Nishaurini mdogo wenu nipo njia panda

Irene marwa

Member
Jul 25, 2020
35
36
Me ni yule niliyeuliza kuhusu kuwa na mimba ni kweli nilipima na nikakuta ni mjamzito wa mwezi mmoja ila shida me nipo mbali na wazazi na kwa sasa nipo chuo.

Yaani mpka mwakani mwezi wa sita ndo namaliza na hapo chuon huwa tunavaa uniform nashindwa hata kuelewa nifanye nini lakini kuhusu baba wa mtoto kakubali Kulea mimba. Sasa naombeni ushauri jamani maana me sihitaji kuwaelezea wazazi kwa sasa mpka ntakapomaliza chuo na kutoa mimba siwezi kabisa.

Nishaurini mdogo wenu nifanye nini maana yeye mwanaume kakubali kunipangia chumba na mahitaji mengine ila shida nitaendaje chuoni na tumbo kubwa na pale tunavaa uniform si nitakuwa wa ajabu wenye mawazo naombeni mnisaidie.
 
Yaani hato ungeyaweka kwenye equation wakati umemuachia baba kijacho ajiachie bila condom......!!!! Anyway, sio muda wa kulaumiana. Kama utaona so kwenda na ushahidi kwamba umezini, nakushauri omba kuahirisha mwaka.

Lakini jihakikishie kwamba kuna miundombinu ya kuendelea kusoma baada ya kujifungua, kama vile ada, support kwa mtoto na mengineyo. Na kwa tahadhari tu, kusoma huku unalea kichanga ni challenging.
 
Kwani kuwa na tumbo ajabu? Nani asiejua tumbo na mimba?wewe nenda kwa wazaz na tumbo lako wakikufukuza nenda kwa jamaa yako.
 
Kwahiyo wewe ofu yako ipo juu ya kuvaa uniform uku ukiwa na mimba au juu ya wazazi wako.

Shida sio uniform maana naweza tu kuongea na uongozi nikashona gauni ila shida ni kubwa n kuhusu wazazi nafikiria nisiwaambie kitu mpka ntakapohitimu
 
Kama umekubaliana na changamoto zingine, mimi nakushauri tumbo likianza kuonekana ujishonee uniform za kijanja. Pia sio kila mwanamke akibeba mimba tumbo linajaa
 
sihitaji kuwaelezea wazazi kwasas mpka ntakapomaliza chuo na kutoa mimba siwezi kabisa nishaurini mdogo wenu nifanye nn
Sio sahihi wazazi kutojua hili swala.

Ni vyema ukaanza kuzungumza na mama, anza kwa kumueleza kuwa tayari umepata mchumba na yuko tayari kuja kujitambulisha ili mumtambue, Utaona nini atakueleza na kukushauri.

Kisha swala la mimba lifuate baada ya hili la kwanza kulifanikisha.
 
Kwani vyuo vinawafukuzawajawazito/waliopata mimba wakiwa chuoni?
 
Kuna msichana alikuwa anasoma chuo fulani kati ya huko mwanza au moshi namfahamu. Mwaka juzi alirudi home kwa wazazi wake akiwa na mtoto,wazazi wakashangaa, ksbb walikuwa hawana taarifa kabisa ya ujauzito,alikuja kuwa-suplies na kichanga, lakini maisha yakaendelea. Kama chuo haitakuwa shida wewe maliza tu kwanza usiwaambie wazazi.

MUHIMU ongea na mumeo na wakwe hiyo hali kwamba hutawaambia wazazi wako mpaka umalize chuo na ujifungue,ila wakuhakikishie utaenda nao kwenu hata wakajitambulishe on advance tu.

Wasiwasi ni wewe kusoma kwa kutokujiamini hapo chuo kutokana na hiyo hali. Kama utakuwa vizuri we zaa tu. Muhimu uwe na uhakika kabisa na baba kijacho wako,maana baadae asije akakugeuka. Kuzushi japo nijibu-ndio wewe hapo avatar hiyo?
 
Kuna msichana alikuwa anasoma chuo fulani kati ya huko mwanza au moshi namfahamu. Mwaka juzi alirudi home kwa wazazi wake akiwa na mtoto,wazazi wakashangaa,ksbb walikuwa hawana taarifa kabisa ya ujauzito,alikuja kuwa-suplies na kichanga, lakini maisha yakaendelea...

Ndiyo
 
Kwanza lazima wazazi wafahamu mapema hilo swala sababu hata baadae ukitaka ndo uwaambie bado watapiga hesabu na kugundua uliipata mimba shuleni, nadhan hofu yako kuu iko hapo kwa wazazi.

Pili ni wenzio kukuona ukiwa unaenda chuoni na ujauzito au tumbo kubwa, hilo wala lisikuumize kichwa ila hujaandika kama chuoni kwako wanaruhusu wajawazito kuendelea na masomo yao iwapo kuna mazuio hayo hapo lazima uhairishe mwaka kama hamna zuio basi endelea na chuo.

Ushauri wangu ni vyen kuwapa taarifa wazaz muda huu na pia uanze kufuatilia kanuni na sheria za chuo chako kama ni ualimu sawa haina shida ila kama uko veta sahau hiyo elimu mpka ukijifungua.
 
yani uzazi wako mama mkweo ndio akushughulikie?? mama atabaki kua mama heri uongee na huyo baba k wako mkubaliane tu aende kwenu akajitambulishe na aseme yeye ndio mhusika wa hilo tumbo heri hii itawauma wazaz lakini there is no way watafanya wakiangalia mhusika kaja mwenyewe kidogo itawapunguzia hasira
 
Hakuna kitu kigumu kama Mzazi kukubali Mwanae ana Mimbaa hasa kipindi hiki Unasomeshwaa na kulipiwa Ada yani utapataa tabu sanaa lakini HAKUNA MZAZI ANAEKATAA MJUKUUU so point ni Kwamba sababi jamaa kakwambia atakusupport ili kuepusha shari na nyumbani kaushaa kabisaa mpaka utakapojifungua au ukikariboa kabisaa sio kipindi hiki mimba bado changa.

Pale ukiwapelekea mtoto watamind lakini kidogo sanaa na watafurahii piaa ila now ukiwaambia aisee Watakumind mnoo yani utakula msotoo sana so kaushaa tu cha muhimi una support ya jamaa.
 
Back
Top Bottom