Nini tofauti ya Hirizi, Rozali na Tasbihi?

Nini tofauti ya Hirizi, Rozali na Tasbihi?

Tofauti ni hizi : 1. Rozari ni sala inayotumiwa na wakristu haswa wakatoliki na waanglikan, ina maneno aliyosema mhalaika alipomtokea bikira maria 2. Tasbihi ni chombo kinachotumika kwenye kusali ili anayesali asikosee idadi ya sala aliyokusudia, hutumiwa na wakristu na waislam, hapa naona wengi wanachanganya sala na chombo kinachotumika, kwa wakristu sala ya rozari takatifu hutumia chombo kinachoitwa tasbihi, hivyo ile inayovaliwa ni tasbihi ila sala ndi inaitwa rozari. Tasbihi ya wakristu na waislam zinatofautiana. Hirizi ni chombo kinachotengenezwa na wanaoamini uchawi kupiga watu mkwara.

Jibu hili limeshiba kila aina ya Vitamin..
 
Naona zote ni sawa. Mwenye kujua tofauti zake anijulishe. Uchawi wa Kirumi, Uchawi wa Kiarabu na Uchawi wa Kiafrika.

mshana jr
mzee wa chanting karibu sana..

Nimechelewa kuja Bujibuji niwie radhi, tofauti yake iko kwanza kwenye mwonekano moja ina msalaba, nyingine ina kifundo na ya mwisho ina kitu kama kinyoya
Lakini vilevile ni idadi ya shanga rangi na matumizi
 
Last edited by a moderator:
Hirizi wanatumia Wachawi na washirikina katika mambo yao.

Rozari wanaitumia wakristo hasa Waroma katika Ibada zao.

Tasbihi wanatumia Waislam katika Ibada zao hasa ya Kuyataja na kuyatukuza majina matakatifu ya Allah (s.w)

Nadhani izo ndo tofauti kuu.
Rozari na tasbihi zote humrahisishia anaesali/kuswali kupata hesabu sahihi katika sala/swala yake pale inapohusisha kurudiarudi sala/swala ya aina moja.

Hirizi naona inatumika zaidi kichawi.
 
Hirizi wanatumia Wachawi na washirikina katika mambo yao.

Rozari wanaitumia wakristo hasa Waroma katika Ibada zao.

Tasbihi wanatumia Waislam katika Ibada zao hasa ya Kuyataja na kuyatukuza majina matakatifu ya Allah (s.w)

Nadhani izo ndo tofauti kuu.



Nini tofauti kati ya Ibada na Ushirikina?.
Je na Waganga wa Jadi nao wanachokifanya siyo Ibada ?.(Mungu wa Mwafrika)

cc Bujibuji Yericko Nyerere (Mada -Mungu wa Mwafrika)
 
Last edited by a moderator:
Halafu pia wale wanaosema wakatoliki sala ya rozari haipo kwenye bible wakasome jinsi malaika alietumwa na mungu kwa mariamu alivyomwambia maria ujumbe kutoka kwa mungu hiyo inapatikana luka sura ya 1: aya ya 28-35

MALAIKA ALIMWAMBIA MANENO HAYA. JE ALIYASEMA AKIWA KASHIKILIA ROZARI? AU UNA MAANA GANI???

Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
 
Hakuna tofauti. Zina maana ile ile katika imani tofauti.
 
wote hawa uliowataja ni ndugu tena mapacha kutoka tumbo moja ila wamelelewa mazingira tofauti. wanadamu wa leo wanawaangalia hawa kwa mavazi yao na maneno yao na kudhani ni tofauti kumbe tofauti zimetokana na malezi waliyoyapata baada ya kutengana lakini wote hawa asili yao ni moja.

Naona zote ni sawa. Mwenye kujua tofauti zake anijulishe. Uchawi wa Kirumi, Uchawi wa Kiarabu na Uchawi wa Kiafrika.

mshana jr
mzee wa chanting karibu sana..
 
Ni ngumu kuonyesha tofauti za vyombo/vifaa hivi. Kwanza ili uweze kuonyesha tofauti lazima ujipambanue upo upande upi.

Kwa wakrito wa madhehebu ya kikatoliki wao huamini Mama wa Yesu Bikira Maria aweza kumuombea mtu kwa mwanae kama ilivyotokea kwenye harusi ya Kana. Rozari ni kifaa maalum ambacho hutumika kumuongoza mtu (mwenye kuamini) kusali kumuomba Bikira Maria ili amwombee kwa mwanae Yesu Mnazareti. Ndio maana BIKIRA MARIA hufahamika kama Mama wa Rozari Takatifu.

Hirizi ni kifaa kinachotumiwa na mtu (mwenye kuamini) katika kumuunganisha na mizimu ya kwao. Hii hufanyika ili kumsaidia kumweka karibu na Mungu wake kupitia mizimu yake. Kama ilivyo kwa Imani nyingine suala hili ni la kiimani zaidi.

Wapo pia wenye kupewa hirizi zenye "majini" ndani yake lengo likiwa ni kupewa ulinzi na usalama ktk kazi, biashara na maisha ya kila siku.

Kuhusu tasbihi hili swala ni la kiimani zaidi na wenye Imani yao hawapendi kufikiri nje ya boksi. Ni vizuri kuheshimu fikra zao kwa kukaa kimya.

Umeonyesha Hekima ktk kuheshimu Imani za watu.
 
MALAIKA ALIMWAMBIA MANENO HAYA. JE ALIYASEMA AKIWA KASHIKILIA ROZARI? AU UNA MAANA GANI???

Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Mambo ya Kiroho ni ngumu kuyaelewa ukitaka kulazimisha sana Akili yako iweze kuelewa,mimi ni Mkatoliki na ninasali Rozari almost kila siku kwasababu inanisaidia sana;Kwa ufupi Rozari Takatifu-ni ufupisho wa Injili,hivyo kwa kusali Rozari tunakuwa tunatafakari Maisha na Matendo ya Kristo pamoja na Mama yake,Yaani kuanzia Masimulizi ya utoto wa Yesu,Namna alivyofanya kazi yake ya kuhubiri hbr njema,Mateso yake,Kifo,Ufufuko wake hadi Kupaa kwake kwenda Mbinguni,Karibu RC uonje utamu na Raha ya Kusali Rozari Takatifu.
 
Back
Top Bottom