Waziri Tabia Mwita Aweka Bayana Mkakati wa Maboresho ya Miundombinu ya Michezo Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

WAZIRI TABIA MWITA AWEKA BAYANA MKAKATI WA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MICHEZO ZANZIBAR

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Mwita Maulid akiwa katika Ufungaji wa Mafunzo ya Siku 10 ya Twende Olympics 2024 kwa Makocha na Walimu wa Michezo wa Skuli mbalimbali amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayo mikakati ya kufanya maboresho makubwa sana katika Sekta ya Michezo kuanzia kuboresha miundombinu ya Michezo mpaka kuendeleza vipaji vya watoto.

"Tunapozungumza Sera ya Michezo tunahakikisha kwamba Zanzibar inakuwa na miundombinu bora ya Michezo. Kwenye hili tumpongeze sana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada zake kubwa za kuhakikisha miundombinu ya Michezo nchini inaimarika na inakuwa bora" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar

"Tunayo program ya uendelezaji na uimarishaji wa viwanja vya michezo ambapo tumejitahidi sana kuhakikisha tunavikarabati ikiwemo Uwanja wa Amani, wengi wenu mnashuhudia yanayoendelea tunaukarabati uwe wa kisasa ambao utakuwa na vigezo vinavyotakikana na FIFA na CAF kwa lengo la Zanzibar kufikia kiwango cha kimataifa kama nchini zingine" - Mhe. Tabia Mwita Maulid.

"Tukishapeana mafunzo tutahitaji viwanja vya kuyatumia mafunzo yetu ya kutunufaisha sisi na vizazi vinavyokuja. Tunajenga Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa na viwanja vya vingine nje viwili vidogo. Tunajenga ukumbi mkubwa wa stadium ambao utaweza kuchezesha Basketball 🏀, Netball, Volleyball 🏐 na Michezo mingine, na ukumbi wa Judo, kumbi za mikutano kwaajili ya kuendesha mafunzo na shughuli mbalimbali" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri, Zanzibar

"Tunakwenda kujenga viwanja viwili viwili kwa kila Wilaya. Kuna Wilaya zitapata viwanja vya mpira wa miguu na kuna Wilaya zitapata viwanja vya michezo mingine. Lengo ni Wilaya zinakutana Tunajenga urafiki, tunaimarisha afya zetu, tunajikinga na tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri, Zanzibar

"Tunayo sheria ya Baraza la Michezo la Taifa. Tuna changamoto, kuna vyama vina zaidi ya miaka 15 havijafanya uchaguzi, viongozi ni hao hao, hakuna maendeleo kwenye michezo kwasababu viongozi wameendelea kuwa na mawazo mgando wameshakuwa watu wazima. Tunajitahidi kuhakikisha vyama vyote vilivyosajiliwa michezo karibu 41 tuhakikishe tunafanya chaguzi tunaweka viongozi imara ambao wanajua nini maana ya michezo" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri, Zanzibar

"Lazima tuone Zanzibar tunachangamkia fursa za michezo mbalimbali kwasababu vipaji vipo. Ukienda kwenye mchezo wa riadha, hatujawahi kushiriki riadha tukafanya vibaya, tunafanya vizuri. Nimefurahi kuona Muunganiko wa washiriki. Najua ujumbe utafika sehemu nyingi" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri, Zanzibar.

"Tunakuja na mpango wa kuibua vipaji, hii ni program ambayo ipo muda mrefu na kwenye Sera ipo, tunaishia kuwachukua watoto wetu kwenye elimu bila malipo, UMISETA, UMITASHUMITA, tukimaliza tunawaacha. Haiwezekani, lazima kwenye Mitaala ya Elimu tuwe na kipindi cha michezo vya watoto maana vipaji vinazaliwa mashuleni na siyo kwingineko" - Mhe. Tabia Mwita, Waziri, Zanzibar

"Nimefarijika kuona wanawake kwa kiasi kikubwa wanakwenda kushiriki katika michezo na hatujalisahau kundi la watu wenye ulemavu, Ndugu zetu wanafanya vizuri na wanatuwakilisha vizuri hasa walipoenda kwenye Olympics l, Germany 🇩🇪" - Mhe. Tabia Mwita Maulid, Waziri, Zanzibar
 

Attachments

  • 34098927.jpg
    34098927.jpg
    28.9 KB · Views: 3
Back
Top Bottom