Ninunue desktop computer yenye specifications gani ili baadae ni upgrade mwenyewe?

Kama budget sio shida Angalia Mac mini ambayo ni around $700, hii ndio rahisi huku ikiwa na top specs, sababu pia ni kadogo ni rahisi kuagizishia online bila kuchajiwa gharama nyingi.

Amazon product ASIN B08N5PHB83
Siku 2 zilizopita ilikuwa kwenye offer kwa $600, hivyo unaweza subiria offer kama hizi ili unachosave kikusaidie kwenye usafiri na kodi. Uzito wake ni 1.8kg hivyo kinasafirishika na hawa kina DHL na FedEx. Pamoja na kodi pengine around milioni 2 itaku cost.

Kama unaenda upande wa used Intel generation ya 2 mpaka ya 7 ndio tunazojidai nazo mtaani maana bei zake ndio rafiki kwa maisha yetu. Hivyo tuki convert kwa Mac Ina maana angalau iwe Mac ya 2011 kupanda,

Kuwa makini sana na Mac za core 2 duo zimejaa kibao mtaani ni bora ukanunue Samsung simu mtumba kuliko hizi, dual core 2021 haitakusaidia kwenye ku edit video.

Kujua specs za imac kirahisi Wana andika nyuma model we Igoogle.
Mkuu Chief Mkwawa ahsante sana kwa muda wako na ushauri.
 
Natumae mleta mada umepata muongozo...
Bila shaka mkuu nimepata mwongozo wa kutosha na niwashukuru wana JF bila kujali umri, rangi, cheo, ujuzi, uzoefu pamoja na dini. Nilikuwa nipo njia panda kwa kipindi sasa, lakini kwasasa nategemea kuwa na mashine yenye akili kubwa kuchakata data. Na hii ni kutokana na uhitaji wangu na bajeti finyu.

Mwisho wa mwezi huu nitaingia Dar hapo kuzunguka machimbo ambayo nimeelekezwa pamoja na kuwasiliana na baadhi ya wadau ili kufanikisha ununuzi wa hivyo vitendea kazi.

Ninaamini uwepo wenu hapa JF si bure na muendele na moyo wa Kujitoa kwani wengine bado baadhi ya mambo tuomba ufafanuzi kwenu ninyi qenye upeo kwa kiasi chake.
 
Kwa haraka haraka nunua pentium gen ya 4 kwa around 180k ama kama Una HDD around 130k, then nunua i7 4790 kwa 80k utapata machine ya i7 kwa chini ya laki 3, budget inayobakia upgrade ram, 8gb minimum.

Then Vuta pumzia Kisha upgrade ssd na Gpu.

Computer pentium gen ya 4 nilipata duka linaitwa kaale mtaa wa likoma kkoo linaangalizana na KkkT kkoo.

Cpu ya i7 kuna jamaa anaitwa Andrea anazo mkombozi bank hapo hapo likoma na Agrrey, jengo linaangalizana na bank ukiingia ndani duka LA kona.

Hio ni budget option.

Option nyengine ya uhakika future proof ila unahitaji kujipinda ni kwenda straight gen ya 8, (gen ya 7, 6, 5, 4, 3 na 2 ni kama zinafanana) hapa utafute pentium ama i3 ama celeron ya gen ya 8, ila itabidi uhangaike sana, naziona sometime hadi laki 5, I hope zitakuwepo za bei ya chini zaidi.

Kuna option nyengine sema hii ni kama Una kwenda all out kwenye video editing na una sacrifice mambo mengine kama gaming, Autocad na mambo mengine ya single thread perfomance.

Kuna machine za xenon zenye dual cpu unaweka cpu mbili kwenye motherboard moja, cpu moja inakuwa na core 6 na thread 12, hivyo unapata core 12 na thread 24, hizi ni zaidi ya i7 yoyote chini ya gen ya 8, ila zinakula umeme balaa.

Huyu mdau kuna kipindi alikuwa nazo
MTOTO WA KUKU

Zipo pia maduka mengi ya madesktop, sema hizi si future proof Sababu ni gen za kizamani.
Habari ndugu #chief mkwawa kwa mchango wako.

MREJESHO

Nilifanikiwa kununua Desktop yenye specs hizi hapa:

INTEL PENTIUM DUAL CORE E5700 3.0 GHZ, RAM 2GB, 320HDD BRAND HP.
WAT 65.

Naomba #CHIEF MKWAWA uniambie je kwa ushauri wako nitaweza kuiup grade hiyo mashine??? Na je ni generation ya ngapi? Mana nimeyumba sana kariakoo na duka ulilonitajia niliambiwa hawana kwa sasa. Niliipatia duka moja mtaa wa msimbazi B kariakoo kwa bei ya 160k.

Bado sijaijua gen ya ngapi na nikii upgrade nifanyaje. Karibuni wadau. Asanteni kwa michango yenu.
 
Dah mkuu hii wame kupiga, huwezi kuirudisha? Hii ni Pentium ya zamani sana, una upgrade kwenda core 2 duo.

Kaale mbona nilikwenda karibuni zipo machine bado?

Pia naona kupatana/zoom Tanzania pentium za 6th gen za kutosha around 180,000.
 
Aiseee kumbee. Kaale nimefika nimeeuliza wanasema hawana tena. Anyway basi tena nipo mkoani ngoja niitumie kwa kazi nyepesi tu nitafanya mpango tena. Ila kaale nilifika boss.

Kaz bado ninayo Kumbe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom