Nionavyo kuhusu sakata la Mbowe na NHC

Nionavyo kuhusu sakata la Mbowe na NHC

Issue hapa ni jinsi lilivyotekelezwa sio uhalali wa madai
Ulitaka wakampigie goti?Mimi nikidaiwa na mwenye nyumba huku mtaani naona tabu yake.yeye naye alipe.KUPATWA KWA MBOWE tareh1-9-2016
 
naamini huu ni mkakati mwengine kwa chadema,, ni suala la mtu binafsi.. lilitakiwa liende ki ubinafsi lakini wamelifanya kuwa la kisiasa... wamekurupuka tena ngoja tuoni safari hiii ni ngoma ya wapi itachezwa
 
Kukwepa kodi ni kuhujumu uchumi, wapelekwe mahakamani.

Haiwezekani wahubiri mabadiliko kumbe wao ndio wa kwanza kuwaibia wananchi.

Chama la hovyo sijawahi kuona, wanayohubiri ni kinyume na wafanyayo.

Watanzania wenye akili timamu hawana hamu na machadema.
Mkuu inaonyesha una hasira sana,jaribu kuzipunguza Kwa kunywa maji bariiiiiiiiidi.
Kumbuka hasira ni kichocheo cha kufanya mabaya.
 
Ulitaka wakampigie goti?Mimi nikidaiwa na mwenye nyumba huku mtaani naona tabu yake.yeye naye alipe.KUPATWA KWA MBOWE tareh1-9-2016
Angalia andiko langu juu, kwamba wako wengi wanadaiwa; kwa nini yeye tu na sio wawili? Ni kweli wasingeweza kufanya na kwa mwingine jana? Linganisha na jana ilikuwa iwe nini kwa Mbowe,
 
Kudaiwa mtu sio kosa na kulipa ni uungwana. Lakini ukiangalia kwandani suala hili lina mkono wa siasa.

Wadaiwa wakubwa tunaambiwa ni wengi. Kwa nini waanze na huyu moja na si wawili? Kwa nini waanze tar 1 Sept?

Mbowe alipe lakini kuna mkono wa mtu ktk kulishughulikia zaidi ya NHC.
swala la mkono wa siasa lina misingi ya hisia, la misingi ni kujua je? kuna uhalali kisheria kufanya hivyo? that is my concern! na tukumbuke kuwa, " before you preach about righteousness, clean first your hands"
 
NI RAHISI CCM KUKWEPA KULIPA KODI NA KUFANYA BIASHARA KIUJANJA UJANJA KULIKO CHADEMA KUFANYA HIVYO. Msiniulize kwann mtaonekana hamnazo kichwani nanyinyi!!!
 
Ni utamaduni usiopendeza na unaozidi kujikita baina ya jamii yetu juu ya kutotenganisha sasa vyama vya siasa na mambo mengine.

Kwa jamii zilizostaarabika, mwanachama wa chama fulani cha siasa anaweza kufanya biashara na mtu wa chama kingine.

Ifahamike pia kuwa kiongozi wa chama fulani sio dhambi kufanya biashara ilimradi asichanganye siasa na biashara.

Kwa sasa kuna Suala la Mbowe hotels ltd na NHC kuhusu kudaiana na sakata la kuondoshwa kwenye pango hilo.

Mimi nadhani kampuni hiyo iliingia mkataba na NHC ambao unalindwa kisheria na sio kisiasa. Jambo la kushangaza, swala hili limeibua makundi mawili ambayo ukiyatizama yanaendeshwa na mihemuko na ushabiki wa kisiasa.

kuna wanaoipongeza NHC kwa kuiondosha kampuni hiyo kwenye pango na wengine wanaponda hatua hiyo, wote ukisoma ama kusikiliza hoja ama kelele zao ni mihemuko na ushabiki wa vyama vyao vya siasa.

Mimi nadhani Mbowe kama mtanzania mwingine anahaki ya kufanya biashara, Na NHC kama shirika la umma Lina haki ya kufanya biashara kwa mujibu wa sheria.

Tuwaache NHC na Mbowe hotels limited wamalize swala lao kwa mujibu wa mkataba wao na siyo porojo zetu za siasa uchwara.

Mbowe hotels ltd msitumie wanavyama vya siasa kupotosha ukweli ama kupata huruma maana biashara hiyo haiwahusu. Vilevile NHC tekelezeni shughuli zenu bila kushinikizwa na itikadi yoyote bali sheria kwa kuwa sheria ni msumeno.

Aidha nishauri tu kuwa kwa wanasiasa wafanyabiashara itapendeza kuona wanakuwa mstari wa mbele kulipa kodi maana ndiyo kipimo cha uzalendo kwa taifa. Kwa nchi nyingine kukwepa Kodi ni disqualification namba moja katika siasa.

Tuache kuchanganya siasa za vyama na mambo ya biashara.
Mkuu umenena,kuna tofauti kubwa kati ya Mbowe and Mbowe Hotel katika jicho la sheria za makampuni "a company under the law is legal person",therefore Freeman Mbowe and Mbowe Hotel Ltd are two different persons when it comes to Business issues.Hapo hadaiwi Mbowe wa CHADEMA anayedaiwa ni Mbowe Hotel anayefanya Biashara na NHC.Wanasheria mtanisahihisha.Ila Mbowe akipatikana na kosa la kukwepa kodi ya serikali na mengineyo hapo waliopo nyuma ya Mbowe Hotel Ltd ndiyo wanatafutwa kujibu mashtaka.Sasa hapa naona ni madai ya pango.Mbona serikali inadaiwa hawatoi samani zake nje?.Nimesema aya kwasababu nimewahi kufanya field NHC,katika computation ya Tenants Debts kuna wanasiasa wengi sana walikuwa wanadaiwa.Naomaba niishie hapa,nisijekuitwa mchochezi.
 
Mwambie Mbowe aende mahakamani

Wewe bado umelala. Kesi ipo mahakamani kitambo. Ndio maana inashangaza kuona NHC wakikomalia kutoa vitu nje. Hapo ni mkono wa siasa kutoka korido kuu ndio umeingilia; na kutetea mshahara mnono wa bwana Nehemia.
 
Hivi inaingia akilini kesi ipo mahakamani shirika kama lile litoe vyombo?
Yumkini mbowe alikuwa anatumia mahakama kama kichaka cha kukwepa kodi
Bado deni la Ppf,itachukuliwa ile hoteli yake kule Machame
 
Mkurugenzi wa NHC anajaribu kujipendekeza kwa mkuu wa nchi kwa kumtimua Mbowe.Lets wait and see.
 
Hivi inaingia akilini kesi ipo mahakamani shirika kama lile litoe vyombo?
Yumkini mbowe alikuwa anatumia mahakama kama kichaka cha kukwepa kodi
Bado deni la Ppf,itachukuliwa ile hoteli yake kule Machame

Ndiyo kesi ipo mahakamani. Hii siyo siri.
 
Ili suala lilianza Feb 2015 tatizo mbowe alilichukulia kisiasa

Na ni muda mrefu sana kumbe toka mwaka jana!!? Hapo ni sawa hatua zichukuliwe, lakini suala linakuja nini kilifanya NHC wasubiri muda wote mpaka sasa deni liwe kubwa hivyo? Pili, ni yeye pekee anayedaiwa na NHC? Huoni kwa timing hii hata kama ni kweli huwezi kuliepusha na siasa? Tuwe wakweli vinginevyo dhamira ya serekali itabaki na taswira ya kufanya kazi kwa chuki na fitina dhidi ya wale wanaoikosoa. Na kama sio siasa ngoja tuone kama litakuwa zoezi endelevu, na tunajua wengi wa wanaodaiwa katika nyumba hizo wengi wao wakiwa wanachama wa chama tawala lakini zoezi hili halitowagusa kwani dhamira sio uzalendo bali utashi wa kisiasa.

CC: Buberwa D
 
Nimesema suala liko mahakamani siwezi kuingilia sana lkn nakumbuka mwaka 2004 suala hili liliandikwa kwenye gazeti la Rai baadae ikaenda ikapoa ni mgogoro wa muda mrefu kati ya mbowe hotel na nhc na lilikuwa mahakamani kesi mpk mwaka jana
 
Back
Top Bottom