BUBERWA D.
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 2,293
- 1,170
Ni utamaduni usiopendeza na unaozidi kujikita baina ya jamii yetu juu ya kutotenganisha sasa vyama vya siasa na mambo mengine.
Kwa jamii zilizostaarabika, mwanachama wa chama fulani cha siasa anaweza kufanya biashara na mtu wa chama kingine.
Ifahamike pia kuwa kiongozi wa chama fulani sio dhambi kufanya biashara ilimradi asichanganye siasa na biashara.
Kwa sasa kuna Suala la Mbowe hotels ltd na NHC kuhusu kudaiana na sakata la kuondoshwa kwenye pango hilo.
Mimi nadhani kampuni hiyo iliingia mkataba na NHC ambao unalindwa kisheria na sio kisiasa. Jambo la kushangaza, swala hili limeibua makundi mawili ambayo ukiyatizama yanaendeshwa na mihemuko na ushabiki wa kisiasa.
kuna wanaoipongeza NHC kwa kuiondosha kampuni hiyo kwenye pango na wengine wanaponda hatua hiyo, wote ukisoma ama kusikiliza hoja ama kelele zao ni mihemuko na ushabiki wa vyama vyao vya siasa.
Mimi nadhani Mbowe kama mtanzania mwingine anahaki ya kufanya biashara, Na NHC kama shirika la umma Lina haki ya kufanya biashara kwa mujibu wa sheria.
Tuwaache NHC na Mbowe hotels limited wamalize swala lao kwa mujibu wa mkataba wao na siyo porojo zetu za siasa uchwara.
Mbowe hotels ltd msitumie wanavyama vya siasa kupotosha ukweli ama kupata huruma maana biashara hiyo haiwahusu. Vilevile NHC tekelezeni shughuli zenu bila kushinikizwa na itikadi yoyote bali sheria kwa kuwa sheria ni msumeno.
Aidha nishauri tu kuwa kwa wanasiasa wafanyabiashara itapendeza kuona wanakuwa mstari wa mbele kulipa kodi maana ndiyo kipimo cha uzalendo kwa taifa. Kwa nchi nyingine kukwepa Kodi ni disqualification namba moja katika siasa.
Tuache kuchanganya siasa za vyama na mambo ya biashara.