vyama vinavyounda UKAWA vilisimamisha wagombea, chama kilichoshika nafasi ya pili nyuma ya CCM ndiyo kitapewa jukumu la kumteua mgombea atakayepeperusha bendera ya UKAWA. Maana yake nini? Katika Jimbo la Segerea 2010 chama kilichoshika nafasi ya pili nyuma ya CCM ni CHADEMA. Hivyo kutokana na matokeo hayo Chama chenye Jukumu la kumteua mgombea wa UKAWA ni CHADEMA sio CUF ya Julius Mtatiro, kama makubaliano hayo yatafuatwa kama yalivyo.

MAONI YANGU. Kama kweli viongozi wa UKAWA wako serious na muungano huu, inabidi watoe/waweke wazi makubaliano hayo kwa wanachama na wapenzi wao nchi nzima, mapema sana iwezekanavyo ili kuondoa chaos. Kama kiongozi wa juu kama Julius Mtatiro hajui hayo makubaliano, huko kwenye majimbo kwenye wanachama wa kawaida hali iko je, itakapofika wakati wa kuachiana majimbo. Tatizo viongozi wa nchi hii huwa hawa learn through history, hali hii ilitakiwa kushugulikiwa mapema tu na UKAWA, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ilishaanza kujitokeza.

Pili viongozi wa UKAWA wanatakiwa ku stick kwenye makubaliano yanayounda UKAWA bila kuangalia SURA YA MTU au WADHIFA wa mtu katika kutekeleza makubaliano waliyojiwekea. Kama wakianza kuhamisha post za magoli eti kwasababu huyu ni Mtatiro, Ben Saanane (no offense intended), make no mistake hawatafika popote. Mind you CCM is watching you, kwasababu kusambaratika kwa UKAWA ndiyo KARATA ya mwisho itakayowaokoa CCM.

You can just ignore my plea/advise at your own peril, But you have been warned!

Kama Kamanda Julius Mtatiro ataamua kuhamia CDM sidhani kama kutakuwa na tatizo...Na inawezekana ndiyo plan yake ndiyo maana katangaza nia mapema, haiwezekani katibu wa UKAWA asijui makubaliano yao
 
Last edited by a moderator:
Kila la kheri my dear comrade Julius Mtatiro....Natumaini UKAWA hawatafanya makosa kukuacha watu kama ninyi mnahitajika sana Bungeni kupambana na wezi wa nchi hii...
 
Mtatiro hapa umenipa mashaka makubwa sana kutangaza nia kupitia ukawa ndani ya jimbo ambalo unajua chama chenye mizizi segerea ni chadema na pia kama kiongozi ndani ya cuf na ukawa unatumia data za uongo za matokeo ya serikali za mitaa kuhalalisha matakwa yako binafsi ili kuhadaa na kupotosha umma imenipa mshtuko mkubwa na hofu kutokana na mtu anayefanya ivi ndio watu tunaoamini wanaibeba ukawa lakini matendo yanakuwa tofauti. Si dhambi alichofanya mtatiro,hofu ni data za uongo anazotumia kupotosha je safari ya ukawa ipo salama chini ya mtu kama mtatiro ambaye uaminifu kwake ushaanza kushuka sana
 
Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa cuf ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la segerea bw.juliu mtatiro

source:nipashe
 
sasa na yule mpendazoe atagombea wapi??

UKAWA msije kujilipua mapema
 
Back
Top Bottom