Nitaficha wapi uso wangu? Rais Kikwete ameniumbua

Nitaficha wapi uso wangu? Rais Kikwete ameniumbua

Wakati fulani tuseme na ukweli, wajerumani walitukuta hatuna hata nguo, tunauzwa sokoni kama mbuzi, je hilo jengo la ikulu kajenga nani kama sio wajerumani, reli ya kati kajenga nani kama sio wajerumani.ukweli mazuri ya wajerumani kwa miaka 35 waliyokaa hayawezi kulinganishwa na ya kwetu.

Acha uongo, jengo la ikulu ya Dar halikujengwa na Wajerumani, ni Waingereza. Hata ikulu ya Zanzibar walijenga Waingereza. Wakati walikuwa na system ikiitwa BOMA (British Overseas Management and Administration). Ilikuwa baada ya Wajerumani kuondoka
 
  • Thanks
Reactions: Awo
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Profesa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru serikali ya Ujerumani kwa kututawala na kutuletea maendeleo wakati wa ukoloni.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jana, Rais Kikwete alimuambia Rais wa Ujerumani kwamba wakati wanatutawala walitufanyia mambo mengi sana mazuri ikiwemo kutujengea jengo la ikulu ambalo tunalitumia hadi sasa.

Rais ameniumbua. Sijui nitaficha wapi uso wangu.

Tangu mwaka 2008 nimekuwa nikiwafundisha wanafunzi wangu Historia nikiwaaminisha kwamba wakoloni hawakuwa na nia njema. Nimekua nikiwaambia wanafunzi wangu kuwa wakoloni walikuwa wakitunyonya, kutukandamiza na kutudhalilisha sana.

Niliwaambia hata elimu waliyoitoa na miundombinu waliyojenga ilikuwa ya kuendeleza unyonyaji.

Niliwaambia wanafunzi wangu kuwa watu waliowapinga ukoloni na kuwapiga vita kama kina Mkwawa, Mangi Meli, Mtemi Isike na Chifu Kimweri ndio mashujaa wetu. Niliwasema vibaya sana wakoloni huku nikitumia vitabu vya kina Walter Rodney kama “HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA” katika kujenga hoja. Pia nilitumia sehemu ya nukuu za “The Dar es salaam School of thought” kuaminisha wanafunzi wangu kwamba wakoloni walikuwa watu makatili na wasiotufaa.

Leo rais kaniumbua. Kawaambia Watanzania kuwa Wakoloni walikuwa watu wema sana na waliotuletea maendeleo. Rais akafika mbali zaidi na kukiri bila Ujerumani kututawala tusingekuwa na Ikulu ya Dar es Salaam.

Sasa najiuliza kama wanafunzi wangu wamemsikiliza Rais Kikwete nitakoma maana nitaumbuka. Na kama wamemsikiliza Lazima watamuamini kwa sababu Rais wetu ni Profesa.!!

Kwa heshima ya Malisa Godlisten naomba kushirikisha hii simanzi!

Mwalimu hayo yasikushangaze hizo zilikuwa ni mbinu za kumuliza mtu mzinga kwani serekali ya sasa inaendeshwa kwa mizinga.
 
sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus
kumbe wajerumani ndio Jesus.sikujua
 
Kwa jinsi huyu FF anavyo mshobokea JK kwa kila kitu hata kile ambacho kiko wazi kuwa kakosea napata mashaka kuwa kuna siku ataambiwa mkulu kaamua kupiga kiti moto na faizaFox atatafuta aya za kuhalalisha ili kumtetea kuwa mradi iive tuu haina shida kuliwa.
 
Last edited by a moderator:
Bila kusahau hata Hospitali ya Bugando ilijengwa na Wajerumani...

Wacha aisifu Germany tu...
 
sisi tunawashukuru Wajerumani kutuletea Lutheran church,machame yote ni walutheri,ingekuwa siyo wakoloni inawezekana kilimanjaro yote ile ingekuwa kama Tanga vibaghashia kila kona,Thank you Jesus

Yaani wewe ni mpumbavu wa mwisho kabisa, sa ndo umeandika nini hapa? we kafir ni tubwasha hatari sana hata akili huna
 
Namshukuru Hitler kwa kuninunulia chai hapa Lumumba asubuhi hii
 
Ndo maana watanzania tunaambiwa tuna IQ ndogo sababu ya kuwakilishwa na watu wa aina ya Kikwete.
 
Kwani thamani ya mali walizochuma zinaendana na maendeleo waliyoyaacha.?

Kwa muono wa jk bado haamini kama Tanzania inaweza kuendelea bila wahisan.

Tulikosea sana kumchagua jk.

Bravo! Na alishindwa kumwambia huyo Mzungu kuwa sehemu ya maendeleo yao inatokana na rasilimali wailizpora huku kwetu. Na wanao wajibu - na sio ombi,- wa kuturejeshea ili waondokane na lawama ya milele
 
Tena licha ya Ikulu, Mjerumani kafanya kweli, reli ya kati mpaka leo.

Barabara karibu zote unazotumia leo ni zile zile za Mjerumani, sanasana tumezipanuwa na kuweka lami.

Nenda Tanga, moja katika miji ambayo imepangika vizuri na hiyo ni toka Mjerumani, si leo.

Ukweli ubaki kuwa ukweli. Natamani tungebaki kutawaliwa na Wajerumani hadi leo hii. Hatuwezi lolote.

Duh! umeongea pointi dada hadi raha. Hawa jamaa ni wema sana na wana upendo sana. Kuna wale jamaa walikuja wakatuachia urithi wa dini tu, wakasepa. Leo hii huu urithi wa dini waliotuachia umekuwa ni mwiba kwetu - wametutengenezea watanzania walalamishi balaa! kiu ya ulalamishi imeingizwa kwenye akili zao na hakuna anayeweza kui-quench. Hata uwape chuo kikuu cha bure watazua lingine tu. (...sasa hebu fikiri kidogo chuo hicho wapewe watanzania wa dini nyingine - hilo balaa lake!) Wajerumani wangeendelea kubaki wangeokoa pia akili za wengi sana! si ajabu FF leo angekuwa mtawa pale saint Joseph akiwafundisha watoto wetu thawabu wanazopata kwa kumpenda adui kama kristo alivyotufundisha.
 
  • Thanks
Reactions: Awo
Yaani wewe ni mpumbavu wa mwisho kabisa, sa ndo umeandika nini hapa? we kafir ni tubwasha hatari sana hata akili huna

Du! huu ndo urithi wa waarabu tulioachiwa. Kwa kweli wajerumani wangeendelea kuwepo, pengine huyu jamaa leo hii angekuwa katekista akiwafundisha watoto wetu kuwa matusi ni dhambi.
 
Kama tumeshindwa kujenga IKULU yetu huko Chamwino Dodoma, hata baada ya miaka ya 54 ya uhuru, kwanini asiwapongeza Wajerumani walioweza kujenga hiyo Ikulu ya Magogoni zaidi ya miaka 100 iliyopita!

Pia angeendelea kuwasifu Wajerumani, kwani tangu walipotuletea meli ya MV Liemba, Sisi hata baada ya miaka 54 ya Uhuru tumeshindwa kuweka meli ya kiwango hicho ziwa Tanganyika.
Ndio tumeshindwa kutokana na udhaifu wa selikari yetu,wizi,ufisadi na tamaa za viongozi wetu.
 
Wakoloni waliwakuta mababu zote juu ya miti......wanaishi maisha ya kinyani pamoja na manyani,

Walitustaarabisha na kutupa elimu angalau tuonekane na sisi watu duniani. Na ndio maana mpaka leo baadhi ya

wazungu wakimuona Muafrika wanamwita nyani, huo ndio ukweli !! Tusibishe wala kukasirika, sisi ni manyani!!

sisi ni manyani!! Sisi ni Manyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani !!
 
Hivi na wewe ulimchagua kweli au shongondo tu!

Kwani thamani ya mali walizochuma zinaendana na maendeleo waliyoyaacha.?

Kwa muono wa jk bado haamini kama Tanzania inaweza kuendelea bila wahisan.

Tulikosea sana kumchagua jk.
 
Wakoloni waliwakuta mababu zote juu ya miti......wanaishi maisha ya kinyani pamoja na manyani,

Walitustaarabisha na kutupa elimu angalau tuonekane na sisi watu duniani. Na ndio maana mpaka leo baadhi ya

wazungu wakimuona Muafrika wanamwita nyani, huo ndio ukweli !! Tusibishe wala kukasirika, sisi ni manyani!!

sisi ni manyani!! Sisi ni Manyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani !!

Ndugu yetu Nyani hoja yako tumeipata na tutakutengenezea memorandum yako ili utambulike nyani kisheria na urudi kwenu mwituni!
 
Ndio maana mkono sweta huko bado tatizo, babu yako alikuwa anakupiga kamba tu Rorya si imekuja juzi na vita ilikuwa mijini enzi hizo.

...tabia ya wakwere si watu wapwani,hakuna kitu.....sisi huku Rorya tuliwatimua hao jermani vibaya...babu alikuwa anatusimlia.
 
Tumekuwa kama watoto yatima tunaolelewa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima, na kwa mujibu wa ndugu J.K inabidi tuwashukuru walioleta maangamizi kwenye familia zetu kwa maana kama sio maangamizi yao tungeendelea kuishi na familia zetu maisha duni ila sasa tunakula walao mkate na kupewa zawadi ya kandambili kwenye vituo vya malezi!
 
Kwa nini CCM wanashindwa kuendesha nchi Kama walivyoiendesha Wajerumani?

Nyerere aliiuwa hii nchi, Kikwete ameanza kuijngea Tanzania na ameweka misingi mizuri sana baada ya kubomoa lile jisingi bovu lililowekwa na Nyerere. Sasa Tanzania inapaa tu, hakuna kizuwizi. Think Big.
 
Acha uongo, jengo la ikulu ya Dar halikujengwa na Wajerumani, ni Waingereza. Hata ikulu ya Zanzibar walijenga Waingereza. Wakati walikuwa na system ikiitwa BOMA (British Overseas Management and Administration). Ilikuwa baada ya Wajerumani kuondoka

Mkuu
Naona wewe umesoma sayansi na si Historia.
 
Back
Top Bottom