Ninunue desktop computer yenye specifications gani ili baadae ni upgrade mwenyewe?

Alex Gk

Senior Member
Sep 4, 2016
107
225
Salamu sana kwenu JF experts na sisi wengine ma newbies.

Najichanga bajeti alau niwe na around 350k hivi. Kwa sasa imebakia kidogo tu ili itimie hiyo bajeti.

UHITAJI ni kwamba napenda kujifunza graphics hususani video editing na design mbalimbali kwa kutumia programs za Photoshop, illustrator, InDesign, premier na maxon 4d mayor. Programs hizi zinahitaji mashine nzuri ili ziweze kufanya kazi vzuri. Sasa natarajia ninunue mashine ya kawaida ya kawaida computer tupu bila monitor, ila iweze kuwa na options za ku UPGRADE siku za mbeleni.

Je kwa bajeti ya around 350k hapo kariakoo nikachague mashine gani? Kwa maana brand name na yenye SPECIFICATIONS gani? Kwa manaa huko mbeleni ni UPGRADE mwenyewe.

NB. Nina basics za Photoshop na illustrator japo nilikuwa na laptop yenye uwezo mdogo nilikomaa nayo mwisho ikaja kufa kabisa mwezi wa kwanza, mwakain huu.

Karibuni kwa ushauri
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,413
2,000
Mkuu hiyo ni Bei ya CPU tuu. Bado sana hapo.

BTW tafuta mother board ambayo haina Ram wala CPU unaweza pata kwa bei hiyo, baadae uanze kutafuta Enclosure, Power Supply na Vitu vingine
 
Alex Gk

Senior Member
Sep 4, 2016
107
225
Aaaah sawasawa mkuu. Asante kwa kunifungua macho. Na je motherbody nitaipata hapa bongo karikooo au wapi? Na nitatambuaje uwezo wa hiyo mother body mkuu?

Lengo niunde mashine hatari sana alau processor iwe kuanzia intel i5+, 3.4Ghz na Ram Gb 16, kuhusu storage nitasonga nayo. Mdohow mdo ila tu iwe optimized na software kubwa mkuu. Nifungue macho bajeti naunga unga mdomdo sina haraka, kama kuna uwezekano wa hiyo mother body nijue wapu zipo
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Kwa haraka haraka nunua pentium gen ya 4 kwa around 180k ama kama Una HDD around 130k, then nunua i7 4790 kwa 80k utapata machine ya i7 kwa chini ya laki 3, budget inayobakia upgrade ram, 8gb minimum.

Then Vuta pumzia Kisha upgrade ssd na Gpu.

Computer pentium gen ya 4 nilipata duka linaitwa kaale mtaa wa likoma kkoo linaangalizana na KkkT kkoo.

Cpu ya i7 kuna jamaa anaitwa Andrea anazo mkombozi bank hapo hapo likoma na Agrrey, jengo linaangalizana na bank ukiingia ndani duka LA kona.

Hio ni budget option.

Option nyengine ya uhakika future proof ila unahitaji kujipinda ni kwenda straight gen ya 8, (gen ya 7, 6, 5, 4, 3 na 2 ni kama zinafanana) hapa utafute pentium ama i3 ama celeron ya gen ya 8, ila itabidi uhangaike sana, naziona sometime hadi laki 5, I hope zitakuwepo za bei ya chini zaidi.

Kuna option nyengine sema hii ni kama Una kwenda all out kwenye video editing na una sacrifice mambo mengine kama gaming, Autocad na mambo mengine ya single thread perfomance.

Kuna machine za xenon zenye dual cpu unaweka cpu mbili kwenye motherboard moja, cpu moja inakuwa na core 6 na thread 12, hivyo unapata core 12 na thread 24, hizi ni zaidi ya i7 yoyote chini ya gen ya 8, ila zinakula umeme balaa.

Huyu mdau kuna kipindi alikuwa nazo
MTOTO WA KUKU

Zipo pia maduka mengi ya madesktop, sema hizi si future proof Sababu ni gen za kizamani.
 
Nianze kwa kusema kwamba, umetoa muongozo uliotukuka sana sana. Mimi nikushukuru na naamini wengine wamepata ABC... kuhusu namna gani unaweza kumiliki machine alau kwa bajeti ya kuunga unga. Mana pesa ya pamoja ya kuchomoa DESKTOP computer yenye SPECIFICATIONS za kutosha ni mziki ukizingatia kuna mahitaji mengine ya kimaisha.

Nitakomaa ndugu yangu nizame kariakoo. Nianze safari ya maisha ya graphics. Na mrejesho nitauleta hapa. Shukrani sana mkuu. Endelea kuwa na moyo huo aisee.
 
Walec

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
770
1,000
Kwa haraka haraka nunua pentium gen ya 4 kwa around 180k ama kama Una HDD around 130k, then nunua i7 4790 kwa 80k utapata machine ya i7 kwa chini ya laki 3, budget inayobakia upgrade ram, 8gb minimum.

Then Vuta pumzia Kisha upgrade ssd na Gpu.

Computer pentium gen ya 4 nilipata duka linaitwa kaale mtaa wa likoma kkoo linaangalizana na KkkT kkoo.

Cpu ya i7 kuna jamaa anaitwa Andrea anazo mkombozi bank hapo hapo likoma na Agrrey, jengo linaangalizana na bank ukiingia ndani duka LA kona.

Hio ni budget option.

Option nyengine ya uhakika future proof ila unahitaji kujipinda ni kwenda straight gen ya 8, (gen ya 7, 6, 5, 4, 3 na 2 ni kama zinafanana) hapa utafute pentium ama i3 ama celeron ya gen ya 8, ila itabidi uhangaike sana, naziona sometime hadi laki 5, I hope zitakuwepo za bei ya chini zaidi.

Kuna option nyengine sema hii ni kama Una kwenda all out kwenye video editing na una sacrifice mambo mengine kama gaming, Autocad na mambo mengine ya single thread perfomance.

Kuna machine za xenon zenye dual cpu unaweka cpu mbili kwenye motherboard moja, cpu moja inakuwa na core 6 na thread 12, hivyo unapata core 12 na thread 24, hizi ni zaidi ya i7 yoyote chini ya gen ya 8, ila zinakula umeme balaa.

Huyu mdau kuna kipindi alikuwa nazo
MTOTO WA KUKU

Zipo pia maduka mengi ya madesktop, sema hizi si future proof Sababu ni gen za kizamani.
Hivi naweza upgrade lets say i3 gen 4 kwenda i7 gen kuanzia 4 kwenda juu? Vp zile min cpu ziko upgradable?
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Hivi naweza upgrade lets say i3 gen 4 kwenda i7 gen kuanzia 4 kwenda juu? Vp zile min cpu ziko upgradable?
Gen ya 4 mwenzake ni ya 5 zinaingiliana, in theory machine yenye i3 gen ya 4 inaweza kuingia i7 gen ya 5, sema kiuhalisia gen ya 5 zilitoka chache sana ngumu kukuta machine zake mtaani.

Hivyo unaweza upgrade i3 gen ya 4 kwenda i7 gen ya 4 kirahisi.

Mini pc zipo ambazo unaweza ku upgrade na zipo ambazo huwezi, si kila i3 ni sawa, hizi zinazo kuja na desktop cpu kama i3 4130 unaweza uka upgrade kwenda i7, ila kuna mini pc zinakuja na low power cpu ama cpu za laptop kabisa hizi hutaweza ku upgrade.
 
Nashukuru mkuu...mana kuna mwanangu mtaani anapenda games...kwa sasa ana 500 cash...ila nilimwambia atafute setup ya desktop mana laptop itakua gharama sana..

So kwa ushauri wako kwa hyo 500 aanze kusaka cpu aina gan
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Nashukuru mkuu...mana kuna mwanangu mtaani anapenda games...kwa sasa ana 500 cash...ila nilimwambia atafute setup ya desktop mana laptop itakua gharama sana..

So kwa ushauri wako kwa hyo 500 aanze kusaka cpu aina gan
Ushauri wa juu unamfaa pia, kama Anaaandaa mdogo mdogo aende moja kwa moja gen ya 8, hela hio atapata desktop tu,

Kama anataka kitu kamili acheze sasa hivi aende gen ya 4 atapata desktop na change itakayobakia atapata gpu low-end kama Gt 1030, gtx 750ti ama rx 550.
 
Walec

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
770
1,000
Ushauri wa juu unamfaa pia, kama Anaaandaa mdogo mdogo aende moja kwa moja gen ya 8, hela hio atapata desktop tu,

Kama anataka kitu kamili acheze sasa hivi aende gen ya 4 atapata desktop na change itakayobakia atapata gpu low-end kama Gt 1030, gtx 750ti ama rx 550.
Nimekupata mkuu... shukran

Sasa naomba nisaidie kitu kimoja..ukipata muda hebu pitia hii page ya hawa jamaa..naona wana cpu za bei nzuri sana huku specs zikiwa nzuri...kama kuna yoyote unaweza recommend kweny hii page naomba uniambie...post za cpu ni recently tu wala huendi mbali

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Nimekupata mkuu... shukran

Sasa naomba nisaidie kitu kimoja..ukipata muda hebu pitia hii page ya hawa jamaa..naona wana cpu za bei nzuri sana huku specs zikiwa nzuri...kama kuna yoyote unaweza recommend kweny hii page naomba uniambie...post za cpu ni recently tu wala huendi mbali

Computer ni nzuri kweli Mkuu, Sema Kuna jambo moja muhimu nalo ni power supply, sijawahi ku deal na desktop za Epson ama NEC sifahamu kama wanatumia proprietary ama power supply za kawaida.

Kama unapata wasaa nenda wakuoneshe power supply za hizo machine kama ni za kawaida kwa hio bei ni nzuri sana, naona hadi 6th Gen i5 6500 kwa 350k,

Kama ni hizi za pin kidogo vyema ipige picha ama wakwambie ni watts ngapi ili ujue limits zako za ku upgrade kwa baadae.
 
Shukran mkuu..wacha niwasiliane na jamaa yangu mmoja yupo karbu na offis za hao jamaa...akifanikiwa piga picha nitaweka hapa..
 
BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
1,659
2,000
Computer ni nzuri kweli Mkuu, Sema Kuna jambo moja muhimu nalo ni power supply, sijawahi ku deal na desktop za Epson ama NEC sifahamu kama wanatumia proprietary ama power supply za kawaida.

Kama unapata wasaa nenda wakuoneshe power supply za hizo machine kama ni za kawaida kwa hio bei ni nzuri sana, naona hadi 6th Gen i5 6500 kwa 350k,

Kama ni hizi za pin kidogo vyema ipige picha ama wakwambie ni watts ngapi ili ujue limits zako za ku upgrade kwa baadae.
Mkuu salam..naomba ushauri nahitaji desktop computer hasa imac au kama utashauri vinginevyo kwa ajili ya video editing na graphics..ushauri wa specs na wapi kwa kuzipata na bei elekezi.
Natanguliza shukrani.
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Mkuu salam..naomba ushauri nahitaji desktop computer hasa imac au kama utashauri vinginevyo kwa ajili ya video editing na graphics..ushauri wa specs na wapi kwa kuzipata na bei elekezi.
Natanguliza shukrani.
IMac kama huna Budget nzuri achana nayo, kama shida ni osx tumia Hackintosh.

Ushauri Angalia comment yangu ya kwanza jamaa pia a nataka machine ya video.
 
BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
1,659
2,000
IMac kama huna Budget nzuri achana nayo, kama shida ni osx tumia Hackintosh.

Ushauri Angalia comment yangu ya kwanza jamaa pia a nataka machine ya video.
Nashukuru Mkuu..budget sio shida..vitu vya kuungaunga wakati mwingine sio vizuri...sihitaji mpya nafahamu zipo used.
 
Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
25,471
2,000
Nashukuru Mkuu..budget sio shida..vitu vya kuungaunga wakati mwingine sio vizuri...sihitaji mpya nafahamu zipo used.
Kama budget sio shida Angalia Mac mini ambayo ni around $700, hii ndio rahisi huku ikiwa na top specs, sababu pia ni kadogo ni rahisi kuagizishia online bila kuchajiwa gharama nyingi.

Siku 2 zilizopita ilikuwa kwenye offer kwa $600, hivyo unaweza subiria offer kama hizi ili unachosave kikusaidie kwenye usafiri na kodi. Uzito wake ni 1.8kg hivyo kinasafirishika na hawa kina DHL na FedEx. Pamoja na kodi pengine around milioni 2 itaku cost.

Kama unaenda upande wa used Intel generation ya 2 mpaka ya 7 ndio tunazojidai nazo mtaani maana bei zake ndio rafiki kwa maisha yetu. Hivyo tuki convert kwa Mac Ina maana angalau iwe Mac ya 2011 kupanda,

Kuwa makini sana na Mac za core 2 duo zimejaa kibao mtaani ni bora ukanunue Samsung simu mtumba kuliko hizi, dual core 2021 haitakusaidia kwenye ku edit video.

Kujua specs za imac kirahisi Wana andika nyuma model we Igoogle.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,925
2,000
Kwa haraka haraka nunua pentium gen ya 4 kwa around 180k ama kama Una HDD around 130k, then nunua i7 4790 kwa 80k utapata machine ya i7 kwa chini ya laki 3, budget inayobakia upgrade ram, 8gb minimum.

Then Vuta pumzia Kisha upgrade ssd na Gpu.

Computer pentium gen ya 4 nilipata duka linaitwa kaale mtaa wa likoma kkoo linaangalizana na KkkT kkoo.

Cpu ya i7 kuna jamaa anaitwa Andrea anazo mkombozi bank hapo hapo likoma na Agrrey, jengo linaangalizana na bank ukiingia ndani duka LA kona.

Hio ni budget option.

Option nyengine ya uhakika future proof ila unahitaji kujipinda ni kwenda straight gen ya 8, (gen ya 7, 6, 5, 4, 3 na 2 ni kama zinafanana) hapa utafute pentium ama i3 ama celeron ya gen ya 8, ila itabidi uhangaike sana, naziona sometime hadi laki 5, I hope zitakuwepo za bei ya chini zaidi.

Kuna option nyengine sema hii ni kama Una kwenda all out kwenye video editing na una sacrifice mambo mengine kama gaming, Autocad na mambo mengine ya single thread perfomance.

Kuna machine za xenon zenye dual cpu unaweka cpu mbili kwenye motherboard moja, cpu moja inakuwa na core 6 na thread 12, hivyo unapata core 12 na thread 24, hizi ni zaidi ya i7 yoyote chini ya gen ya 8, ila zinakula umeme balaa.

Huyu mdau kuna kipindi alikuwa nazo
MTOTO WA KUKU

Zipo pia maduka mengi ya madesktop, sema hizi si future proof Sababu ni gen za kizamani.
Mkuu desktop ya i3 generation ya 8 ina core ngapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom