Nisaidieni jibu la kumpa mwanangu...

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
31,275
31,404
Mwanangu kanikuta nipitisha macho kwenye thread.."nini tofauti ya polisi hawa".. Nipofika kwenye picha za polisi wa kike akaniuliza.. Baba unaangalia nini? Nikamjibu nasoma magazeti. Akaniuliza., yameingiaje humo kwenye simu? SINA JIBU
 
Mwambie ulikosea kusema. Unasoma habari, husomi magazeti. Alafu mwambie waandishi wa habari waliandika wakaweka kwenye 'mtandao' na vingine wakachapa kwenye magazeti, vingine tena wakaweka TV na redio. Sasa wewe umeamua kusoma zile za kwenye mtandao, na mtandao wenyewe unaupata kupitia sim, compyuta na tabloids. (or keave the tabloids for now, unless you have it at home)
 
Mwambie watoto wanatakiwa wawe wamelala muda huu au wakubwa huwa hawaulizwi maswali na watoto.
 
Mwambie watoto wanatakiwa wawe wamelala muda huu au wakubwa huwa hawaulizwi maswali na watoto.
Mtoto aliuliza swali mapema kidogo ila baba alikosa jibu ndio bado anamweka macho... labda akamlaze alafu tuendelee kumtafutia jibu
 
Ili kuilinda akili yake isichanganyikiwe na maelezo mengi kwako yazungukayo kama bara bara za treni au majibu mafupi na mazito mithili ya jibu fumbo kwa kwa swali fumbo, muelekeze namna linavyofunguliwa hilo gazeti, then aki practice na kufuzu mwambie kuwa wameandika huko huko kwa na kuweka kutuma kwenye kompyuta za watu.
Mengine atayajua taratibu kupitia elimu dunia
 
Mjibu kama utakavyo mjibu mtu mzima, kama wewe unaelewa jibu lake na kama hulijui basi mfahamishe kuwa utalitafuta jibu umpe, na ulitafute kweli na umpe kweli haraka iwezekanavyo.
 
Mpe mfano wa picha zilivyoingia mu-simu ili kumwelewesha zaidi...
 
mfundishe computer ni nini na matumizi yake.mwanao ana bahati babaake ana computer nyumbani na ni dalili njema kwani uelewa huanzia udadisi
 
Wala usimdanganye, mwambie ukweli tena kwa kutxmia lugha rahis,mambo ya 'yu noo, yu noo ze cp yuu' achana nayo. Watoto wa siku hizi wanaelewa mambo mengi na wanauelewa mkubwa wa mambo tofauti na tunavyo wachukulia
 
Back
Top Bottom