Nini uhusiano wa Bongo FM na TBC

Protector

JF-Expert Member
May 20, 2019
419
889
Nisiwachoshe niende kwenye mada moja kwa moja. Nimevumilia sana ila nimeshindwa, napenda kujua uhusiano ulipo kati ya Bongo FM na TBC kwa sababu mic ya Bongo FM zina stika ya TBC.
Je, ni tawi la TBC au ni kampuni binafsi TBC ana hisa zake? Mwenye kujua anijuze
Screenshot_20240516_191052_Facebook.jpg
 
Ina maana hujui kuwa hiyo ilikuwa TBC FM? Wameibadilisha jina na kuizindua upya eti iwavutie vijana na ishindane na Clouds fm, wasafi fm na e fm!. Hiyo redio ni kitu kimoja na TBC.
 
Ina maana hujui kuwa hiyo ilikuwa TBC FM? Wameibadilisha jina na kuizindua upya eti iwavutie vijana na ishindane na Clouds fm, wasafi fm na e fm!. Hiyo redio ni kitu kimoja na TBC.
OK chief nilikuwa sijui hilo, asante kwa ufafanuzi wako
 
Ina maana hujui kuwa hiyo ilikuwa TBC FM? Wameibadilisha jina na kuizindua upya eti iwavutie vijana na ishindane na Clouds fm, wasafi fm na e fm!. Hiyo redio ni kitu kimoja na TBC.
Wamebadilisha na frequency au zimebaki zilezile?
 
Hiyo redio ilianza kuitwa city radio, ikaitwa PRT, halafu TBC FM na sasa Bongo fm. Wanaona ni ubunifu kubadili brand name ili kuwavutia vijana. Wana watangazaji vijana wengi akina upete na wachambuzi wa soka wengi ni vijana kama kina abdulghafal chissano na wengine wengi
 
Tawi la TBC kwa ajili ya wateja vijana..hii inapambana na hizi FM zingine na hakuna kufuata sana itifaki kama ilivyo kwenye hizo TBC zingine. Huku ukikuta mtangazaji anaongea kama yuko mtaani sawa tu
 
Back
Top Bottom