Nitafanya KESHO

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Najua wengi walidhania nitafanya kwa maana ya "ku do" - lol - , lakini ninachotaka kuongelea ni tabia ya AJIZI, USIRI, UCHOVU, DHARAU...ya kuacha jambo la kufanya leo ukasema "nitafanya kesho". Iwe ni kujibu PM, simu, sms, barua...kuacha chombo ulichokulia usiku uje kukosha asubuhi, kurundika nguo chafu mpaka ukakosa nafasi, umepaka rangi nyumba ikabaki sehemu ndogo sasa ni mwaka wa nne hujarejea kupaka hapo; miezi minne ulibadilisha makazi mpaka leo mizigo mengine imo ndani ya maboksi, taa ya stoo iliungua, lakini badala ya kubadilisha unaingia stoo na tochi....Mambo ni mengi yanayotufanya tuwe na ajizi na kuna misemo mingi ya ajizi:

- Ajizi nyumba ya njaa.
- Ajizi mwizi wa wakati
- Kesho haifiki
- Kesho kesho mavituzi yakuwa
- Tusiliache kesho tunaloweza kulifanya leo
Iko hata nyimbo moja ya zamani, "Bomoa tutajenga kesho".

Nianze na mimi. Ajizi zangu kubwa ni kujibu na/au kuandika sms na barua; na kwenda kumwona mtu. Ninakaa mpaka siku zinapita sana kiasi cha kushindwa baadae nianzie wapi.

Wewe je, ajizi yako iko wapi? Ni kitu gani ulipaswa kukifanya ukakiacha kwa ajili ya kesho na mpaka leo bado hujakifanya au ulikifanya siku, wiki, miezi miaka kadhaa baadae?
 
Nikisema nitajibu kesho ndo yaleyale
:biggrin:Leo akili imekaa ki weekend weekend
 
dah.....uvivu wa kusoma,kila siku nasema nitasoma,nitasoma kesho mpaka unakuta mtihani umeshafika
 
Nikisema nitajibu kesho ndo yaleyale
:biggrin:Leo akili imekaa ki weekend weekend
Hahaha! Hamna neno, ikifika kesho J1 itakua ndio harakati zaidi,
hivyo utachangia kesho J2.Lo! Umeamka na kazi za ndani kibao,
Hapana tabu, si kesho J3 ipo. Duh! J3 harakati za kusaka mkate zimeanza,
lakini haidhuru, kesho ipo, utachangia kesho.

Wikiendi njema FL1, lakini ianze leo sio kesho.
 
dah.....uvivu wa kusoma,kila siku nasema nitasoma,nitasoma kesho mpaka unakuta mtihani umeshafika
Na hili nalo sikulitaja kule lakini noma sana. Unasubiri mpaka mwezi wa mtihani unajipangia kusoma kesho, wiki tatu zinakatika. Inabaki wiki moja bado unajipangia kusoma kesho. Kesho mtihani, "Kesho nitaamka mapema sana nisome".
Unachelewa kuamka, "nitasoma nikifika shule/chuoni". Hujui uanze wapi...!
 
Mamamia !
Umeshuka na changamoto , ok
Mimi nna ajizi ya kuhesabu pesa, kuna mihela hua naitumbukiza kwenye box (hadi box limejaa)
Lakini kila nikitaka kuhesabu nasikia uvivu ! Najiambia ntazihesabu kesho.
 
Mamamia !
Umeshuka na changamoto , ok
Mimi nna ajizi ya kuhesabu pesa, kuna mihela hua naitumbukiza kwenye box (hadi box limejaa)
Lakini kila nikitaka kuhesabu nasikia uvivu ! Najiambia ntazihesabu kesho.
Mkuu, kwanza naomba ucheki vizuri jina la avatar.
:focus:Hiyo mihela wala haina haja ya kuihesabu, itajihesabu wenyewe wakati unadokoa kuitumia. Siku ukiona box limebakia "nearly empty" utahesabu tu.
 
Time and tide wait for no man !!!!!!!!!!!
Look to this day for every tomorrow has a tomorrow !!!!!!!!!!!
 
Mi nlivyoona sentensi ya kwanza umeandika siyo "ku do" nimeacha kusoma sredi nzima so napita tu hapa.
MAPROSOO.
 
Mi nlivyoona sentensi ya kwanza umeandika siyo "ku do" nimeacha kusoma sredi nzima so napita tu hapa.
MAPROSOO.

MAPROSOO !
Mbona mi naona kupita ndiyo kanuni !
Kwani kuna kwingine hua unakaribishwa kulala ?
Labda kule kwenye jukwaa la wenye nywele zenye rangi kama Mbunge wa Monduli .
 
Liwezekanalo leo lisingoje kesho maana hatuna hata hakika kama hiyo kesho tutafika. Asante kwa uzi wako mzuri umenikumbusha viporo vya mambo mengi niliyopanga kuyafanya kesho ila naona ngoja nianze sasa.
 
MAPROSOO !
Mbona mi naona kupita ndiyo kanuni !
Kwani kuna kwingine hua unakaribishwa kulala ?
Labda kule kwenye jukwaa la wenye nywele zenye rangi kama Mbunge wa Monduli .

Kumbe wote huwa tunapita?! sasa mbona kuna wengine kila nikifungua nawakuta!! inakuaje?
MAPROSOO.
 
MAMMAMIA
Nakusalimu mkuu ..

Kwa kifupi ni kwamba sina kitu ambacho nakiacha kwa kesho ..lakini mpaka Jioni ifike na nikiwa nimechoka basi kutakuwa na kiporo.
lakini kwa ujumla napenda kufanya leo au sasa
 
We acha tu, mi nafanana na wewe Mammamia, hayo ya kwenda kumuangalia mtu zishapita wkend kibao.
Jamaa wanafiwa, wanumwa, wanojifungua kila siku napanga kwenda wkend bt ikifika siendi napanga tn wkend inofuata hatimae imepita miezi.
Hayo ya kujibu sms na barua ndo hata sisemi, mpk aibu
 
Back
Top Bottom