Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

Nitagombea ubunge Jimbo la Segerea – Dar es Salaam

NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.

Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani ya UKAWA.

Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.

Pamoja na kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.

Mimi ni muumini wa demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.

Nawaomba wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na labda mtu huyo atakuwa ni mimi.

Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki https://www.facebook.com/JuliusSundayMtatiro/posts/578218822317742:0

Julius Mtatiro,
+255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com

Karibu sana segerea kaka mkubwa Julius Mtatiro. Kiukweli Makongoro tumemchoka huyu jambazi sugu hana nafasi miyoyoni mwa wana segerea.
 
Ndugu yangu JAKACKSERU,

Hata hiyo UKONGA ina wagombea wazuri tu wa CHADEMA akiwemo Kamanda Mwita Waitara, ngoja tusubiri kujua UKAWA inagawanaje majimbo ndipo tutahitimisha masuala haya. Lakini kwa namna nilivyojipanga sitakuwa na kinyongo kumuunga mkono mgombea yeyote wa UKAWA ikiwa atapitishwa kugombea Segerea.

Sina tabia ya kupigania madaraka kwa sababu najua kuna masuala mengi ya kufanya kuliko kuongoza. Jambo la msingi ni kuwa UKAWA itapata mgombea imara SEGEREA. Wana Segerea wameichoka CCM na wanahitaji kiongozi imara zaidi, ukiongea nao wanakueleza hawachagui chama, watahitaji kuwa na kiongozi imara kutoka chama chochote kati ya vyama vyetu na kwamba huyo ndiyo chaguo lao. Mimi ni mmoja wa watu wanaohitaji ridhaa hiyo na wapo wenzangu, sote tutapimwa, atakayepitishwa tutampigania.

Na jambo la mwisho unalopaswa kujua ni kuwa vyama vya CHADEMA na CUF vinahitajiana mno UKONGA na ukiangalia hata matokeo ya serikali za mitaa utagundua kuwa kati ya mitaa takribani 33 ya UKAWA, CUF ndiyo ina mitaa mingi. Hii ndo hali ya kisissa ya sasa. Lakini CUF kuwa na mitaa mingi SEGEREA mwaka 2014 au CHADEMA kupata kura nyingi za ubunge mwaka 2010 siyo hoja ya vyama hivi viwili kuweka u-vyama wao mbele na kusahau ushirikiano.

UKAWA ikiweka mgombea mmoja Segerea itashinda kwa kishindo. Ikivurugana na kila chama kikajiwekea mgombea sote tutaanguka.

Ni hayo tu.

J. Mtatiro.
 
kamanda julius unajulikana toka udsm uliendesha figisu figisu nyingi hauna mashaka yeyote we ni kamanda
 
Huyu jamaa ni mtumba, kama alishindwa 2010, nini anadhani kumembadilisha na kuwa bora 2015?
 
Daaah, Mkuu Julius Mtatiro kila lakheri kaka Ni hakika na ni kweli tupu endapo taratubu za chama chako, UKAWA zikakupitisha kama mgombea hapa Segerea then tayari wewe ni Mwakilishi wa wananchi kwa jimbo hilo...!!!

Si kwasaba ya umaarufu wako,Elimu ama ukubwa wa chama chako bali kwakuwa wananchi wameichoka ccm.. naam hawaitaki tena, Matokeo ya uchaguzi mwaka 2010 yanasema yote.!!!

Mimi binafsi nadhani ukigombea jimbo lolote la uchaguzi kwa hapo Dareslaam uhakika mkubwa wa kupata ubunge unao hasa kutokana na ushirikiano wa vyama vyetu (UKAWA) Ila kwa jimbo hilo la Segerea nadhani kutokana na umaarufu wako na kazi ama nafasi ya uongozi uliyoitumikia ndani ya cuf kipindi cha nyuma, Vinakuhitaji kupata jimbo ambalo kwa hapo Dar ccm inaonekana inanguvu..!!!

Jimbo la Segerea halihitaji nguvu kubwa kulichukua, ni kampeni lidogo ushawishi kidogo tu unatosha kutupatia jimbo hilo... Sasa kutokana na umaarufu wako nilidhani ungehitaji jimbo tafu kidogo kwa upinzani (UKAWA)

Lengo ni nini??

Kuwaondoa ccm ktk jiji la Dareslaam, ambalo mimi nadhami ndilo kitovu cha mabadiriko. Hivyo majimbo yale mepesi tuyaache kwa watu ambao labda twaweza sema si maarufu sana Bali wanakariba ya uchapakazi. Narudia tena lengo lisiwe kupata tu ubunge, bali kuitokomeza ccm Dareslaam. Kingine ni taratibu za UKAWA ambazo nimekuwa nikizisikia....

Kwamba kama kwenye jimbo mojawapo linalogombewa linambunge mwakilishi wa UKAWA then jimbo hilo linabaki mikononi mwa chama chenye Mbunge. Halafu kama jombo husika linambunge wa ccm then kinaangaliwa chama cha (UKAWA) kilichosimamisha mwakilishi na akapata nafasi ya pili...!!!!

Sasa kwataratibu hizi naona tayari mwakilishi wa hilo jimbo anapaswa kutoka Cdm (Kwa uwiano wa kura alizopata Mpendazoe mwaka 2010)

Note,
Silisemi hili kama mwanachadema ama kama nakipigania chama changu, hapana bali kulingana na taratibu ambazo tumekuwa tukisimia kuwa UKAWA wamekubaliana.

Sasa kwa changamoto hii unasemaje kaka??

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Kwanini na wewe ni mnyiramba wa Ndago singida lakini bado upo segerea? Kwanini na wewe usiende kuishi kwenu singida mkuu?

Makamanda hivi CHADEMA kimesharuhusu fomu za ubunge zichukuliwe?
 
Hilo jimbo kama la watu toka mkoa fulani hivi!
Sio kama, ndio ukweli wenyewe!, kama ilivyo kwa Ubungo nako wanatoka mkoa fulani.

My Take.
Mtatiro anachagulika zaidi kuliko Mpendazoe!.
Mtatiro ni born and breed in opposition, Mpendazoe ni CCM aliyepotezwa maboya na CCJ, akajiunga Chadema because he had no option!, na amino nawaambie saa hizi anajuta!, anatamani kurudi zake CCM, ndio maana hasikiki kabisa katika harakati!, hivyo kama ni kweli bado ana nia na opposition, ashauriwe aende Kishapu. Jimbo la Segerea ni la Mtatiro!.

Kwa majimbo ya Dar es Salaam, karibu yote yatakwenda UKAWA isipokuwa Ilala! na Kigamboni!.

Pasco.
 
Ndugu yangu JAKACKSERU,

Hata hiyo UKONGA ina wagombea wazuri tu wa CHADEMA akiwemo Kamanda Mwita Waitara, ngoja tusubiri kujua UKAWA inagawanaje majimbo ndipo tutahitimisha masuala haya. Lakini kwa namna nilivyojipanga sitakuwa na kinyongo kumuunga mkono mgombea yeyote wa UKAWA ikiwa atapitishwa kugombea Segerea.

Sina tabia ya kupigania madaraka kwa sababu najua kuna masuala mengi ya kufanya kuliko kuongoza. Jambo la msingi ni kuwa UKAWA itapata mgombea imara SEGEREA. Wana Segerea wameichoka CCM na wanahitaji kiongozi imara zaidi, ukiongea nao wanakueleza hawachagui chama, watahitaji kuwa na kiongozi imara kutoka chama chochote kati ya vyama vyetu na kwamba huyo ndiyo chaguo lao. Mimi ni mmoja wa watu wanaohitaji ridhaa hiyo na wapo wenzangu, sote tutapimwa, atakayepitishwa tutampigania.

Na jambo la mwisho unalopaswa kujua ni kuwa vyama vya CHADEMA na CUF vinahitajiana mno UKONGA na ukiangalia hata matokeo ya serikali za mitaa utagundua kuwa kati ya mitaa takribani 33 ya UKAWA, CUF ndiyo ina mitaa mingi. Hii ndo hali ya kisissa ya sasa. Lakini CUF kuwa na mitaa mingi SEGEREA mwaka 2014 au CHADEMA kupata kura nyingi za ubunge mwaka 2010 siyo hoja ya vyama hivi viwili kuweka u-vyama wao mbele na kusahau ushirikiano.

UKAWA ikiweka mgombea mmoja Segerea itashinda kwa kishindo. Ikivurugana na kila chama kikajiwekea mgombea sote tutaanguka.

Ni hayo tu.

J. Mtatiro.
Mkuu Mtatiro. kiukweli umeni impress sana!. Segerea ni yako na hili sasa ndio somo la kwanza kwa Chadema, mafanikio ya ushirikiano wowote ni give and take!.

Pasco
 
Ndugu yangu ungerudi kwenu ukale kimoro tu tungu lini kiongozi anakuwa mapepe kiasi hicho kwani hujiulizi kwanini tulikufyatua kwenye unaibu katibu mkuu?
 
hapo ndipo uwezo wako wa kufikiri ulipokufikisha, hii inchi ina shida kweli.

Shida hapa unayo wewe hutaki kukubali fact ni lazima tuseme sasa ili limalizike, nje mnakataa halipo lakini kiukweli ni tatizo kubwa.
 
Back
Top Bottom