Nisikilizeni CHADEMA: Tatizo ni UKAWA, Hili ndilo chaguo langu la rais wa 5

Naambiwa blaza Mtei ana dictate mambo...Dr Slaa anasema anarudisha kadi mkisimamisha Lowassa

Lowasa yupi jamani ndani ya CHADEMA ? Ndugu yangu (binafsi) sijakuelewa. Au labda niulize tu, Lowasa amejiunga na CHADEMA? Kama bado, sasa iweje watu mlete hisia ( assumptions) zenu humu? Kwahiyo tunajadili hisia na sio reality.
 
Siku ya siku utaikumbuka hii post..
 
Mtayasema mengi sana mwaka huu wakati niliwapa kila hoja inayoonyesha UKAWA ni wachumia tumbo. Chadema waliharibu wenyewe walipomfukuza Kitila, Mwigamba na Zitto kwa sababu wangeweza kuwa contain within the party hadi Uchaguzi huu kwa sababu ilikuwa mpango wa CCM kuhakikisha Chadema inajimaliza yenyewe. Niliwaasa mkasema Mkandara anajifanya anajua! Haya yakowapi...

Haya makosa yalishafanyika, basi ungananeni oooh haiwezekani, siasa za Bongo haiwezekani hakuna kiongozi anayetaka kuwa chni ya mwingine!... damn sasa mliendelea kubebana ili iweje?. majibu yenu UKAWA wamesimama imara kutetea katiba ya wananchi hadi kwenye uchaguzi mkuu?..Maskini wanaotetea pumba kwa sababu wanalipwa fedha! ni hatari kabisa wataweza vipi kulipa hizo fadhila!

UKAWA hawana jinsi, it's too late now na hata kama kila chama kijikate na kuanza upya nyote mtapoteza kabisa imani ya wananchi waloiweka kwenu na kibaya zaidi hata yale majimbo mlokusudia kuyapata hamtayapata tena. Hiki ndicho kilikuwa kilio changu muda wote kwa sababu nawajua WADANGANYIKA ni FITNA na UNAFIKI mwanzo mwisho. 1. WAONGO, 2. WAKIAHIDI HAWATIMIZI na 3. WAKIAMINIWA hufanya KHIYANA.. Haya yote yametimia.
 
ukawa+px.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Dr. Magufuli hapo na chama chake watapata mchecheto wa karne. CCM kwa kumpitisha kimizengwe Magufuli wameuliza swali tu ambalo jibu lake wanalihofia; wanalitetemekea na wanaliombee lisiwe; Dr. Willbroad Slaa.

Niandikie:Mwanakijiji@jamiiforums.com

Mkuu MJJ,

Analysis yako iko biased na haijaeleza lolote zaidi ya kupanga hoja za kuwasuta wengine, eg. Prof. Lipumba, na kumpamba chaguo lako Dr. Slaa bila kuelezea kasoro zake zozote. Vimbwanga vyake vyote alivyoibuka navyo Dr. Slaa, kuanzia ndoa na vimada, hadi kukaa kwake kimya na kuburuzwa na Mbowe wakati wa mbinu za kumtimua Zitto kutoka kwenye chama, ni sifa mbovu za kiongozi ambazo hukuzigusia kabisa. Ulichongalia tu ni kujulikana kwa jina lake ambalo kwa sasa umaarugu wake umeshafifia kupita kiasi. Madhambi yake itakuwa ni sherehe kwenye kampeni za CCM hasa ukilinganisha na utendaji bora na usafi wa Magufuli.

Ni muhimu kwa UKAWA / CHADEMA kufikiria kwa upana kama walivyofanya CCM na kuchagua kiongozi anayelingana na nyakati na kuachana na viongozi ambao wameoza kama Dr. Slaa, Lowassa, Mbowe n.k..

CCM tatizo lao kubwa ilikuwa ni rushwa na utendaji mbovu, walichofanya ni kuchagua kiongozi aliye mtendaji na msafi. Magufuli akipambanishwa na Dr. Slaa, mzee ambaye ana madhambi kibao yanayofahamika na kila mtu, hiyo itakuwa ni kifo CHADEMA na UKAWA.
 
KJ wewe ukijisikia unaweza tu kiweka mabaya hayo kama unavyoyajua.
 
Madhambi gani ya Dr. Slaa unayosema kuwa na vimada? unafurahisha, nilifikiri utazungumzia issues za kitaifa kama kuuza nyumba za serikali zinazogusa wananchi wote, kama dhambi ya Slaa ni kuwa na vimada unafikiri Magufuli ni msafi kwa hilo? tena yeye mbaya zaidi kahonga hadi nyumba ya serikali.
 
Ukawa wanamtafuta kiongozi atakayeishinda ccm. Cuf hawaamini kwamba Slaa atashinda.Tatizo la cuf,naambiwa,ni kujiita chama cha waislamu. Hiyo ndiyo inawakosesha kura.
 
Hayo ni Mawazo Mazuri sana!; Ambayo ni Nccr na Nld tu, Wanaweza Kuyaafiki!; Cuf hawawezi kuyaafiki! Hivyo basi wapelekee hii Ajenda kwa walio Tayari, kwa ajili ya utekelezaji! Muda si rafiki tena kwa kusubiri!
 
Hivi mtu kama Professor anashindwa kusoma alama za nyakati? Mtu ambaye ana vision ya kimataifa anaongozwa na tamaa? Anashindwa kujua kuwa siasa za kiafrika kuna shortcut? UKAWA ndo ilikuwa shortcut ya wapinzani walau kupata wabunge na kupunguza zile ndiyooooo za upande mmoja bungeni.

Mimi niko miongoni mwa watu wanaoshangaa hii sintofahamu inayoendelea ndani ya UKAWA. Muda umekwisha hawajatoa mgombea wakati Magufuli ashaanza kuchanja mbuga. Kwakweli wakiongozwa na tamaa na wakapoteza hii nafasi, watapoteza muda na matumaini ya watu na watapoteza hata walichonacho.
 
Hiyo ni kuwa intellectually dishonest. Umeandika zaidi ya maneno 4500 ya kuchagua kiongozi wa nchi, halafu unasema mimi ndio nikaandike upande wa pili wa habari yako? Hiyo habari itakamilikaje nusu huku nusu kule? Kwa nini usiweke picha halisi yaa Dr. Slaa?

Mkuu Kubwajinga mimi nimekuelewa sana, nafikiri hawa watu wawatafute viongozi wa CHADEMA wakaenao chini wawashauri kuwa ni busara CHADEMA wakajitoa UKAWA hii itawasaidia sana kuliko kutupigia kelele kila siku na kuwapa sifa za kijinga kina Dr. Slaa haisaidii kitu.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ni kuwa intellectually dishonest. Umeandika zaidi ya maneno 4500 ya kuchagua kiongozi wa nchi, halafu unasema mimi ndio nikaandike upande wa pili wa habari yako? Hiyo habari itakamilikaje nusu huku nusu kule? Kwa nini usiweke picha halisi yaa Dr. Slaa?

Kwa nini ulifikiria naandika kitu hakiko biased. CCM wamemtaja Magufuli na kutuambia ndio chaguo lao umeona wanapita kutuambia ubovu wake? Si ni jukumu la upinzani kufanya hivyo?
 
Mwanakijiji umeyagusa yale ambayo Cuf tumeyaomba kwa muda mrefu. Hao ndugu zako hawasomeki na fuatilia kila ukiwaambia kupitia vikao hawatoi majibu ya maana ndio maana cuf tumeona tufunge gavana.
Kuhusu chadema kuwa chama imara bara nadhani unajidanganya... mambo yamebadilika na ujio wa ACT imewapunguza kasi zaidi. Cuf bado tupo stable.
 
I would not go to that extent and assert that; ila naweza kusema tu kuwa ACT inategemea nguvu yake kwenye Uchaguzi huu kutoka kwa watu watakoachwa vyama vingine hasa kutoka CCM.
 
Ubinafsi mtupu, Ukawa ni vyama vyote kama kweli lengo ni kuwakomboa watanzania kutoka kwenye mikono dhalimu ya CCM na mafisadi lazima mgombea atoke chadema au CUF?

kwanini wasikubaliane tu kama Chadema na CUF wana nguvu ya kupata viti vya ubunge na uwakilishi, basi NCCR Mageuzi au NLD watoe mgombea urais ambaye kwa nguvu ya pamoja atanadiwa na kuungwa mkono na wapenda mabadiliko wote wakiwa chama chochote, hiyo haibadilishi hadhi ya chama chochote kuwa ni kikubwa au kidogo, kitakachobadilika ni kuwa Tanzania itakuwa imeingia kwenye utamaduni mzuri wa kimageuzi kama walivyofanya wenzetu Kenya, kujidai jidai hapa siju chama gani kina nguvu wapi na wapi, huo ni ubinafsi ambao hauna msingi wowote.

Na kama tutaendelea kama hivyo, ni sawa na kukubali CCM iendelee kutawala si kwasababu inapendwa na uwezo wa kushinda, bali kwasababu ya udhaifu, ubinafsi na kushindwa kimikakati kwa vyama vya upinzani...vinavyotazama nani na kutoka wapi agombee na siyo mkakati gani wa kuunganisha nguvu zidi ya CCM na Mafisadi.

Ninachoamini kama Ukawa watakubaliana kikweli CCM haina muda kutawala Tanzania.

Afadhali wewe umeona mbali kidogo!
CHADEMA haina turufu hata moja ya kuviburuza vyama vingine vinavyounda UKAWA kwasababu uwanja wa kisiasa nchini, 2015, ni tofauti sana na ule wa2010 na hata ikisema isimame yenyewe ni wazi kuwa ina mengi ya kupoteza kuliko kufaidika (haitaki shahada ya uzamili kuliona hili!)

CUF inaogopa kupoteza maslahi yake, endapo haitaweka mgombea, na kwakua CHADEMA imechukua majimbo mengi ya Ubunge kwanini isiwaachie NCCR au CUF kusimamisha mgombea uraus?
KWA KIFUPI, NAFIKIRI ULE MUDA WA KUMWAGA UGALI NA MBOGA UMEFIKA, KAMA SIO CHADEMA KUJIREKEBISHA NA KUHESHIMU VYAMA VINGINE NDANI YA UKAWA!
 
I would not go to that extent and assert that; ila naweza kusema tu kuwa ACT inategemea nguvu yake kwenye Uchaguzi huu kutoka kwa watu watakoachwa vyama vingine hasa kutoka CCM.

Mkuu M.M Mwanakijiji, mimi nadhani huyu jamaa wa CUF hajaelewa vizuri siasa zinavyokwenda kwa sasa hivi. Uimara wa CUF anaoongelea kwa upande wa huku bara ni upi? Pamoja na ujio wa ACT bado CHADEMA kimezidi kuimarika zaidi. Tena mimi nikiangalia kwa makini, ninaona kama kufukuzwa kwa Zitto Kabwe na genge lake kumeifanya CHADEMA iwe imara zaidi kuliko kipindi kile walipokuwemo CHADEMA. Utagundua kuwa wakati Zitto Kabwe bado yuko CHADEMA na kundi lake, kulikuwa na CHADEMA mbili ndani ya chama kimoja. Kufukuzwa kwa Zitto Kabwe a.k.a Supreme Leader au Ayatollaaah na genge lake kumeifanya CHADEMA ibaki na viongozi ama wanachama ambao ni waaminifu na wafia chama. Zitto Kabwe na genge lake walipofukuzwa CHADEMA, waliondoka na wale watu wote ambao walikuwepo CHADEMA si kwa sababu ya kuamini katika itikadi, falsafa na sera za CHADEMA, bali katika mtu binafsi ambaye ni Zitto Kabwe. Na kwa sehemu kubwa Zitto Kabwe alitumia muda wake mwingi kujijenga yeye binafsi kuliko kujenga chama.

Aidha, kitu kinachoipa nguvu CHADEMA sasa hivi, ni kujijenga kitaasisi zaidi na kutokutegemea sana viongozi wakuu au watu maarufu katika kuendesha mambo yao ikiwemo mikutano ya hadhara, na ufunguzi wa matawi. Ni kipindi hiki cha mwaka 2010-2015 ambacho tumeshuhudia CHADEMA ikijipanua zaidi kutoka mijini hadi vijijini, na kuanza kujenga mashina na matawi katika ngazi za chini kabisa kule vijijini. Hali hii imeifanya CHADEMA ianze kung'oa ile mizizi ya mashina vijijini ambayo ilikuwa inategemewa sana na CCM nyakati za uchaguzi. Kutokana na mambo kama hayo tunashuhudia CHADEMA, angalau kwa mwaka huu imekuwa na watia nia wengi sana tofauti na miaka ya nyuma. Mfano, juzi niliona kwenye tovuti yao watia nia wa Ubunge wakiwa wanafika takribani 900, na bado wanaendelea kuchukua fomu. Mwaka 2010 ambapo CHADEMA ilifanya vizuri idadi ya wagombea wa Ubunge ilikuwa 186 tu. Ina maana hawakusimamisha wagombea wa Ubunge majimbo yote, achilia mbali watu waliorubuniwa. Kwa mara ya kwanza CHADEMA wataenda kufanya kura za maoni km CCM ili kupata wagombea wa Ubunge na Udiwani nchi nzima.

Kwa maana hiyo, mwaka huu haturajii CCM wapite bila kupingwa katika majimbo yote, labda kutokee mapingamizi ya kisheria zaidi. Sasa hao CUF anaosema wako imara, bado msemaji wao alikuwa anahamasisha watu waendelee kuchukua form za kugombea. Majimbo mengi hawataweza kusimamisha wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani. Mimi bado ninaamini CHADEMA wameshafanya harakati za kutosha sana mijini na vijijini. Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana ulitupa picha kidogo tu ya matokeo halisi ya mwaka huu. Ndio maana binafsi ninaungana na ushauri wako ulioutoa kwa sababu CHADEMA wasipokuwa makini watapoteza zaidi kwa kujifunga katika zimwi hili la UKAWA, ilhali wana uwezo wa kusonga mbele.

Kuhusu ACT uimara wake ni wa bahati nasibu na kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Kama ACT wataanza kutegemea zaidi wabunge wa CCM ambao wataachwa kwenye kura za maoni lazima tuhoji uimara wao. Hayo ni makosa ambayo CHADEMA walikuwa wanayafanya huko nyuma, mfano tuliona John Shibuda alivyowasumbua CHADEMA. Pia, wagombea wengi wa CCM kwa mwaka huu wanaweza wasiwe na mvuto wa kuchagulika sana na wapiga kura. Wengi wao wataangushwa mwaka huu kwa sbb wananchi wamewachoka kutokana na style yao ndiooooooo! bungeni na wanahitaji mabadiliko. Kuwachukua wagombea kama hawo kunaweza kusiwe na maana sana katika kujenga chama imara. Isipokuwa, wale wagombea ambao wataamua wenyewe kuhama kwa hiari kabla ya kura za maoni.
 
Chadema wamebugi sana kuungana na hicho chama cha Buguruni, Hiyo CUF haina nguvu yoyote zaidi ya Zanzibar
 
Back
Top Bottom