Ni vyema umeomba ushauri, ni hekima maana ushauri utakusaidia katika maamuzi yako, inategemea wapi umeomba ushauri maana inaweza kupelekea kuanguka zaidi au kusonga mbele, umeeleza kuwa kuna Mzungu amekupenda,nilivyosoma nilitamani kujua muitikio wako wa kihisia uzuri umeeleza kuwa haumpendi,huwezi kuwa na furaha+amani kwa mtu usiyempenda ndugu, maisha si bahati ila ni mipango, kujituma na kumuomba Mungu, mara nyingi sana tunatolea mfano kuwa Barkhresa alikuwa fundi viatu halafu tunarukia kuwa leo anamiliki makampuni mengi, tunasahau kujiuliza hapo kati kipindi cha mabadiliko! Nafikiri alipitia mengi,usikubali kununuliwa kwa hela kijana mwenzangu,hakuna kitu kizuri katika mapenzi kama amani+furaha,pili anataka usahau kabisa mambo ya Mungu ibariki Tanzania pole! Kaa na huyo umpendae, omba Mungu+ fanya kazi utafanikiwa.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums