Nishati ya kutumia majumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nishati ya kutumia majumbani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtumiabusara, Jan 5, 2012.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani watanzania wenzangu,
  Naomba tushauriane ni nishati gani nafuu ya kutumia majumbani kupikia hasa kwa watu wa kipato cha chini au cha kati tunaoishi mjini? Maana bei ya gesi au mkaa ni zaidi ya Sh. 50,000. Umeme ndo huo huwezi kupikia na haupatikani kwa uhakika. Mafuta ya taa sina uhakika kama yanaweza kukidhi haja.

  Hivi kwa nini tusitumie gesi asilia kutoka mikoa ya kusini kupikia badala yake tunategemea gesi ya kutoka nje? Ambayo bei yake hatuwezi kuidhibiti?
   
 2. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu hii ni hoja nzuri na ngumu kidogo.
  Kwanza kabisa mimi ni mdau katika nishati na ninapenda watu watumie nishati ambayo inapatikana wakati wote, bei poa na rafiki wa mtumiaji (haina madhara).

  Suala la kutumia gesi yetu lina utata mwingi kwakuwa "wenye nguvu" hawataki kuona unapata nishati ya bei poa "kwani wao hawatauza ile ya kwao wanayoileta toka majuu".-NOTE: Biashara ya mafuta na gesi yote inafanywa na "wenye nguvu".
  Gesi yetu ya asili ina uwezo wa; KUTUMIKA MAJUMBANI KUPIKIA, KUZALISHA UMEME NA KUJAZA KWENYE MAGARI YOTE KUANZIA BAJAJI HADI MABASI YA GHOROFA. Kwa kulijua hili "wenye nguvu" wanaona giza mbele yao, hivyo wanahakikisha "hatutoki" kwenye kununua vya kwao.

  Ushauri wangu; Wakati tukisubiri "uhuru wa Tanganyika/Tz" unaweza kutumia teknolojia ya "BIOGAS" ambayo mini ni mtaalam. Kwa mtu yeyote mwenye nafasi katika maeneo ya nyumbani kwake, awe na mifugo au hana anaweza kuzalisha biogas kwaajili ya kupikia na kwaajili ya matumizi mengine. Ili biogas izalishwe "mtambo wa biogas"(Biodigester) unatakiwa kusanifiwa, kujengwa na vifaa vyake kufungwa tayari kwa matumizi. Mtambo mdogo ambao unatosha matumizi ya familia utachukua siku 25-30 kuujenga na ukishajengwa unadumu miaka 35-40. Kama uko interested kupata taarifa zaidi ni-PM.

  Faida za mtambo wa biogas ni pamoja na; Kutumia nishati ambayo unazalisha mwenyewe, unaipata wakati unapoitaka, unazalisha mbolea ya asili (organic manure), mazingira yanakuwa safi na salama, hakunaa madhara ya moshi, inalipa ndaani ya miaka kati ya 3-5.
   
 3. N

  Ngoiva Lewanga Senior Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumia kuni, magunzi, au kinyesi cha ng'ombe.
   
 4. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi wako. Labda unaweza kutujulisha gharama za huo mradi ili watu wote wenye interest tuweze kunufaika. Lakini nichojiuliza wataalam wetu wa uchumi, waheshimiwa wabunge na wadau wengine hivi kweli wote kwa pamoja tunashindwa kujenga hoja ya kutetea suala hili ambalo litatupunguzia ugumu wa maisha?
   
 5. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kaka mjini utapata wapi hizo malighafi kwa gharama nafuu kuliko mkaa, gesi na umeme?
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  u

  mkuu unacho sema ni sahihi kabisa 100% biogas ni nzuri sana na ukisha install ndo imetoka wewe ni kutumia tu,

  ila mkuu kila kitu kina vikwazo vyake, kwa upande wa biogas vikwazo vyake ni hivi

  1. Biogasi inatumiwa kwa mtu mwenye nyumba yake tu, vipi walio panga?

  2. Mkuu kwa walio panga hii haiwezekani kabisa,

  3 hata kama umejenga nyumba yako inatakiwa uwe na eneo la kutosha make mfumo wa choo za biogasi ni tofauti na hizi tulizo zizoea.

  Biogas ni nzuri sana lakini uwe na nyumba yako mwenyewe, ukiwa umepanga kwenye magorofa ya nhc hii kitu haiwezekani
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hebu nielekeze hapo kwenye kinyesi cha ng'ombe
   
 8. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu Komandoo na wengine; Teknolojia ya biogas ni pana sana, vikwazo vyote ulivyozungumzia hapo juu vyaweza kuvukwa. Kwa wenye nyumba zao na nafasi watafaidi zaidi kwa kupata mtambo wa kudumu muda mrefu bila longolongo. Kwa walio kwenye nyumba za kupanga na wana nafasi ningewashauri kujadiliana na land lords wao ili waingie jv ya kujenga huu mtambo.
  Kwa wale walio kwenye nyumba za kupanga na wasio na nafasi au wenye nafasi lakini hawawezi kufanya lama nilivyoshauri hapo juu, pia wale walio kwenye NHC na hata maghorofani; unatakiwa uwe na space kama 2sqm ili kuweza kuweka mtambo wa kuhamishika. Sehemu ya verandah au balcony ni ideal kwaajili ya hili. Mitambo hii ya kuhamishika si imara kama ile mingine.

  Kwa mitambo yote aina mbili nilizotaja haihitaji kuunganishwa na choo. (i.e it's not mandatory).

  Karibuni kwenye nishati mbadala!
   
 9. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mkuu eucalyptos tupe japo kontact zako basi, kusema tu 'karibuni kwenye nishati mbadala', wapi? kumbuka hii ni JF, be open.
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Chief Eucalyptos, im in. But ungeweka hadharani estimated cost za hiyo plant kwa matumizi ya nyumban ingekuwa vizuri zaidi na ingekuwa na effect kubwa zaidi kwa wadau wa JF. Thanks
   
 11. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Biogas kwa mkoa wa DAR,Pwani kuna offer ya COSTEC ,wanakutengenezea kwa gharama ya laki2 tu.
  ni mradi uliofadhiliwa na wazungu.unachotakiwa ni kutoa eneo na vifaa vya ujenzi.
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Then gharama yake ni zaidi ya laki2.
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  nazungumzia gharama za labour na utalaam.unatakiwa uwe na eneo na vitofali size ya tofali za kuchoma,kokoto/mawe,na plastic pipes za 1/2 "'
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  @ eucalyptos
  Thanks kwa useful info; najua utakuwa unazungumzia Biogas from kitchen waste, kwa wale wasio na mifugo. Lkn kwa umaskini na kipato chetu waTZ wengi, do u know how much waste tunaproduce? Kwa waste ninamaanisha mabaki ya chakula (maganda ya ndizi, nyanya, ukoko etc).

  How many liters of gas do a family of 5 need to cook 3 meals a day? Na how many liters of kitchen waste does a digester need to produce that amount of gas?

  Nafikiri ni vyema na ni busara kuwaambia watu kuwa; huwezi zalisha gas ya kutumia siku nzima bila kukusanya mabaki ya chakula from hotels etc; pia njia nyingine kama supplement ni solar heaters, ambayo if u have warm water utapunguza cooking time hivyo energy pia!
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kama huna mifugo na uko kwenye nyumba ya kupanga; the minimum you need ni:-
  1.two simtanks na bomba la Maji taka kubwa
  2.some few plumbing fittings
  3.bacterias (from mavi ya ng'ombe)
  4.jiko la gas (modified for methane)
  5. lots of water.

  1000l gives you 2 hrs of cooking time but requires at least 20l of uji uji wa mabaki ya chakula!

  Check na website ya ARTI hasa India
   
 16. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Good Staff inafaa kwa wanaopenda kuitumia, nimeipenda. Big Up
   
 17. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  WAKUU NASHUKURU KWA MAONI MAZURI,ila bado tuna changamoto kubwa, hiyo biogas inaweza kupata vikwazo vya kupata hizo taka
   
 18. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #18
  Jan 10, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani suala la bei bado ni muhimu, minimum cost that someone will have to apy ni kiasi gani ndugu?!?!?!?!
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  About 600,000/= to 1,000,000/= kwa materials na pia yategemea amount ya cooking gas one needs.

  Ila challenge kubwa ni hiyo mabaki ya chakula; kwa wenye migahawa this is the type of energy ifaayo, kwani unamanage waste zako.
   
Loading...