Heshima kwenu GTs,
nahitaji mchango wa mawazo yenu hasa kwa wazoefu wa biashara na ujasiliamali.
ninayo tsh 20,000,000. sitaki kuajiliwa kwa sababu nimeshaajiliwa for 5 years toka nlipomaliza chuo in 2008, sasa
nimeona ni wakati muafaka wa kufanya mambo yangu mwenyewe kwa huu mtaji ambao nimeulimbikiza kwa muda
niliofanya kazi.
nakaribisha mchango wenu wa mawazo.
the boss upo, nakukubali sana kaka kwenye hizi anga, please assist.
Kirumi, kimara.
kweli umeacha kazi, hata biashara hujaanza, wala hujui unataka kufanya nini? huo muda unaofikira unaishije? au unatumia mtaji?
Biashara nzuri change hzo pesa kuwa dolla au euro then weka ndani mwaka au miezi sita zitakuwa zimeongezeka zaid sana hata mara 50 zaid,
anza kama bakhressa
Mara nyinigi Biashara huwa inategemea na interest yako kwanza ama profession yako. Na kama ungesema labda biashara kadhaa unazopenda kufanya ili tukushauri katika hizo kulinga na uzoefu. Umeishawahi kufikiria juu ya biashara hizi.
1. Biashara ya Kuku, Kuku wa nyama ana mayai?
2. Biashara ya Kukodi Mashamba na kulima mazao ya msimu.
3. Biashara ya kununua miti na kuchana Mbao.
hizo ndio baadhi ya biashara nini uzoefu nazo.
Ni rahisi mtu kukushauri kama anajua interest zako!
wekeza kwenye kilimo, halafu kata bima ya kujikinga na hasara. huduma hiyo wanatoa CRDB.Kilimo kinalipa ila watanzania hatuko focused