NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA DAR ES SALAAM.
Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.
Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.
Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.
Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.
Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.
Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0
Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com
tunataka mabadiliko!!! hizo zingine mbwembwe!!
Unajisumbua bure. Ccm kisiki cha mpingo itachukua jimbo hilo kama kawaida yake
Jimbo la Mpendazoe hilo.
Yatakukuta yaleyale ya Ubungo, ulirukia jimbo ambalo Mnyika alikuwa kajipanga kwa muda mrefu, it's like hilo. Mpendazoe kajipanga muda mrefu na anafahamika na kasikia
Sasa wewe miezi 6 unataka jimbo?
Hilo jimbo kama la watu toka mkoa fulani hivi!
Changamoto za wananchi ni mengi sn je umeshiriki vipi kuzitatua au watu wanasubiri mpk upate uongozi ndiyo uzitatue
Changamoto za wananchi ni mengi sn je umeshiriki vipi kuzitatua au watu wanasubiri mpk upate uongozi ndiyo uzitatue
Ndugu yangu JAKACKSERU,
Hata hiyo UKONGA ina wagombea wazuri tu wa CHADEMA akiwemo Kamanda Mwita Waitara, ngoja tusubiri kujua UKAWA inagawanaje majimbo ndipo tutahitimisha masuala haya. Lakini kwa namna nilivyojipanga sitakuwa na kinyongo kumuunga mkono mgombea yeyote wa UKAWA ikiwa atapitishwa kugombea Segerea.
Sina tabia ya kupigania madaraka kwa sababu najua kuna masuala mengi ya kufanya kuliko kuongoza. Jambo la msingi ni kuwa UKAWA itapata mgombea imara SEGEREA. Wana Segerea wameichoka CCM na wanahitaji kiongozi imara zaidi, ukiongea nao wanakueleza hawachagui chama, watahitaji kuwa na kiongozi imara kutoka chama chochote kati ya vyama vyetu na kwamba huyo ndiyo chaguo lao. Mimi ni mmoja wa watu wanaohitaji ridhaa hiyo na wapo wenzangu, sote tutapimwa, atakayepitishwa tutampigania.
Na jambo la mwisho unalopaswa kujua ni kuwa vyama vya CHADEMA na CUF vinahitajiana mno UKONGA na ukiangalia hata matokeo ya serikali za mitaa utagundua kuwa kati ya mitaa takribani 33 ya UKAWA, CUF ndiyo ina mitaa mingi. Hii ndo hali ya kisissa ya sasa. Lakini CUF kuwa na mitaa mingi SEGEREA mwaka 2014 au CHADEMA kupata kura nyingi za ubunge mwaka 2010 siyo hoja ya vyama hivi viwili kuweka u-vyama wao mbele na kusahau ushirikiano.
UKAWA ikiweka mgombea mmoja Segerea itashinda kwa kishindo. Ikivurugana na kila chama kikajiwekea mgombea sote tutaanguka.
Ni hayo tu.
J. Mtatiro.

Seriously speaking. Hivi anayetatua shida za wananchi ni mbunge(hakusanyi kodi anasimamia tu serikali) au serikali inayokusanya kodi? Sasa we ulitaka afanye nini kama yeye si mkusanya kodi? Nilitegemea uelekeze malalamiko yako zaidi kwenye serikali ya chama tawala(CCM) badala ya "individual". Halafu na wewe unataka uitwe GT!!!! Embarassing!!!
machipi member, udsm member i support you 100%,