apple mac mini, computer nzuri kushinda zote?

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,735
39,836
apple jana walizindua vitu vingi kwenye event yao lakini kwenye macho yangu niliona ni vya kawaida na havikuwa vya kushangaza. ila pale nilipokuja kuiona mac mini nilishangaa sana na sikutegemea apple kutoa kitu kama hiki.

kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu hizi mini pc zipo nuc, saphire edge, gigabyte na hizi mac mini lakini nyingi zilikuwa either zina specs ndogo au zikiwa specs kubwa basi bei nayo inakuwa kubwa.

ni nini mini pc?
kwa wale ambao hawafahamu hizi ni computer ndogo sana ambazo zinareplace desktop zetu kubwa, zinakuwa haziji na monitor ni nzuri kueka sebuleni pamoja na tv yako, zinakuwa na hdmi port na pia zinatumiwa sana na designer ambao hawawezi ku afford pc za bei ghali.
apple_mac_mini_2014_apple.jpg


specification za mac mini 2 ya 2014
mac mini hii itakuja na flavour tatu ambazo ni

1.mac mini ya dola 499
dola 499 ni around 800,000 mpaka 900,000 za tanzania na kwa bei hio utapata latest core i5 4th generation yenye speed ya 1.4ghz pamoja na gpu ya intel hd5000. kwa wale wasiofahamu hiki ki mini kwa specs hizo hapo juu ni powerful kuliko surface pro ya i5 na mac book air hivyo unapata powerfull machine kwa bei ndogo. itakuwa preloaded na os ya yosemite, ram yake itakuwa ni 4gb na hdd ni 500gb rpm5400.

hiki ni kizuri kwa watu wanaocheza game ambazo ni za kawaida kama fifa na pes, wanaoedit picha na photoshop na pia wanaoanza video editing.

hii ndio perfomance ya intel hd5000 kwenye fifa
u3Slvfd.jpg

hivyo utaweza kucheza hadi ultra setting full hd na gpu hii.

2.mac mini 2 ya dola 699
hii itakuwa ni kama around 1,200,000 za kitanzania na itakuja na specs hizi. processor intel i5 4th generation 2.8ghz dual core, na gpu ya iris pro. hii gpu ya iris ni very powerfull ina uwezo wa kucheza karibia games zote za ulimwengu huu. pia utakuwa na uwezo wa kuchagua either 1tb ya rpm5400 kama hdd yako au 256gb ssd. kama unapenda games au una shughuli nzito kama video editing ssd ndio choice nzuri. ram yake itakuwa ni 8gb.

mac mini hii ndio imenifanya niandike huu uzi, ukitaka laptop/desktop yenye specs kama hizi itaanzia dola 1000 kupanda juu lakini kwa mtu nisiemtegemea ameleta machine kama hii kwa dola 700 tu. hebu angalia jinsi gani iris inavyohandle fifa 14 na 15, crysis, far cry na battlefield
6OPnBei.gif

game kama fifa 14 hii gpu inaenda hadi 300fps hivyo nafkiri hakuna mjadala kuhusu iris

kama unajiweza hii ndio computer ya kumiliki unatupia chochote inafanya kwa bei ambayo ni fair.

3. mac mini 2 ya 999
tumeshaingia kule ambapo sio mahala petu sasa hii ni kama 1,7000,000 ya kitanzania na itakuja na i7 4th generation 3.0ghz dual core, ram 16gb, 1tb ya flash storage na hii pia ina iris pro kama gpu.


je unasemaje? hii mac mini ni over priced au bei ni fair?
 
Sasa hivi apple wanauza logo, true price hapo ni nusu ya hiko kitu
 
Good but duh bado weng hatuwezi ku afford hiyo price...izi za laki tano kumbe cnzuri au ni za kubahatisha?
 
kaka kila kitu na matumizi yake. kama unaangalia video na kutumia ms word hio ya laki 5 inatosha
Nataka nichukue ya laki 750000 mpaka 800000 niwe natumia ms word na bila kusahau games sijui nitapata mkuu? Ila sihitaji Apple nahitaji Lenovo.
 
Nataka nichukue ya laki 750000 mpaka 800000 niwe natumia ms word na bila kusahau games sijui nitapata mkuu? Ila sihitaji Apple nahitaji Lenovo.
Laki 2 na nusu mpaka 3 brand za hp, lenovo, dell etc vile vidogo kabisa.
 
Back
Top Bottom