Nishati Jadidifu: TotalEnergies yafanya tena kweli, yaongoza njia. Waziri Makamba aipongeza, awataka wengine wafuate

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Japo Tanzania tunaagiza mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, kwa uagizaji wa pamoja, yaani Bulky Procurement, lakini ubora wa mafuta hayo haufanani, mafuta ya TotalEnergies ndio mafuta bora zaidi, kutokana na kuongezwa kiambata kiitwacho excellium, kinachoyafanya mafuta yao kuwa bora zaidi.

Sasa licha ya TotalEnergies kuongoza kwa mafuta bora zaidi, dunia ya sasa inaelekea kwenye matumizi ya nishati Jadidifu, "cleaner energies", kwenye matumizi ya nishati hizi jadidifu, Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, imefanya kweli tena, imeongoza kwa kufungua njia ya matumizi jadidifu nchini Tanzania, kwa kutumia nishati ya jua, kuendesha vituo vyake vyote vya mafuta zaidi ya 100 Tanzania nzima, hivyo kuokoa matumizi ya umeme wa gridi ya taifa. Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewapongeza kwa hili, na kuwataka wengine waige mfano wa TotalEnergies.

Andamana nami katika Safu yangu, ya Jumapili ya hii.

Screen Shot 2022-03-28 at 8.10.16 AM.png
Screen Shot 2022-03-28 at 8.13.07 AM.png

Matumizi ya Nishati Jadidifu, Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies, Yaongoza Njia, Wengine Wafuate.

Wiki hii imeanza kwa uzinduzi wa Kituo cha kwanza cha mafuta nchini Tanzania, kutumia nishati jadidifu, ambapo kituo hicho kinatumia nishati jua, kuendesha kila kitu, hivyo kupunguza matumizi ya umeme, na kutumia umeme safi, rafiki wa mazingira, (clean energy, eco friendly).

Kituo kilichozinduliwa ni kituo cha kampuni ya mafuta ya TotalEnergies kilichopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam, na uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania, Ltd., Bwana Jean-Francois Schoepp amesema kati ya vituo zaidi ya 100 vya vya mafuta vya TotalEnergies nchini, vituo 24, tayari vimeishafungwa umeme jua, na kufikia mwaka 2023, vituo vyote vya TotalEnergy vitatumia nishati jua.

Uamuzi huu wa TotalEnergy kutumia nishati mbadala ni uamuzi wa busara sana na wa ki maendeleo endelevu, hivyo kufaa kupigiwa mfano na makampuni mengine. Busara za uamuzi huo ni kuukubali ukweli wa hali halisi ya nishati yetu ya umeme kwenye grid ya taifa, ya megawati 1,600, kwa nchi kubwa kama Tanzania yanye watu milioni 60, umeme hautoshi na matumizi makubwa ya umeme kuliko uwezo wa transformers ni moja ya visababishi vya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara kwa transfoma kukata (trip),

Hivyo matumizi yoyote ya nishati jadilifu kwa mtu yoyote, taasisi yoyote, kampuni yoyote au ofisi yoyote, tuu ni kujisaidia kwa kupata umeme jadilifu, bali ni kulisaidia taifa kwa kutoa fursa kwa Mtanzania mwingine kutumia umeme wa grid, na kulipunguzia taifa mzigo wa umeme kwenye grid ya taifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Nishati, January Makamba, amewapongeza TotalEnergies kwa kuzindua kituo cha kwanza kinachoendeshwa na nishati ya umeme jua, na kusema matumizi ya umeme jua, umeme wa upepo, umeme wa joto ardhi na umeme mwingine wowote jadidifu, ndiko dunia inakokwenda, hivyo hongera sana Total kuonyesha njia, wengine wafuatie.

Waziri Makamba, amesema, Rais Samia amedhamiria kuifanya Tanzania kuwa ni kitovu cha biashara ya Nishati ukanda huu wa Afrika Mashariki, kati na Kusini”.

Waziri Makamba anasema na hapa ninamnukuu “Tanzania imedhamiria kufanya mapinduzi makubwa ya nishati, kwa kuifanya nishati ya kupikia, kupatikana kwa wingi na kwa urahisi zaidi, kufuatia asilimia 70 ya nishati yote Tanzania, kutumika kwa kupikia, ikifuatiwa na mafuta na umeme. Nishati kubwa inayoongoza kutumika n kupikia, ni nishati ya Tungomotaka (biomass).

Ila katika haya mambo ya nishati ya mafuta na gesi, inayoagizwa kutoka nje ya nchi, kuna jambo moja kubwa la ajabu ambalo mimi ambaye sii mchumi silielewi, baadhi ya nchi majirani zetu, wanaagiza gesi, mafuta ya taa, petrol na dizeli, kupitia bandari ya Dar es Salaam. Mafuta hayo na gezi hiyo, inasombwa kwa malori ya mafuta, mpaka nchini mwao, kitu cha ajabu ni kwa nchi hizo kuuza mafuta kwa bei nafuu kuliko Tanzania. Wakazi wote wa mikoa ya mipakani, kujikuta wananunua mafuta ya jirani zetu kwa bei nafuu kuliko mafuta yetu.

Total Energies Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya TotalEnergies inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na

bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo.

085A8417.jpg
TotalEnergies Group Photo.jpeg
TotalEnergies Photo 1-Uzinduzi.jpeg
TotalEnergies Service Station.jpeg


Ukifika vituo vya mafuta vya TotalEnergies, lile paa linaloonekana kwenye vituo hivyo, sio tuu ni paa, lile ni li solar panels kubwa la kunyonya solar energy kuzaliza umeme jua wa kuendesha kituo hicho.

Enzi za Mwalimu, baadhi ya bidhaa muhimu zikiwemo, mbegu, mbole na pembejeo za kilimo, zilifanywa bei nafuu kuliko hata bei halisi kwa kupewa ruzuku ya serikali ili wananchi wamudu gharama. Kuna wakati wa uhaba wa maji, Tanesco ilikuwa inatumia gharama kubwa kuzaliza umeme wa gesi na mafuta na kuuza kwa bei ndoa kama ya umeme wa maji ili kutowabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama.

Hali ya nishati ya nchini Tanzania, sio nzuri, watu 22,000 wanapoteza maisha, kila mwaka kutokana na magojwa ya upumuaji yanayosababishwa na moshi wa kupikia kwa kuni na mkaa, hivyo kufuatia hali hiyo, kipaumbele cha kwanza kwenye sekta ya nishati, ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu na inafika kwenye kila nyumba, hivyo kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Kama Tanesco iliweza kuuza umeme kwa bei ya chini, na enzi za Mwalimu kulitolewa ruzuku kwenye bidhaa muhimu, na enzi za JPM, gharama za kuunganishwa umeme wa REA, zilikuwa ni Shilingi 27,000 tuu, na tumeshuhudia hadi vijumba vya nyasi, vimeunganishwa na umeme.

Jee kuna ubaya gani serikali ya Mama Samia, ikaondoa kodi zote kwenye ikiwemo VAT kwenye majiko ya gesi na gesi ya kupikia?. Mbona kwenye computes tumeondoa kodi?!. Nini muhimu kati ya compyuta na jiko la gesi?!. Hawa Watanzania wenzetu elfu 22, wanaokufa kila mwaka kwa matatatizo yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, maisha yao yangeokolewa kwa matumizi ya gesi na umeme!.

Mimi naamini tukiamua tunaweza, nina imani sana na Mama Samia, akiamua Watanzania tupunguze kupikia kuni na mkaa, kwa kuondoa kodi kwenye vifaa vyote vya nishati jadidifu zikiwemo sola panels, na gesi, anaweza, Tanzania tunaweza.

Wasalaam

Paskali
 
Pascal napenda makala zako zenye hoja...ila nahisi uko kazini kwa ujumla wake: kiumoja umoja na kiwingi wingi
 
Pascal napenda makala zako zenye hoja...ila nahisi uko kazini kwa ujumla wake: kiumoja umoja na kiwingi wingi
Mimi ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, nafanya kazi ya uandishi kwa mapenzi tuu, sio kwa kupata chochote, na nafanya bure.

P
 
Hiyo nishati "jadilifu" si wangetuuzia tuweke kwenye magari kuliko hii bei ya petroli?
Wao wanatumia cleaner energy ili kupunguza matumizi ya umeme wa gridi ya taifa a.k.a kupunguza gharama za umeme. So wao wana save cost while at the same time sisi wanatuumiza na mafuta. I dont see how hili ni suala la kushangilia
 
QUOTE="Pascal MayallaView attachment 2166599View attachment 2166600
Matumizi ya Nishati Jadi

View attachment 2166610View attachment 2166611View attachment 2166613View attachment 2166614

Ukifika vituo vya mafuta vya TotalEnergies, lile paa linaloonekana kwenye vituo hivyo, sio tuu ni paa, lile ni li solar energy kubwa, la kuzaliza umeme wa kuendesha kituo hicho.

Enzi za Mwalimu, baadhi ya bidhaa muhimu zikiwemo, mbegu, mbole na pembejeo za kilimo, zilifanywa bei nafuu kuliko hata bei halisi kwa kupewa ruzuku ya serikali ili wananchi wamudu gharama. Kuna wakati wa uhaba wa maji, Tanesco ilikuwa inatumia gharama kubwa kuzaliza umeme wa gesi na mafuta na kuuza kwa bei ndoa kama ya umeme wa maji ili kutowabebesha wananchi mzigo mkubwa wa gharama.

Hali ya nishati ya nchini Tanzania, sio nzuri, watu 22,000 wanapoteza maisha, kila mwaka kutokana na magojwa ya upumuaji yanayosababishwa na moshi wa kupikia kwa kuni na mkaa, hivyo kufuatia hali hiyo, kipaumbele cha kwanza kwenye sekta ya nishati, ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu na inafika kwenye kila nyumba, hivyo kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Kama Tanesco iliweza kuuza umeme kwa bei ya chini, na enzi za Mwalimu kulitolewa ruzuku kwenye bidhaa muhimu, na enzi za JPM, gharama za kuunganishwa umeme wa REA, zilikuwa ni Shilingi 27,000 tuu, na tumeshuhudia hadi vijumba vya nyasi, vimeunganishwa na umeme.

Jee kuna ubaya gani serikali ya Mama Samia, ikaondoa kodi zote kwenye ikiwemo VAT kwenye majiko ya gesi na gesi ya kupikia?. Mbona kwenye computes tumeondoa kodi?!. Hawa Watanzania wenzetu elfu 22, wanaokufa kila mwaka kwa matatatizo yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, maisha yao yangeokolewa kwa matumizi ya gesi na umeme.

Mimi naamini tukiamua tunaweza, nina imani sana na Mama Samia, akiamua Watanzania tupunguze kupikia kuni na mkaa, kwa kuondoa kodi kwenye vifaa vyote vya nishati jadidifu zikiwemo sola panels, na gesi, anaweza, Tanzania tunaweza.

Wasalaam

Paskali
[/QUOTE]
Mie Nilicho Kipenda Ni hapo Kuanzia Enzi za Nyerere basi Hayo mengine Bakinayo
 
Kadanganye wengine pia uweze kuwapumbaza, aliyekwambia kuwa mwandishi wa kujitegemea hupati kitu Nani?. Wabongo bhana aliyeturoga kafa
Kazi ya uandishi ni kazi ya wito. Zaidi ya uandishi, kuna shughuli nyingine ninazofanya za kuniingizia kipato, hivyo siutegemei uandishi wa habari kuendeshea maisha yangu, kazi ya uandishi naifanya bure kwa kujitolea kutokana na mapenzi tuu na sio kipato. Silipwi chochote na media yoyote kwa kuwapelekea habari zangu.

P
 
Duuh hizo gharama za pump za solar watakaozimudu ni hao hao mabeberu na bado hapo panel na inveter.

ukipigiwa hesabu utaona bora ukubaliane na hawa hawa ambao bwana Febu kama kajitoa hivi maana kiukweli kwenye hili yeye kama mwenye dhamana alitakiwa awashawishi waachane na mpango huo na badala yake awahakikishie kuwa umeme wetu utakuwa stable siku zote na miaka yote.

Ni kama kaenda kutangaza biashara ya solar hapo kwa kuihujumu tanes...

Mimi nakumbuka muitaliano mmoja nilikuwa nikifanyanae kazi shirika fulani alikuwa akishangaa sana umeme kukatika katika na akanieleza wao kwao kwa miaka yake 35 ya kuwa na akili timamau hajawai kuona umeme ukikatika hata mara moja na hapo ilikuwa ni miaka ya 2003 nipo na huyo mtu.

Hivi wote tukihamia kwenye solar hilo shirika litakuwa na hali gani na wakati kwa sasa wao wako pekee na hawajiwezi??
Hao total kutumia solar sytem ni kwamba umeme wetu kwa asilimia kubwa hauaminiki japo wamesema nishati jadidifu ila cost ya mafuta kwa ajili ya genarator ipo juu na kama utajiweza kwenye solar ni afadhali ujifungie hii.
 
Back
Top Bottom