Msaada wa wazo la biashara

Mhanga Mkuu

Member
Oct 21, 2020
11
5
Habari za muda huu, na poleni na harakati za kimaisha.

Nikiwa na imani na members wa jukwaa hili, nina imani kubwa nitapata mchango wa mawazo ya biashara kulingana na maeneo niliyopo na vitangulizi nilivyo navyo. Kwa uzoefu wenu, naomba nisaidiwe wazo la biashara niweze kujikwamua kiuchumi.

MAHALI NILIPO: Dar es salaam

MTAJI: Laki Tisa. Pia nina vifaa vifiatavyo; Camera Canon 7D, Printer Epson L382, Laptop na Vifaa baadhi vya saluni ya kiume, kama kiti, vioo na mashine.

Kwasasa sina kazi, nategemea madili ya kupiga picha na kuuza vitabu vya masomo ya sekondari ya fizikia na kemia, ambavyo nimekua niki viandaa na kuvi print mwenyewe. Shughuli zote hizi zimekua hazinipatii kipato cha kukizi mahitaji yangu walau ya chakula na malazi.

Kabla nimewahi kufanya biashara ya saloon ya kiume, mara mbili kwa nyakati tofauti na sehemu tofauti tofauti, ambapo ilikumbwa na changamoto mbali mbali na kushindwa kuendelea kutokana na mapato yake kutotosha walau kulipia pango ya flem. Nilijaribu kufanya biashara ya fedha za mitandao (mpesa, tigo pesa na airtel money) nazo niliishia kuuza laini baada ya kushindwa kufikia malengo ya kibiashara kwa kukosekana mzunguko wa wateja.

Nimekuja kwenu mnisaidie wazo la biashara kulingana na mtaji nilio nao na vifaa hivyo. Nimejaribu kupitia mawazo mbali mbali yaliyo kwisha kutolewa, ingawaje nimeona mawazo ambayo yatakua specific na hali yangu yatakua bora zaidi.

Nje ya mada, elimu yangu ni Shahada ya ualimu wa masomo ya sayansi, fizikia na kemia. Hivyo kama nitapata connection huku nitashukuru pia.

Mwanzo nilikua na mtaji wa around 2.5M, lakini kutokana na kila biashara ninayo ianzisha kushindwa kufanikiwa mimejikuta natumia pesa bila faida na kubakiwa na hii 900k tu. Nimekuja kwenu kabla hali haijawa mbaya zaidi ili niweze kupata wazo lenye tija kutoka kwa wazoefu, maana nahisi huenda nakosea mahali.

Natangulisha Shukrani.

======
Kwa maoni zaidi soma>>>Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?
 
Kwanza elimu uliyokuwa nayo ni mtaji tosha tu
Walim wa fizikia ni wachache sana na wanatafutwa kuajiriwa
I dnt knw y you failed to persue ur carrie

Biashara siku zote hailet faida ya haraka lazima iwe na up n down
Huwez kupata faida ndan ya miez kadhaa

Inaonekana sio mvumiliv kwa kila biashara unayofanya na unataka faida za haraka. Kwa mtazamo huo hata ukiwa uendeshe biashara za bakhesa utaona hazina faida
 
Kama vp nenda mkoani ndani wilayani huko fungua stationary & Photoshop, tution center Tena ya mwezi wa tisa pre form hela utaipata Tena hiyo na jaribu kilimo wa kumi na mbili then pre form five mwakani pia unaweza kujaribu online business kwa shutterstock ,Amazon Kindle, Fiverr, blogging.
 
Mim ni mvumilivu sana, na hua siamini katika kushindwa. Lakini mpaka kusema nilishindwa, jua nilishindwa kweli. Kuhusu career yangu ya ualimu, ninaipenda na nimekosa sehemu walau ya part time. Na siwezi kujitolea bure shuleni hali ya kua ninahitaji nipate pesa kukidhi mahitaji ya lazima kama chakula na malazi.
 
Kama vp nenda mkoani ndani wilayani huko fungua stationary & Photoshop, tution center Tena ya mwezi wa tisa pre form hela utaipata Tena hiyo na jaribu kilimo wa kumi na mbili then pre form five mwakani pia unaweza kujaribu online business kwa shutterstock ,Amazon Kindle, Fiverr, blogging.
Sina experience za hizi online business. Mkoani sina connection, ningesha enda
 
Back
Top Bottom