- Thread starter
- #181
Swali zuri sana mkuu na limekua likileta shida sana kwenye familia zetu.Dokta huwa nasikia kuwa kuna baadhi ya group zadamu huwa haziendani katika kupata watoto endapo mnapokuwa mke namume au wapenzi.
Swali langu je mimi mwanaume nina group O- namwenza wangu wakike ana O+ vipi hapo kwenye kupata watoto hatuwezi Pata shida
Kabla sijajibu swali lako fuatilia maelezo yafuatayo.
Tatizo hili Kiko kwenye group tunaloliita kitaalamu "Rhesus factor incopatibility"
Hiyo Rhesus fotor Ni aina ya protein ipo kwenye damu zetu, ambaye anayo hiyo factor tunamuita Rhesus foctor positive (Rh+), ambaye hana anaitwa Rhesus foctor negative (Rh-).
Watu wengi wako kwenye kundi la Rh+. Na factor hii uweza kurithishwa toka kwa baba kwenda kwa mtoto.
Sasa ukiwa wewe mwaume ni Rh+ na mkeo ni Rh-, mtoto wenu atakua Rh+.
Sasa mama mjamzito ambaye ni Rh- akibeba kichanga chenye Rh+ , mwili wa mama utazalisha antibodies na kukishambulia kichanga, na hapo mimba huaribika.
Mara nyingi tatizo hili utokea kwa mimba zitakazotungwa baada ya ujauzito wa kwanza. Hapa ndo unasikiaga watu wakisema mama yule alizaa mwanae wa kwanza vizuri, ila mimba zilizofuata zote zinaharibika!! Msipoelewa tatizo mtaanza kushikana uchawi.
Kitu Cha kuzingatia ,ukiwa mjamzito ,mme na mke fikeni clinic ,mtafanyiwa uchunguzi na mtaelekezwa namna bora za kuzibiti hali hiyo.
Nadhani nimekusaidia.