Nisikilizeni CHADEMA: Tatizo ni UKAWA, Hili ndilo chaguo langu la rais wa 5

Sifahamu sana kuhusu mambo ya UKAWA, zaidi ya kirefu cha neno UKAWA ila nilipenda tu kujua kama ni kweli ulipinga tangu mwanzo wakati wanatengeneza huo UKAWA kwa nguvu zote kama unavyofanya sasa hivi!

ndio maana nimekushauri tumia search engine hapo juu kutafuta mada nilizoanzisha tangu UKAWA ilipogeuka kuwa na nia ya kutaka kushinda uchaguzi. Ndio maana nimekuuliza nikusaidia kutafuta?
 
Sidhani kama umechelewa kivile; kwa sababu bado mambo mengi yanahitaji kufanyika. NI suala la kuamua tu kuweka bolts nyingine wapi lakini ikibidi kuwa huru basi na iwe.
Kwa sasa Chama kitakachoonekana kuvunja ushirika huu kitaadhibiwa na kutikisika kwelikweli kwa sababu itakuwa kinyume cha matarajio waliokwishaaminishwa wengi. Vingine vitakavyobaki vitapata msukosuko kidogo lakini vitabaki salama. Kanuni hii aliisema Nyerere akiongelea muungano.
 
Sidhani kama iko haja ha kuuvunja hasa bali CDM ichukue uongozi wa kute geneza jmoja wenye nguvu zaidi kulilo ilivyo sasa. Na wananchi waeleweshwa vizuri tu.
Muda hauko pamoja nao na wanatakiwa kuwa na adhari wasionekane wao ndiyo chanzo cha kuvurugika ushirikiano huo, kwa sababu negative publicity itakayotoka hapo itakuwa ya nguvu kweli pande zote upinzani na chama tawala/serikalini. Bado wana nafasi kuendeleza ushirika huo lakini kwa adhari.
 
MM, uchambuzi barabara!

CDM wafahamu kwamba walikosea sana kufanya muendelezo wa kuwepo kwa UKAWA baada ya majadiliano kuhusu katiba kule bungeni.

Tumeona jinsi mtu mmoja alivyojipenyeza kwenye kambi ya Lowasa na akafanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa na tukashuhudia yalotokea kule Dodoma.

Hivyo, sioni mantiki ya UKAWA tokea mwanzo iwapo hakuna mkono wa upandikizi kutoka kwa hawa jamaa wawili Lipumba na Mbatia.
 
Mzee Mwanakijiji! umenikosha, kwakweli hata Mimi ni maono ambayo nilikuwa nayaota japo kwa huku kwetu TZ huwaga mala nyingii mambo ya msingi kupelekeshwa kwa emotions za hovyo.

Yeah umoja ni nguvu, lakini unakuwa nguvu kwa kuzingatioa nature ya waunganaji, ukijaribu kuweka umoja wa mafuta na maji expect Ku fail, it will never happen to be nguvu!

CDM tukili tumeingia kichwakichwa, viongozi wetu wangejaribu kuwa na maamuzi shirikishi zaidi rether than emotional! lakini hatujachelewa, nachelea kusema labda tubadili strategy na Ku base kwenye umoja wa the willing kwa kuwa jamii yetu imeanza kuelewa maana halisi ya ukawa sasa hebu uwepo lakini it should be a coalition for the willing!

Tuzunguuke lakini ukweli ni kuwa CDM ndio itakuwa inawabeba hao wengine, kama ni wazito please tuwatue and tufight kivyetu jamii itatuelewa for wanakumbuka 1995 we supported NCCR, then CUF, we have never been selfish!
 
Atleast imejulikana kwamba CDM haikuwa inavizarau vyama vingine ilikuwa tayari kushirikiana navyo.Naomba iyo tarehe 25 ifike cuf watangaze kujitoa,ili tuwe na huru wa kwenda kusini kutangaza ukombozi alafu kwa dar tuzoe majimbo yaliyobakia.tuone baada ya 2015 kama CUF itarud na jimbo lolote kutoka Tanzania bara,maana wanaukaata muungano ambao ungewarudisha kwenye ramani za siasa za tanzania bara.watu wapo tayari kuyaachia majimbo ambayo wameinvest kwa muda mrefu kwa ajili yao alafu wao wanaleta mchezo.NI NGUMU SANA KUTEMBEA NA MTU AMBAYE HANA VISION
 
Tukitafakari na kuangalia muda unavyoyoyoma ni wazi sasa umefika wakati wa Chadema kumtaja mgombea wao wa kiti cha urais na kuachana na hii fantancy ya UKAWA.
 
Ni kweli mkuu. Wanasema subra huvuta heri ila sasa hii imezidi isije ikawa shari.
 
Atleast imejulikana kwamba CDM haikuwa inavizarau vyama vingine ilikuwa tayari kushirikiana navyo.Naomba iyo tarehe 25 ifike cuf watangaze kujitoa,ili tuwe na huru wa kwenda kusini kutangaza ukombozi alafu kwa dar tuzoe majimbo yaliyobakia.tuone baada ya 2015 kama CUF itarud na jimbo lolote kutoka Tanzania bara,maana wanaukaata muungano ambao ungewarudisha kwenye ramani za siasa za tanzania bara.watu wapo tayari kuyaachia majimbo ambayo wameinvest kwa muda mrefu kwa ajili yao alafu wao wanaleta mchezo.NI NGUMU SANA KUTEMBEA NA MTU AMBAYE HANA VISION

Aisee point ya muhimu sana. Chadema endeleeni kuwa wanyenyekevu. Mtu akiamua kujitoa basi ajitoe mwenyewe bila kisingizio. Lakni kusema eti chadema isitoe mgombea urais is a joke. Prof. Lipumba tunategemea busara zako kuokoa huu umoja. Puuza wanachama wanoingiza udini katika hili swala. Huu umoja unaifavor sana CUF na naona wakinapata wabunge zaidi ya kumi kutoka kwenye mmoja walie naye sasa. Itakuwa ajbau sana km CUF wataikataa hii opportunity. Itabidi tujiulize kwamba wako serious kiasi gani km chama kinachotaka kurudisha nguvu zake? Unless labda wana mshiko wa uhakika kutoka CCM. Lakini huu ushirikiano hakuna atakayepoteza, wote watapata. Infact chadema ndiye atapoteza kiasi Fulani kwa kuachia majimbo ambayo tayari ameshajijenga. CUF think twice otherwise mtapotea kwenye siasa.
 
How come mpaka tarehe 25 ndio CUF wakae kijadili kama wataruhusu mgombea mmoja wa UKAWA?Inakuaje vyombo vya maamuzi vya CUF havijakaa kuamua suala hilo mapema?walifikiri UKAWA ni mzaha?
 
Tukitafakari na kuangalia muda unavyoyoyoma ni wazi sasa umefika wakati wa Chadema kumtaja mgombea wao wa kiti cha urais na kuachana na hii fantancy ya UKAWA.

Wanaogopa aibu itakayowapata mbele ya wana UKAWA wenzao na wale wa chama tawala. Watakuwa wameipatia CCM mtaji wa kuwamaliza!
 
How come mpaka tarehe 25 ndio CUF wakae kijadili kama wataruhusu mgombea mmoja wa UKAWA?Inakuaje vyombo vya maamuzi vya CUF havijakaa kuamua suala hilo mapema?walifikiri UKAWA ni mzaha?

CUF hawasomeki, tarehe 25 ni mbali ukizingatia wenzao wako tayari wao ndio wanaochelewesha kisa 'vuguvugu' ndani ya chama

Kwanini hilo 'vuguvugu' litokee mda huu ambapo UKAWA walishasema watataja mgombea wao tarehe 14?
 
Wanaogopa aibu itakayowapata mbele ya wana UKAWA wenzao na wale wa chama tawala. Watakuwa wameipatia CCM mtaji wa kuwamaliza!
Futa neno Aibu katika siasa.isitoshe CHADEMA imeibeba sana UKAWA lakini inaonekana haibebeki.
 
Back
Top Bottom