Waziri wa miundombinu wa zanzibar hamad masud mh.Hamad Masudi amesema yupo tayari kujiuzuru
Sosi:bbc
Hapo kwenye Red ndiyo ujinga wa viongozi wengi, "eti nipo tayari kujiuzuru endapo tume itadhibitisha uzembe"! Tume gani tusubiri wakati hiyo Meli ilikuwa na idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wake?
Ni uzembe gani anaosubiri utamkwe na tume? Au anadhani tume itasema waziri alitakiwa kwenda kuhesabu idadi ya watu?. Ebu asitupotezee wakati kwa kujifanya yeye muwajibikaji wakati hajui lolote.
Kwa taarifa yake; Leo nimesikia abiria wakilalamika na kusema jana abiria wa kwenda pemba kwa boat ya "Seagull" walizuiwa kuingia bandarini kwa sababu idadi ya abiria kwenye boat ilikuwa ishatitosha japo na wao walikuwa wamekatiwa ticket za boat hiyo hiyo. Aliyekuwa anafanya kazi ya kuhesabu na kuzuia watu kuingia ni serikali si mwenye boat!
Kama huyo waziri anajua utaratibu huu uliotumika jana kwenye boat hii iweje asijue kuwa utaratibu huo ulikiukwa kwa meli ya Spice? Nilisikia kwa masikitiko kuwa abiria walionusurika wakilalamika eti walitaka wapunguzwe na mizigo ipunguzwe wakapuuzwa!!!!!!!
Waziri huoni uzembe bado? Huyo waziri hana tofauti na viongozi wengine anaojaribu kujitofautisha nao (Like Husein Mwinyi na milipuko ya mabomu)!