Nini Tofauti ya Home Theatre na Sond Bar?

Nini Tofauti ya Home Theatre na Sond Bar?

Wa Salaam ndugu.kuna hawa waarabu wanapita na magari mashuleni. Wameniuzia home Thearte ya watts 210 ila napenda kujua tofauti ya Sound Bar na Home Theatre.
Walinianzia 550,000 ila wakanipa kwa 500,000. Niliipenda ilivyo.
Bila picha itakuwa Kam chai
 
Tafsiri ya Home theatre au Sound bar ipo katika maana ya moja kwa ya hayo maneno...

Home theatre: Huu ni mkusanyiko wa spika uliotengenezwa ili zipangiliwe maeneo tofauti tofauti ndani ya chumba katika mtindo unaomithilika na ule unaopatikana kwenye kumbi za kuonesha sinema ili kutengeneza sound effect sawa sawa na uhalisia wa milio ya sauti...

Kama unatazama movie na sauti ilipaswa uisikie upande wa kushoto, basi utaisikia upande huo hivyo hivyo na pande nyingine na effects nyingine...

Sound bar: Huu ni mche wenye mkusanyiko wa speaker (all-in-one) unaotumiwa sana na TV ili tu ku-extend speaker za TV...
 
Tafsiri ya Home theatre au Sound bar ipo katika maana ya moja kwa ya hayo maneno...

Home theatre: Huu ni mkusanyiko wa spika uliotengenezwa ili zipangiliwe katika mtindo unaomithilika na ule unaopatikana kwenye kumbi za kuonesha sinema ili kutengeneza sound effect sawa sawa na uhalisia wa milio ya sauti...

Kama unatazama movie na sauti ilipaswa uisikie upande wa kushoto, basi utaisikia upande huo hivyo hivyo na pande nyingine na effects nyingine..sound bar ikoje mkuu
 
Tafsiri ya Home theatre au Sound bar ipo katika maana ya moja kwa ya hayo maneno...

Home theatre: Huu ni mkusanyiko wa spika uliotengenezwa ili zipangiliwe katika mtindo unaomithilika na ule unaopatikana kwenye kumbi za kuonesha sinema ili kutengeneza sound effect sawa sawa na uhalisia wa milio ya sauti...

Kama unatazama movie na sauti ilipaswa uisikie upande wa kushoto, basi utaisikia upande huo hivyo hivyo na pande nyingine na effects nyingine...
Asante na Sound Bar ipoje?
 
Asante na Sound Bar ipoje?

Nimeandika pia...

Kama ni mtu wa kutazama sana movies na tamthiliya, mpenzo kindaki ndaki wa music, bajeti inaruhusu basi nunua Home theatre...

Kama ni mtu wa matumizi tu ya kawaida ya TV, si mpenzi sana wa movies au music au tamthilia, bajeti ipo limited basi nunua Sound bar...
 
Wa Salaam ndugu.kuna hawa waarabu wanapita na magari mashuleni. Wameniuzia home Thearte ya watts 210 ila napenda kujua tofauti ya Sound Bar na Home Theatre.
Walinianzia 550,000 ila wakanipa kwa 500,000. Niliipenda ilivyo.
Hao wanawapiga sana ila kwa sababu mnawakopa mnaona poa.
Pressure cooker ya 120k wanauza 300k
 
Sound Bar JBL 5.1 Channel.
Ni kitu bora sana sema bei yake ndio imechangamka kidogo ingawaje zipo zenye 2.1 channel na 3.1 channel ndogo zake..
 
Mimi sijaona tofauti yake kwenye sound manake Home theater nilitumia ya Samsung ilikuwa poa kabisa.

Pia nimetumia sound bar ya Bose ina 4 mini sound system na Bass yake hii ipo vizuri zaidi lakini naona hazina tofauti sana. Ni opinion yangu tu
 
Back
Top Bottom