Nitafungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi

Dhuruma kamwe haijawahi kuishinda haki.

Ipo siku haki itashinda tu
 
"ukitekwa" huwezi kutambulika ulipo na usalama wako unakuwa mashakani.

"ukikamatwa" lazima utafahamika ulipo na usalama wako huzingatiwa.

Jeshi la Polisi huwa haliteki watu bali linakamata mtuhumiwa wa uhalifu au wahalifu na pia unaweza kukamatwa papo hapo bila kufuata taratibu endapo kuna hali ya udharura au kwa kufuata taratibu kulingana na mazingira.

Jeshi letu la Polisi linafanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu na kwa kuzingatia sheria na taratibu.
kuna mabadiliko makubwa sana ktk utendaji kazi wa Jeshi letu.
Pongezi za dhati kwa IGP Sirro.
 
Keyboard warrior's
Kwani wewe upo wapi? Acha kuishi kwa Akili za Le mutuz tumia Akili zako kujua kuwa haki husakwa kwa njia zote bila kujali changamoto na wapi ulipo
 
Jeshi letu wewe na nani? Weledi upi? Kufukuza watu mahakamani ni weledi? Pongezi kwa IGP kwa lipi? Kuwabambikia kesi wapinzani ni kufanya kazi kwa weledi? Kingai mahita kuwatesa watu kuwafunga pingu mikono miguu saa 24 ni kufanya kazi kwa weledi?
 
Polisiccm hushitakiwa sana ingawa wengi hawajui kuwa hakuna aliye juu ya Sheria na hapo ndipo Polisiccm hutumia huo udhaifu wa kutojua haki na Sheria kuwatesa watu kuwapiga kuwalipa wakubali ugaidi ambao haupo , kuhoji watu kwa kuwapiga kutojua maana ya PGO nk
 
Hata usiposhinda Itasaidia kufanya watu waanze kuamka na kujua polisi wanafanya utekaji na kupoteza watu, go for it!
 
Kabla ya kuhangaika sana ebu tutolee ufafanuzi kati ya kutekwa na kukamata kwa mujibu wa uelewa wako wewe!

Siku hizi CHADEMA mmekuja na mbinu ya kutangazia umma mnatekwa wakati ukweli ni kwamba mnatenda jinai, halafu mkikamatwa mnakinbilia kutangaza mitandaoni uzushi wa kutekwa.

Mbona hamuendi vituo vya polisi kutoa taarifa ya kutekwa kwenu?

Lini mtaacha hizi siasa UCHWARA?
 
Wafungulie kesi ya moja kwa moja watu wawili mahita na kingai kwa kutesa kuwapiga kuwafunga pingu mikono miguu saa 24 kila siku walinzi wa mbowe, hii itakuwa kesi ya wachache lakini itasaidia kuwafungua macho wapenda haki wote Duniani
 
Hata usiposhinda Itasaidia kufanya watu waanze kuamka na kujua polisi wanafanya utekaji na kupoteza watu, go for it!
Sheria inasema Polisiccm anapokwenda kumkamata mtu lazima awe na RB na pia amweleze mtuhumiwa sababu ya kumkamata na ndugu wa mtuhumiwa wanapewa taarifa alipo ndugu yao, na pindi akifikishwa kituoni ndani ya saa 48 anatakiwa awe amefikishwa mahakamani, pia ipo Sheria inayomruhusu mtuhumiwa kudai fidia endapo amekamatwa kimakosa kwa uonevu ama kwa Bahati mbaya, Sheria hizo zipo lakini kwa kuwa wananchi hawajui haki zao wamekosa wajibu wa kuzitumia na Polisiccm kuendelea kuwakamata kuwaweka vituoni hata week mwezi pasipo kufikishwa mahakamani
 
Kwa kuwa kajitoa mhanga ni mara 100 aombe mawakili wa kimataifa ili waweze kuweka hiyo kesi kidunia iwe kama alama ya kuonyesha mapungufu ya Polisiccm kwenda idara ya ukamataji na mahojiano
Hao mawakili wa kimataifa si ndio kina Amsterdam?

Mbona hatujaona matunda ya kazi yao zaidi ya kupiga hela za Tundu?

Muwe mnajitahidi kusoma mambo ya Dunia ili mfunguke uelewa.

Duniani kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanaisumbua Dunia na siku za usoni kuliko hizi sarakasi zenu za kibongo bongo.

Vitu kama Climate change,Covid19,Taliban na hatari ya kuigeuza Afghanistan kuwa chaka la ugaidi au kashfa za kifisadi kama zilizoibuliwa juzi na na Pandora Documents!

Nyinyi CHADEMA endeleeni kuchezea keyboard tu.

Hakuna kipindi kigumu mtapitia kama hiki,poleni sana.

Lowassa aliwaambia, Sumaye pia aliwaambia,na hata Nyalandu pia wote hawa waliwausia kwamba kuna siasa za kistaarabu na kiharakati bila nidhamu.
Nyinyi mkaishia kuwatusi woote mkiongozwa na Lema na Halima mdee.
Leo hii Lema haongei na Mdee na Lema anatukana kutokea Canada [emoji1063]

Lissu anatukana kutokea Ubelgiji
Leo ndio mnaelewa maneno ya wale wazee yalikuwa mazito.

Laana ya Doctor Wilbroad Slaa itawaumiza sana!
 
Siasa uchwara unazo wewe Yaani umejitoa fahamu zote hata hujui umeandika nini? Chadema wamefanya jinai gani? Kuwabambikia kesi ndiyo jinai zako? Tueleze alipo moses lijenje? Tueleze alipo mwenyekiti wa baraza la wazee chadema?
 

Kwenye kesi itabidi uthibitishe nani katekwa?Alitekwaje tekwaje?Nani aliyetekwa!Mwisho Mahakama inaweza kukubaliana na wewe kwamba utekaji haurusiwi kisheria na hautamkwi na sheria yoyote na ni kosa.Ikaishia hapo na kukuacha kwenye “vacuum” kubwa.Na matukio unayoita ya Utekaji (badala ya Ukamataji) yakaendelea.

Hoja hapa ni lazima uwe “specific” na “matukio” na ni taratibu hizi hasa unazolalamikia kukiukwa ili mahakama “ione”kama kulikuwa na “Utekaji” badala ya “Ukamataji”.
 
Kwa majina bandia hapa unafoka , watu dhaifu hujitutumua kwenye keyboards za simu ,watu wakikamatwanasema wametekwa

USSR
 
Dr slaa hana laana aliacha chadema kwani alinunuliwa na CCM kwa dola milion 2 na kupewa nyumba Canada hana mfano wa kuigwa ni mzee wa hovyo tu, Lowasa na Sumaye walitishwa na marehemu magufuli wakiogopa wakarudi CCM, wewe ndiyo uendelee kuchezea keyboard huna unachokijua zaidi ya kujiona unajua vingi kumbe hujui kitu, wewe kama CCM na Polisiccm wanakusikiliza basi wakataze wasiwe wanawabambikia kesi wapinzani na CCM wafanye siasa safi tume huru ya uchaguzi uone nguvu ya wapiga kura bila uchakachuaji wenu
 
Walinzi wa mbowe walikaa vituoni zaidi ya masaa 48 pasipo kufishwa mahakamani kisheria hata akianza na hapo tu atakuwa kapata pa kuanzia
 
Kwa majina bandia hapa unafoka , watu dhaifu hujitutumua kwenye keyboards za simu ,watu wakikamatwanasema wametekwa

USSR
Kwani wewe hilo ni jina lako? wewe upo mbele ya keyboard? si na wewe upo nyuma ya keyboard kama unaona wanajitutumua hata wewe unajitutumua kusaka uteuzi kwa kujiandikia andikia chochote ili uonekane unawatetea CCM mitandaoni upate cheo kwa njia haramu za kishetani
 
Naona una muda wa kupoteza
 
Hilo swali lako mkuu mi naona ni maisha yamekupiga tu huku mtaani polisi wana kamata ila waasi, magaidi au majambazi hao ndio watekaji ili wapate pesa au kitu fulani au kulipiza kisasi lakini pia hata vitani wanaoshindwa wanakuwa mateka lakini kwa upande mwingine mkamataji kwanza anajitambulisha na anakwambia sababu ya kukukamata pia kama kosa lako linadhamana unadhaminiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…