Nipe maoni yako juu ya hadithi yangu

FirstClass

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,081
1,338
Story inahusisha jamaa wanne na mdada mmoja, kwa pamoja wanakuwa MTU TANO.

Jamaa walijihusisha na utoaji wa misaada kwa jamii, si kanisani wala misikitini, kote walialikwa na huko walitoa pesa na vifaa mbalimbali vya thamani hali hiyo ilipelekea makundi mbalimbali ya watu kupanga foleni kwa lengo la kusaidiwa na kuomba misaada.

Pamoja na mazuri yote toka kwa ndugu hawa, lakini jamaa hawakuwai kuwa na utu ndani ya mioyo Yao, walikuwa ni washenzi zaidi ya ushenzi wenyewe.

Ndani ya jumba walimokuwa wakiishi, palikuwepo na chumba maalumu kilichotumika kwa kutesa na kuuwa watu wasio na hatia. Ilikuwa ni kheri ukapelekwa Gontanamo Bay lakini si ndani ya chumba cha Hawa mabwana. Chumba kilipewa Jina la Death Penalty!! Yani ukibahatika kuingia ndani ya chumba, basi utaitwa Marehemu mtarajiwa. Ndani ya chumba palikuwa na aina5 za adhabu, hapakuwa na ruhusa ya kuchagua adhabu, ila utachagua kupitia mtindo wa vikaratasi, na adhabu zote mwisho wake n kifo tena ni ndani ya siku5 pekee, ukisalia Hai baada ya hizo siku tano basi uongozi utaona ni kwa namna gani wakumalizie ili ukakutane na Malaika wa mbingu. Kwa hiyo kifo ilikuwa ni kama kanuni ya Pai.

Yupo mama wa vijana wawili nae alipambana kuona ni kwa jinsi gani ataweza kupata msaada wa ufadhili kwa vijana wake. Wajuba hawakuwa na shida, walimkubalia na Rasmi walikabidhiwa vijana wale..

Ilitengenezwa picha kama kuna chuo nje ya nchi kimepatikana, hivyo wanatakiwa wajiandae kwa safari. Mama na vijana wote kwa pamoja walifurahi sana kupokea taarifa ilee..

Bda ya kufika Airport MAMA aliagwa na kutakiwa kurudi nyumbani, lakini bda ya daki chache kupita waliamuriwa wapande kwenye Gari kwani kuna document za muhimu zilisahaulika nyumbani..

Safari iliwapeleka paka DEATH PENALTY. Maskini vijana walee..

Ndani ya chumba, kuna dokta ameajiliwa kwa kazi moja tu, kutesa kwa kutumia dhana za kitaalamu, lakini dokta yule ni kama chizi mental, kwa hiyo yeye hajui kitu kinaitwa huruma.

Baada ya kukosekana kwa mawasiliano kati ya mama na wanawe, mama alianza kupatwa na wasiwasi. Lakini hakupata msaada wowote toka kwa mabwana wale..

Ilimbidi aripoti swala lile kituo cha polisi kwa msaada. Jarada la kesi alikabidhiwa askali makini aliyeitwa Samia.
Kutokana na heshima ya mabwana wale, Samia hakuona jinai yoyote dhidi ya watu wale, aliamua kuwapigia simu na kuwaita ofisi ili kuwashirikisha malalamiko ya Mama yule..

Kilichomtia mashaka Afande Samia ni kutajiwa Jina la chuo kinachodahiri wanafunzi wa Open University pekee, aliwaza kwa nini vijana wale waliondoka nchini.

Aliamua kuwasiliana na Uongozi wa chuo ili kuuliza km wanataarifa za vijana wale. Chuo kilisema hakiwafahamu vijana wale..

Samia alifika Uwanja wa ndege ili kujiridhisha juu ya safari ilee, database zilionesha ni kweli vijana wale walilipa nauli na kupewa siti namba, lakini mpaka ndege inaruka vijana wale hawakuwepo eneo la abiriwa..

Samia hakuishia pale,alienda mpaka kwenye server za CCtv Camera, kule aliona gari likiwashusha lakini bda ya mda walipakiwa tena na kupelekwa kusikojulikana..

Baada ya kukusanya ushahidi, Afande Samia aliuwasirisha kwa Mkuu wake wa kazi aliyemwagiza shughuli ilee..

Vipi wakuu niendele au nawachosha tu
 
Ili stori yako ilete mantiki lazima iwepo sababu kwanini wale 'Ze 5' walikuwa wanatekeleza mateso na mauaji na huku wakijivika taswira njema kwa jamii kupitia kutoa misaada.

Bila muunganiko wa kimantiki katika Mambo hayo mawili (yaani misaada na mauaji) hadthi yaweza onekana nzuri lakini ikaishia kuwa kioja cha bongo movies za hapo nyuma; mfano, Kaka Jambazi kuvua viatu wakati anavamia, au jini/zimwi kuvamiwa na kupigwa rungu kichwani Kisha likadodoka baada ya kuviziwa kutoka nyuma na mtu ambaye jini / zimwi hilo lilikuwa linamwinda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom