Nishaurini mdogo wenu nipo njia panda

Nishaurini mdogo wenu nipo njia panda

Bila shaka usharud kwa wazazi wako, umeaibisha wengi kwa hilo tumbo
 
Me ni yule niliyeuliza kuhusu kuwa na mimba ni kweli nilipima na nikakuta ni mjamzito wa mwezi mmoja ila shida me nipo mbali na wazazi na kwa sasa nipo chuo.

Yaani mpka mwakani mwezi wa sita ndo namaliza na hapo chuon huwa tunavaa uniform nashindwa hata kuelewa nifanye nini lakini kuhusu baba wa mtoto kakubali Kulea mimba. Sasa naombeni ushauri jamani maana me sihitaji kuwaelezea wazazi kwa sasa mpka ntakapomaliza chuo na kutoa mimba siwezi kabisa.

Nishaurini mdogo wenu nifanye nini maana yeye mwanaume kakubali kunipangia chumba na mahitaji mengine ila shida nitaendaje chuoni na tumbo kubwa na pale tunavaa uniform si nitakuwa wa ajabu wenye mawazo naombeni mnisaidie.
Matokeo ya tuma na ya kutolea ndio hayo, ungelisoma kwanza mapenzi baadae
 
Pole kwa changamoto, nadhani kwa takwimu zisizo rasmi hii ni nchi inayoongoza kwa watu kuzaa kabla ya kuoana hivyo haupo mwenyewe ndio trend ya sasa.

Ongea na mwalimu uwe unavaa nguo kubwa au sweta litakaloficha uhalisia. Ukikaribia kushusha chukua likizo/ahirisha muhula.

Wazazi haswa mama yako au dada kama yupo, ni muhimu kuwajulisha lolote laweza kutokea, pia utawahitaji haswa mama kwa usaidizi na ushauri baada ya kujifungua.

Hivyo, ikifika miezi sita mpigie mama mueleze hali halisi mwambie uliteleza. Atahuzunika lakini ndio ukubwa atajilaumu malezi yake aliyokupa mwanae na pia atakupongeza kwa kulea mjukuu mtarajiwa.
 
Naaamini tumbo lako...litakuwa lishakua Sasa...Chakufanya Ni kushona uniform Kubwa.. ili usibane tumbo...
 
Utapendeza tu, shona nguo kubwa kubwa waiter fanya kuniongezea konyagi kubwa [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji482][emoji482][emoji482][emoji482][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom