Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Yesu Kristo ambaye ndiye NENO la Mungu alituachia injili na Roho Mtakatifu kutuongoza safari ya Mbinguni.
Mambo yafuatayo ni machukizo mbele za Mungu
Basi enendenj mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa
Mwenye kuongeza neno la uvuvio aongezee yanayotukumbusha utume na agizo la Yesu Bwana wetu
Mambo yafuatayo ni machukizo mbele za Mungu
- Bikira Maria kws sababu hakuna maandiko yanayosapoti ibada ya kupitia Maria ili kumfikia Yesu au Mungu
- Ibada ya Sanamu. Yapo makanisa yamesimika sanamu kwenye makanisa hayo na watu wsnapiga goti kuomba rehema kupitia sanamu hizo wskiamini wapo salama
- Sanda, Yesu alituachia Imani na siyo historia hizi zilizopikwa na shetani na kulikabidhi kanisa lieneze uongo na kuwapoteza wengi
- Holly grail. Kikombe cha karamu ya mwisho. No such a thing
- Kubatiza watoto. Watoto wsnabarikiwa na wakubwa wanabatizwa baada ya kumkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wake. Mtoto anazaliwa huru hadi atakapoamua kuongoka kumfuata Yesu ndo anafanyika kuwa mkristo na mwanafunzi wa Yesu.
- Ibada za ndoa. Jambo hili limewekwa na kanisa kudhibiti waumini. Ndoa Takatifu ni pale ambapo mtu mume akishamaliza taratibu za kumposa mwanamke na hapo wanakuwa tayari wanandoa. Kuwaita watumishi wa Mungu kuombea ndoa ni jambo jema lakini watumishi hao wa Mungu kujitwalia mamlaka ya kufunga na kuvunja ndoa ni kukufuru agizo la Mungu kwenye eneo hilo
- Ibada za mazishi. Imenenwa kuwa kufa ni mara moja na baada ya kifo ni Hukumu. Hata Yesu hakufanyiwa ibada ya maziko. Hakuna sala wala tendo lolote linaloweza kubadilisha hatima ya mtu baada ya kifo chake. Jambo pekee liwezekanalo ni kumfufua endapo itampendeza Mungu. Kufanyiwa ibada baada ya kufa ni makufuru mbele za Mungu.
- Mungu kuchanganywa na Kaisari. Yesu alisema hauwezi kutumikia mabwana wawili ambapo utampenda mmoja na mwingine utamchukia. Huwezi kumpenda Mungu kisha ukaipenda fedha. Fedha ni mamlaka ya kidunia na watumishi wote walioingia kwenye mamlaka za dunia huku wakiwa na kofia zao za utumishi wana nafasi yao motoni kwa sababu wamekaidi injili na kushiriki karamu za kinyama na uharibifu.
Basi enendenj mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa
Mwenye kuongeza neno la uvuvio aongezee yanayotukumbusha utume na agizo la Yesu Bwana wetu