Nitafungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi

Kwa bahati mbaya nchi hii Polisi na Mahakama ni 'mapacha' wasiofanana.Taasisi zote mbili uadilifu wake unatia shaka.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Nakumbuka wakati tuko sekondari tuliambiwa... mwalimu akikupiga ngumi, huo ni ugomvi sio adhabu ya kishule i.e unaruhusiwa kujilinda na wewe ukarusha ngumi.

Inapotokea Polisi wanakamata mtu bila kufuata taratibu za kikatiba, sheria na miongozo yao kama polisi, huo ni UTEKAJI.

Tito Magoti amekamatwa na "polisi" wakiwa na nguo za kiraia, hawakujitambulisha, walikuja na gari isiyotambulika, hawakumwambia kosa lake, wamempeleka polisi bila kumpa nafasi ya kuwasiliana na jamaa zake na huko polisi hakumwandika jina lake etc. Hebu piga picha kwa mfano angekuwa ana maradhi fulani, katika purukushani akafariki, unadhani polisi wangekuja kusema ilikuwa ni sisi?

Kwa ufupi kama taratibu hazijafuatwa, huo ni utekaji. Ndio maana Zakaria wa Tarime alipowatwanga risasi wale wasiojulikana, walishindwa kumpa kesi ya kuwapiga jamaa risasi; kwa sababu sheria iliyorasimisha idara ya usalama haiwaruhusu kukamata, alikuwa na haki kabisa ya kujitetea. Ila wale wangekuwa askari wa kawaida pengine angekuwa na kesi kubwa zaidi.
 
R.I.P HAMZA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…