Nionavyo kuhusu sakata la Mbowe na NHC

Nionavyo kuhusu sakata la Mbowe na NHC

Kukwepa kodi ni kuhujumu uchumi, wapelekwe mahakamani.

Haiwezekani wahubiri mabadiliko kumbe wao ndio wa kwanza kuwaibia wananchi.

Chama la hovyo sijawahi kuona, wanayohubiri ni kinyume na wafanyayo.

Watanzania wenye akili timamu hawana hamu na machadema.
Hivi unajua maana ya kukwepa kodi? Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana.
 
Nimesema suala liko mahakamani siwezi kuingilia sana lkn nakumbuka mwaka 2004 suala hili liliandikwa kwenye gazeti la Rai baadae ikaenda ikapoa ni mgogoro wa muda mrefu kati ya mbowe hotel na nhc na lilikuwa mahakamani kesi mpk mwaka jana

Na mara zote suala hilo limekuwa likiibuliwa wakati wa joto la kisiasa. Hivyo hakuna namna yoyote ile tutashindwa kulihusisha na fitina za kisiasa. Ikibidi Mbowe anyang'anywe hilo jengo kwani inaonekana hawezi kulilipia ili roho zenu zisuuzike, lakini ukweli uko wazi kwamba siasa za chuki, visasi na fitina ndio zilizo nyuma ya suala hili na wala sio uzalendo. Vinginevyo tuone hatua zikichuliwa kwa wadaiwa wote na sio kwa faida ya utawala wenu ama Mbowe iwapo mtafanikiwa kumtisha kwa kosa hili la kutokulipa kodi. Kwani iwapo mtafanikiwa kumnyamazisha haitokuwa afya kwake yeye na chama chake kwani ndio itakuwa fimbo yenu ya kumuangamiza na upinzani kwa ujumla. Tunataka sheria ichukue mkondo wake kwani ndio itakuwa faida kwa hiyo cdm yake na taifa kwa ujumla.
 
Sheria itafata mkondo wake ukweli utajulikana kama ni shinikizo la kisiasa au [HASHTAG]#hapakazi[/HASHTAG] tu haina urafiki round hiii
 
Tatizo ni kama anadaiwa kwa nini atupiwe nje virago siku iliyokuwa iwe ya maandamano ya CDM. Wangekuwa wajanja wangesubiri Siku ingine. Lalini mbona wanaodaiwa ni wengi, hata idara za serikali. Kwa mini mbowe tu na kwa nini siku hiyo?
 
Wajibu wa kulipa kodi ni kwa kila raia, hii ni kutokana na sheria tulizojiwekea hapa nchini. Hivyo kama swala ni kulipa kodi ambayo inastahili sioni kama kuna chuki au niambaya kumwambia mtu atimize wajibu wake kisheria?

Nimeuliza kama amelipa tunaichuliaje au tuichukuliaje serikali pamoja na NHC?Maana amedai amelipa na hana deni!Kuna wakati TRA walisema halipi kodi later wakasema walikosea.Najiuliza wakiprove hawana deni tuwafanyeje mnaoshabikia hili?
 
Halafu mtu anasema mniombee, na hao viongozi wa dini wanakusanyika eti wanafanya sala! haya makanisa na misikiti vitakosa waumini pindi watu watakapojitambua ingawa bado sana- (Kule Mbeya mtu anaishukuru serikali kwa kepeleka kupatwa kwa jua Mbeya na mwaka kesho ifanye hivyo)
Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya viongozi wa dini na wafanyakazi wa dini. Wengi wa hawa tunaowaita viongozi wa dini ni wafanya kazi tu hawana zile karama za kidini zaidi ya mavazi ya kidini yanayowatambulisha kwa mujibu wa vyeo vyao katika ajira yao ya dini. Ndio maana utakuta wachache sana wanasimamia kweli wengi wako kimaslahi. Kwa lugha ya sasa kama anavyosema huyo ambaye mara nyingi anaomba kuombewa tungesema ni wapiga dili tu
 
Kudaiwa mtu sio kosa na kulipa ni uungwana. Lakini ukiangalia kwandani suala hili lina mkono wa siasa.

Wadaiwa wakubwa tunaambiwa ni wengi. Kwa nini waanze na huyu moja na si wawili? Kwa nini waanze tar 1 Sept?

Mbowe alipe lakini kuna mkono wa mtu ktk kulishughulikia zaidi ya NHC.
Na mimi timing ya hili jambo linanipa ukakasi kwa kweli
 
Mkuu umenena,kuna tofauti kubwa kati ya Mbowe and Mbowe Hotel katika jicho la sheria za makampuni "a company under the law is legal person",therefore Freeman Mbowe and Mbowe Hotel Ltd are two different persons when it comes to Business issues.Hapo hadaiwi Mbowe wa CHADEMA anayedaiwa ni Mbowe Hotel anayefanya Biashara na NHC.Wanasheria mtanisahihisha.Ila Mbowe akipatikana na kosa la kukwepa kodi ya serikali na mengineyo hapo waliopo nyuma ya Mbowe Hotel Ltd ndiyo wanatafutwa kujibu mashtaka.Sasa hapa naona ni madai ya pango.Mbona serikali inadaiwa hawatoi samani zake nje?.Nimesema aya kwasababu nimewahi kufanya field NHC,katika computation ya Tenants Debts kuna wanasiasa wengi sana walikuwa wanadaiwa.Naomaba niishie hapa,nisijekuitwa mchochezi.

Mimi mwenyewe naidai serikali tangu mwaka 2010, sijui nikatoe meza na makabati ya ikulu nje??
 
Ni utamaduni usiopendeza na unaozidi kujikita baina ya jamii yetu juu ya kutotenganisha sasa vyama vya siasa na mambo mengine.

Kwa jamii zilizostaarabika, mwanachama wa chama fulani cha siasa anaweza kufanya biashara na mtu wa chama kingine.

Ifahamike pia kuwa kiongozi wa chama fulani sio dhambi kufanya biashara ilimradi asichanganye siasa na biashara.

Kwa sasa kuna Suala la Mbowe hotels ltd na NHC kuhusu kudaiana na sakata la kuondoshwa kwenye pango hilo.

Mimi nadhani kampuni hiyo iliingia mkataba na NHC ambao unalindwa kisheria na sio kisiasa. Jambo la kushangaza, swala hili limeibua makundi mawili ambayo ukiyatizama yanaendeshwa na mihemuko na ushabiki wa kisiasa.

kuna wanaoipongeza NHC kwa kuiondosha kampuni hiyo kwenye pango na wengine wanaponda hatua hiyo, wote ukisoma ama kusikiliza hoja ama kelele zao ni mihemuko na ushabiki wa vyama vyao vya siasa.

Mimi nadhani Mbowe kama mtanzania mwingine anahaki ya kufanya biashara, Na NHC kama shirika la umma Lina haki ya kufanya biashara kwa mujibu wa sheria.

Tuwaache NHC na Mbowe hotels limited wamalize swala lao kwa mujibu wa mkataba wao na siyo porojo zetu za siasa uchwara.

Mbowe hotels ltd msitumie wanavyama vya siasa kupotosha ukweli ama kupata huruma maana biashara hiyo haiwahusu. Vilevile NHC tekelezeni shughuli zenu bila kushinikizwa na itikadi yoyote bali sheria kwa kuwa sheria ni msumeno.

Aidha nishauri tu kuwa kwa wanasiasa wafanyabiashara itapendeza kuona wanakuwa mstari wa mbele kulipa kodi maana ndiyo kipimo cha uzalendo kwa taifa. Kwa nchi nyingine kukwepa Kodi ni disqualification namba moja katika siasa.

Tuache kuchanganya siasa za vyama na mambo ya biashara.
Walivyodaiwa Sabodo na Mkono mlinyamaza kimya.....sasa mnalialia tu.
 
Amelipa na kama anasema amelipa basi NHC wangekuja na proof kwamba anadaiwa.Kwanini waseme tena kesi iko mahakamani?
Wasingemtoa bana, kwani wao hawaogopi kulalamikiwa? Mbowe alipe tu bana, asizidi kujiaibisha.
 
Hivi anadaiwa kodi ama anadaiwa pango (rent)?

Ukifuatilia utata wa deni linalozungumzwa hapo ni kiasi kilicholipwa na kinachodaiwa ni gharama za matengenezo mbali mbali yaliyofanyika kwa mujibu wa mkataba. mwingine anasema kiasi kilichotumika kufanya matengenezzo ni kikubwa ukilinganisha matengenezo yaliyofanyika mwingine anasema kiasi kilichotumika ni sahihi na ndio maana hatudaiani. Kwa muktadha huo court rulling ndio inaweza kumaliza mgogoro huo na sio kutupiana vitu nje etc

tusubiri
 
Nilikuwa sijaelewa kumbe ni kampuni inaitwa Mbowe Hotels Limited? Kama ni hivyo basi tunamuonea Mbowe maana kisheria kampuni na mmiliki wake ni watu wawili tofauti sheria ya makampuni kifungu cha 15 kinasema kampuni ikishaundwa inakuwa mtu kisheria anayejitegemea tofauti na mmiliki wake. Sasa kama MHL ni kampuni hatuwezi kumlaumu Mbowe kwani kampuni ina menejimenti yake, ina wakurugenzi wanaofanya maamuzi kwa ajili yake ambao mbowe siyo sehemu yake kwa vyovyote vile huo mkataba NHC waliingia na MHL si mbowe.
 
Naam ni kwa kila raia lakini baba J.esca pamoja na mshahara wake wa milioni 403 kwa mwaka halipi kodi, huu ni ufisadi mkubwa sana. Kumbuka April 2016 aliahidi akitoka Chato kwenye mapumziko ataweka wazi Salary slip yake hadharani kuonyesha mshahara wake kwa mwezi ni milioni 9.5, lakini hadi hii leo ameshindwa kufanya hivyo baada ya kugundua mshahara wake ni mkubwa zaidi na hakatwi kodi.

Wajibu wa kulipa kodi ni kwa kila raia, hii ni kutokana na sheria tulizojiwekea hapa nchini. Hivyo kama swala ni kulipa kodi ambayo inastahili sioni kama kuna chuki au niambaya kumwambia mtu atimize wajibu wake kisheria?
 
Na mara zote suala hilo limekuwa likiibuliwa wakati wa joto la kisiasa. Hivyo hakuna namna yoyote ile tutashindwa kulihusisha na fitina za kisiasa. Ikibidi Mbowe anyang'anywe hilo jengo kwani inaonekana hawezi kulilipia ili roho zenu zisuuzike, lakini ukweli uko wazi kwamba siasa za chuki, visasi na fitina ndio zilizo nyuma ya suala hili na wala sio uzalendo. Vinginevyo tuone hatua zikichuliwa kwa wadaiwa wote na sio kwa faida ya utawala wenu ama Mbowe iwapo mtafanikiwa kumtisha kwa kosa hili la kutokulipa kodi. Kwani iwapo mtafanikiwa kumnyamazisha haitokuwa afya kwake yeye na chama chake kwani ndio itakuwa fimbo yenu ya kumuangamiza na upinzani kwa ujumla. Tunataka sheria ichukue mkondo wake kwani ndio itakuwa faida kwa hiyo cdm yake na taifa kwa ujumla.
Ndiyo maana nikasema wahalifu wote wako cdm na hasa majambazi wamekingiwa kifua kwa kugeuzwa kuwa walinzi wa viongozi wakiguswa wanakimbilia siasa km mbowe anakimbilia siasa kwa masuala yake binafsi
 
Wajibu wa kulipa kodi ni kwa kila raia, hii ni kutokana na sheria tulizojiwekea hapa nchini. Hivyo kama swala ni kulipa kodi ambayo inastahili sioni kama kuna chuki au niambaya kumwambia mtu atimize wajibu wake kisheria?
kunakitu sijakielewa hapa mbowe anadaiwa kodi au anadaiwa pango na nhc tuwekeni sawa hapa
 
Back
Top Bottom