Tofauti IPO na ni kubwa saana. Mimi nimepitia sehemu mbili kati ya hizo 3.
Hirizi. - hii ni kinga au tochi au king' amuzi inategemeana umepewa kwa ajili gani? na si kila mjuzi anayeweza kukupatia HIRIZI ya kweli.
Kinga kwa maana wabaya watu wanaotaka kukudhuru kwa uchawi au kwa nguvu za mwili kawaida wanashindwa.
Tochi au king'amuzi hiki hutumiwa zaidi na watu waliokatika mamlaka hasa ya ukamataji huweza kung' amua kitu kilichofichwa au mhalifu na hata wahalifu kuweza kuwang'amua walinzi au kuahirisha siku ya uhalifu. Au kutoonekana kwenye eneo la uhalifu. Au kiongozi kuogopwa na kunyenyekewa na wote walio chini yake na wakubwa zake nk.
Rozari - hii ni mahususi kwa ajili ya Wakatoliki pekee, ambao kwa mujibu Wa mfumo Wa kanisa lao,
Imepanga maombi mbalimbali yaliyokatika mpangilio kupitia Msalaba wenyewe uliokatika Rozari na kila punje zilizo katika mpangilio Wa pamoja na iliyo pekee.
Tasbih - hii huwa nawasikia wakirudia neno SUBHUANAH ALLAH, SUBHUANAH ALLAH kila anapoishika punje tofauti kwa mpangilio Wa kusogea mbele.