Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

Julius nakuaminia sana ila nashauri watu wa Dar wamwkuwa wana angusha sana harakati za ukombozi wa kweli. nakuahauei nenda tafuta jimbo mkoani utatoboa. Dar wame lala bado. All the kind of best
 
Niwazo nzuri katika kuleta mabadiliko, ila ningependa kukushauri kama mwanaukawa mwezako,ikiwa lengo nikuchukua majbo mengi hapa Dar,nivyema hilo jimbo ukawaachia CDM nawewe ukaja huku ukonga kwani huku hatuna mbunge bali tunakivuli tu. Nakuhakikishia kwautafiti nilioufanya,jimbo laukonga nirahisi zaidi kuchukua. Mwaka 2010 jimbo hili laukonga lilienda CCM kutokana nakutokuwepo kwampizani mwenye ushawishi na mvuto mbele yajamii.
Tafakari kwaumakini kuhusu hili jimbo la ukonga,segerea CDM wananguvu mno hivyo usijeshangaa ukaacha kupitishwa, njoo huku ukonga japo kunatetesi za Jery Slaa kutaka kugombea ubunge huku, nakuhakikishia mimi nimwana ukonga niliyezaliwa nakukulia huku hivyo najua nijinsi gani wanaukonga tumechoshwa nautawala wakifedhuli wa CCM ila hatujui tumpe nani kura zetu, ukija huku kaka yangu Mtatiro jimbo nilako.
 
Mimi ni mkazi wa Segerea,na jinsi ninavyolijua hili jimbo ni stronghold kubwa ya Chadema.Na huku Chadema only ndo wako political active kuliko vyama vingine.Kwa mfano wanapita kwenye mitaa kurejista wanachama wapya na mashabiki wake.Na nadhani pia wanawenyeviti wengi pia.Lakini elimu kuhusu UKAWA ni ndogo sana.Mfano mdogo,Juzi walipita Chadema kurejista watu katika mtaa wa machimbo,chakushangaza nilisikia watu wanasema kama ni Chadema waandikishwe,kama vyama vingine no!hawataki kabisa.So,mtatiro umejipanga vipi kukabiliana na hii changamoto?
 
Nimependa objectivity kwenye tangazo lako.
CCM wasijisumbue kuweka mgombea
 
Ni vizuri, Mpendazoe nasikia anarudi kishapu kugombea ubunge, mm ni chadema damu damu, ila nakuunga mkono ugombee segerea kwa tiketi ya UKAWA.

Tatizo Mpendazoe hata hasikiki au hahusiki na kujenga chama,amwachie kijana julius mtatiro bwana,go go UKAWA go go go go Mtatito.
 
Last edited by a moderator:
NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.


Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0

Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com

Gombea jimbo la ukonga liko wazi kwa miaka mingi sana
 
Jimbo hili haliwezi kuchukuliwa na wahuni kirahisi hivi.
 
nakuomea Ukawa ipitishe jina lako tutahakikisha unachukua ushindi,sasa maadam umekuwa wazi be careful yule jamaa wa Segerea ni hatari anaweza fanya lolote

Unajua we dadangu sikuelewi kabisa.. Ukiamka UKAWA ila ukilala CCM... Upo upande gani mkuu maana kuna siku niliona ukiwatetea CCM
 
Jimbo hili haliwezi kuchukuliwa na wahuni kirahisi hivi.

Unajisikia raha kutamka neno wahuni eeh? Hujui kama mhuni namba moja ni Kinana? Yeye ndio msaga mirungi namba moja nchini. Kazi yake nyingine ni kupapasa matiti ya viongozi wenzake hadharani
 
nitagombea ubunge jimbo la segerea – dar es salaam.


Ndugu zangu, kesho jumatatu 09 machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa dar es salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya ukawa watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya ukawa.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya ukawa wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya oktoba 2015, segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/juliussundaymtatiro/posts/578218822317742:0

julius mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, juliusmtatiro@yahoo.com
nakuunga mkono mkuu.mungu akutangulie
 
Back
Top Bottom