Hayo ni Mawazo Mazuri sana!; Ambayo ni Nccr na Nld tu, Wanaweza Kuyaafiki!; Cuf hawawezi kuyaafiki! Hivyo basi wapelekee hii Ajenda kwa walio Tayari, kwa ajili ya utekelezaji! Muda si rafiki tena kwa kusubiri!
Kumbe unalijua hilo kua chama chako nichakuhonga honga?Chadema wanachekesha,hivi hawajui Lipumba anaivuruga Ukawa makusudi.?
Lipumba ameshahongwa pesa nyingi sana na JK aivuruge Ukawa. Lipumba sio mjinga ,anajua wazi kabisa hawezi kushinda uchaguzi, Anachofanya ni kuivuruga tu Ukawa
Mnapotaka kushirikiana na mmoja akaanza kujiona yeye ni muhimu kuliko mwenzake basi hapo hakuna ushirikiano tena
Kamwe Lipumba hawezi kukubali kumwachia Slaa agombee Urais, Ameshakula hela za ccm.., subiri hiyo tarehe 25 watapiga tu dana dana ili kuwakatisha tamaa Ukawa,, Hakuna maamuzi yoyote watakayofanya. Teh trh teh,, Huu mvurugano umepangwa kiustadi sana na ccm.. Chadema wameingia kwenye mtego
Mkuu M.M Mwanakijiji, mimi nadhani huyu jamaa wa CUF hajaelewa vizuri siasa zinavyokwenda kwa sasa hivi. Uimara wa CUF anaoongelea kwa upande wa huku bara ni upi? Pamoja na ujio wa ACT bado CHADEMA kimezidi kuimarika zaidi. Tena mimi nikiangalia kwa makini, ninaona kama kufukuzwa kwa Zitto Kabwe na genge lake kumeifanya CHADEMA iwe imara zaidi kuliko kipindi kile walipokuwemo CHADEMA. Utagundua kuwa wakati Zitto Kabwe bado yuko CHADEMA na kundi lake, kulikuwa na CHADEMA mbili ndani ya chama kimoja. Kufukuzwa kwa Zitto Kabwe a.k.a Supreme Leader au Ayatollaaah na genge lake kumeifanya CHADEMA ibaki na viongozi ama wanachama ambao ni waaminifu na wafia chama. Zitto Kabwe na genge lake walipofukuzwa CHADEMA, waliondoka na wale watu wote ambao walikuwepo CHADEMA si kwa sababu ya kuamini katika itikadi, falsafa na sera za CHADEMA, bali katika mtu binafsi ambaye ni Zitto Kabwe. Na kwa sehemu kubwa Zitto Kabwe alitumia muda wake mwingi kujijenga yeye binafsi kuliko kujenga chama.
Aidha, kitu kinachoipa nguvu CHADEMA sasa hivi, ni kujijenga kitaasisi zaidi na kutokutegemea sana viongozi wakuu au watu maarufu katika kuendesha mambo yao ikiwemo mikutano ya hadhara, na ufunguzi wa matawi. Ni kipindi hiki cha mwaka 2010-2015 ambacho tumeshuhudia CHADEMA ikijipanua zaidi kutoka mijini hadi vijijini, na kuanza kujenga mashina na matawi katika ngazi za chini kabisa kule vijijini. Hali hii imeifanya CHADEMA ianze kung'oa ile mizizi ya mashina vijijini ambayo ilikuwa inategemewa sana na CCM nyakati za uchaguzi. Kutokana na mambo kama hayo tunashuhudia CHADEMA, angalau kwa mwaka huu imekuwa na watia nia wengi sana tofauti na miaka ya nyuma. Mfano, juzi niliona kwenye tovuti yao watia nia wa Ubunge wakiwa wanafika takribani 900, na bado wanaendelea kuchukua fomu. Mwaka 2010 ambapo CHADEMA ilifanya vizuri idadi ya wagombea wa Ubunge ilikuwa 186 tu. Ina maana hawakusimamisha wagombea wa Ubunge majimbo yote, achilia mbali watu waliorubuniwa. Kwa mara ya kwanza CHADEMA wataenda kufanya kura za maoni km CCM ili kupata wagombea wa Ubunge na Udiwani nchi nzima.
Kwa maana hiyo, mwaka huu haturajii CCM wapite bila kupingwa katika majimbo yote, labda kutokee mapingamizi ya kisheria zaidi. Sasa hao CUF anaosema wako imara, bado msemaji wao alikuwa anahamasisha watu waendelee kuchukua form za kugombea. Majimbo mengi hawataweza kusimamisha wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani. Mimi bado ninaamini CHADEMA wameshafanya harakati za kutosha sana mijini na vijijini. Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana ulitupa picha kidogo tu ya matokeo halisi ya mwaka huu. Ndio maana binafsi ninaungana na ushauri wako ulioutoa kwa sababu CHADEMA wasipokuwa makini watapoteza zaidi kwa kujifunga katika zimwi hili la UKAWA, ilhali wana uwezo wa kusonga mbele.
Kuhusu ACT uimara wake ni wa bahati nasibu na kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Kama ACT wataanza kutegemea zaidi wabunge wa CCM ambao wataachwa kwenye kura za maoni lazima tuhoji uimara wao. Hayo ni makosa ambayo CHADEMA walikuwa wanayafanya huko nyuma, mfano tuliona John Shibuda alivyowasumbua CHADEMA. Pia, wagombea wengi wa CCM kwa mwaka huu wanaweza wasiwe na mvuto wa kuchagulika sana na wapiga kura. Wengi wao wataangushwa mwaka huu kwa sbb wananchi wamewachoka kutokana na style yao ndiooooooo! bungeni na wanahitaji mabadiliko. Kuwachukua wagombea kama hawo kunaweza kusiwe na maana sana katika kujenga chama imara. Isipokuwa, wale wagombea ambao wataamua wenyewe kuhama kwa hiari kabla ya kura za maoni.
Kamwe Lipumba hawezi kukubali kumwachia Slaa agombee Urais, Ameshakula hela za ccm.., subiri hiyo tarehe 25 watapiga tu dana dana ili kuwakatisha tamaa Ukawa,, Hakuna maamuzi yoyote watakayofanya. Teh trh teh,, Huu mvurugano umepangwa kiustadi sana na ccm.. Chadema wameingia kwenye mtego
Afadhali wewe umeona mbali kidogo!
CHADEMA haina turufu hata moja ya kuviburuza vyama vingine vinavyounda UKAWA kwasababu uwanja wa kisiasa nchini, 2015, ni tofauti sana na ule wa2010 na hata ikisema isimame yenyewe ni wazi kuwa ina mengi ya kupoteza kuliko kufaidika (haitaki shahada ya uzamili kuliona hili!)
CUF inaogopa kupoteza maslahi yake, endapo haitaweka mgombea, na kwakua CHADEMA imechukua majimbo mengi ya Ubunge kwanini isiwaachie NCCR au CUF kusimamisha mgombea uraus?
KWA KIFUPI, NAFIKIRI ULE MUDA WA KUMWAGA UGALI NA MBOGA UMEFIKA, KAMA SIO CHADEMA KUJIREKEBISHA NA KUHESHIMU VYAMA VINGINE NDANI YA UKAWA!
Cdm ni chama chenye wafuasi wengi na ushawishi kwa upinzani lkn bila ukawa nchi hii ni kitendawili, nawasihi wanaukawa wamentain umoja wao na kuomba wasiwe vipande vipande, mtafika ccm furaha yao ni kupasuka kwenu maana hata waliondani na wanataka kutoka wanaangalia nguvu yenu kwanza.
Magufuli ndiyo rais! Hatuwezi weka mzinzi ikulu
Mi ccm siwataki,ukawa siwaamini NISHAURINI NDUGU YENU
Kimahesabu ni majimbo mangapi ambayo ukijumlisha kura za wapinza na jumla ya kura alizoshinda mgombea wa ccm na ikawa kura za wapinzani ni nyingi ndio utajua hoja yako inakosa mantiki
Na ukichukua kura za Dr na Prof ukizijumlisha pamoja unaweza kuona ni jinsi gani ushirikiano huu unaweza kuwa na mntiki kubwa zaidi kuliko wakienda mmoja mmoja kivyake
Mnapotaka kushirikiana na mmoja akaanza kujiona yeye ni muhimu kuliko mwenzake basi hapo hakuna ushirikiano tena
Hivi hata kabla sijakujibu labda unisaidie jambo moja. Ni kwanini unafikiria UKAWA ni Muungano wa vyama vya upinzani Tanzania au inawakilisha "Umoja" wa vyama vya upinzani? Maana hayo mengine yote unayasema inaonekana yamejengwa katika msingi potofu - kwamba UKAWA ni umoja wa vyama vya upinzani.