Nini solution ya hili? Kudumu kwenye ndoa

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,559
Reaction score
89,157
Hellow JF?

Leo nataka nizungumzie suala la kudumu kwenye ndoa, tumeona wazee wa zamani wamekuwa wakidumu kwenye ndoa kushinda vijana wa sasa.

Ndoa za sikuhizi kudumu hata miaka miwili imekuwa kwa mbinde, nimeona katika jamii ndoa zikivurugika kwa mambo madogomadogo, wazee ndio wamekuwa waamuzi wa migogoro hiyo mengine yamekuwa yakiwezekana lakini mengine ngumu kumeza.

Vijana wamekuwa wakilalama na mapenzi kila kukicha, vilio vya kutendwa imekuwa kama wimbo maarufu.Sijui mapenzi ya sasa yamekuwa matamu zaidi lakini mbona wazee wetu wameweza kuyamudu hata kama kulikuwa na migogoro ilimalizika na ndoa ikaendelea kama kawaida.

Kwetu tatizo ni lipi? Wakulaumiwa ni wazee wetu kwa kushindwa kutupa msingi wa haya mambo au wa kulaumiwa ni vijana kwa kuwa na tamaa, kushindwa ku handle mapenzi na kushindwa kufuata maelekezo ya wazee wetu.

Je, nani wa kulaumiwa?
Na nini solution la hili tatizo?
Toa mchango wako kuokoa jahazi hili maana liendako hapastahili.

Karibuni.
 
vijana,wazee,wakati,maendeleo ya teknolojia,hali ya maisha,kila mmoja/kimoja kwa nafasi yake vimechangia katika suala hilo.

how.....(sababu ya muda sitagusia kiundani zaidi)...
 
Wanawake wa zamani(mama/bibi tu) walikuwa wavumilivu, they could take all BS from our dads/grandpas may be kwasababu za kiuchumi,kijamii etc. Ila hawa wa sasa,hawawezi kuvumilia upuuzi. Hii ni moja ya sababu.
 
kivipi..?
 
nini solution ya hili..?
 
Ndoa inahitaji uvumilivu wa pande zote mbili kwanzia kwenye mahusiano
Unachotakiwa kukifahamu ni kila mtu ana tabia zake binafsi hivyo kupelekea mapungufu yake kama binadamu wa kawaida...tumia muda mwingi kumchunguza mwenza wako ili ujue namna ya kuishi nae aidha ukiona kasoro zake huziwezi ni bora mkaachana mkiwa wapenzi na ukatafuta mwingine lakini kikubwa ni kujifunza uvumilivu...hakuna mkamilifu hapa Duniani.
 
yapo mengi sana yanayochangia ndoa zetu za siku hizi zisidumu.

1.KUANZA NGONO MAPEMA. vijana wa siku hizi tunaanza ngono mapema hivyo kutokana na kujua radha mbali mbali za sehemu ya kati ya mwili wa binaadam tunajikuta tukishindwa kuendelea na mahusiano baada ya kugundua radha ya mke ilikuwa tofauti na yule aliepita.

2.UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. hii inatuhusu sisi wanaume kutokana na mabinti kuwahi kuanza ngono mapema, ata kwenye kumkuna inahitajika nguvu ya ziada ila ukimpapasa papasa matokeo yake ni kuachika au mwanaume kuachwa.

3.WANAWAKE KUTOWASIKILIZA WAUME ZAO. kutokana na utandawazi haswa hii aki sawa ya kupata elimu, wanawake wengi wanajikuta wameelimika na kuzijua haki zao za kimsingi na kusahau kuwa katika mahusiano ni haki ya mume kuheshimiwa na mke. hivyo wanawake wengi wanasahau haki hiyo ya mume kutokana na wao kuwa na elimu matokeo yake ni ndoa kuvunjia bibi zetu walimudu kudumu katika ndoa maana wao kinabibi walifundishwa kuwatumikia wanaume. ila sio kinadada wa siku hizi

4.TAMAA ZA NGONO, kutokanA na utandawazi na kukithiri kwa mapicha ya ngono mitandaoni vijana wengi tumejikuta tukikosa uvumilivu wa kingono na kujikuta tunasahau wake zetu na kufanya tendo na wanawake wengine ili tu kumaliza tamaa za kingono zinazotukaba pengine ni offisi. mwisho wa siku ni ndo zinavunjika baada ya mwanamke/mwanaume kugundua kuwa mwenzie ana mpango wa kado.....yapo mengi sana ila baadae nitarudi kuendelea kutililika
 
Mwanaume ndiyo kichwa cha familia (imeandikwa hivyo kwenye biblia), wanawake wa sasa hawataki kufuata maelekezo toka kwa waume zao. Wanataka wao ndiyo watoe maamuzi kwenye familia. Na mwanamke akiwa kichwa kwenye familia mambo huenda kombo. Huu ni uzoefu wa miaka 6 kwenye ndoa. Ukioa au kuolewa jitahidini muwe mnaendana ki tabia, msiangalie muonekano wa nje kwa sababu kwenye ndoa uhalisia huonekana kwa uwiano wa tabia zenu
 
mbona lawama kubwa umezipeleka kwa wanawake tu,mwanaume hawezi kusababisha kuvunjika kwa ndoa..?
 
eddy_mhando
solution kwa hayo uliyoyaandika bila shaka ni kwa kuyageuza lkn hilo no 3 nnamtazamo tofauti
nadhani wote wasikilizane na kufikia maamuzi ya busara.
asante
 
yapo mengi sana yanayochangia ndoa zetu za siku hizi zisidumu.
1.KUANZA NGONO MAPEMA. vijana wa siku hizi tunaanza ngono mapema hivyo kutokana na kujua radha mbali mbali za sehemu ya kati ya mwili wa binaadam tunajikuta tukishindwa kuendelea na mahusiano baada ya kugundua radha ya mke ilikuwa tofauti na yule aliepita.
2.UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. hii inatuhusu sisi wanaume kutokana na mabinti kuwahi kuanza ngono mapema, ata kwenye kumkuna inahitajika nguvu ya ziada ila ukimpapasa papasa matokeo yake ni kuachika au mwanaume kuachwa.
3.WANAWAKE KUTOWASIKILIZA WAUME ZAO. kutokana na utandawazi haswa hii aki sawa ya kupata elimu, wanawake wengi wanajikuta wameelimika na kuzijua haki zao za kimsingi na kusahau kuwa katika mahusiano ni haki ya mume kuheshimiwa na mke. hivyo wanawake wengi wanasahau haki hiyo ya mume kutokana na wao kuwa na elimu matokeo yake ni ndoa kuvunjia bibi zetu walimudu kudumu katika ndoa maana wao kinabibi walifundishwa kuwatumikia wanaume. ila sio kinadada wa siku hizi
4.TAMAA ZA NGONO, kutokanA na utandawazi na kukithiri kwa mapicha ya ngono mitandaoni vijana wengi tumejikuta tukikosa uvumilivu wa kingono na kujikuta tunasahau wake zetu na kufanya tendo na wanawake wengine ili tu kumaliza tamaa za kingono zinazotukaba pengine ni offisi. mwisho wa siku ni ndo zinavunjika baada ya mwanamke/mwanaume kugundua kuwa mwenzie ana mpango wa kado.....yapo mengi sana ila baadae nitarudi kuendelea kutililika
Mkuu umenena yote...hamna haja ya kuongeza...mtu anaingia kwenye ndoa after more than 20 relationships, what do you expect??? kwa vyovyote vile hawezi kuishi ndoa kama yule aliyeolewa akiwa bikra!!!!
 
asante kwa kunielewa mzee mwenzangu
 
Kinachowaunganisha ni Upendo. Na uwepo Upendo wa dhati kati ya mume na mkewe. Unapompenda mwenzako hauwezi kumtenda kwa vyovyote vile, utamthamini, utamheshimu, utajali hisia zake na yote mema. Kwa hiyo si tu kusema wake si wavumilivu, pengine na waume nao wamevuka mipaka ya kuweza kuvumiliwa.
 
tufanye nini kurudisha upendo kama wa wazee wetu..?
 
Haki sawa uchwala..wanajkuta na wenyewe wanaume siku izo!!mi NGOs chungu mzma utasema wanaume tumekuwa wanyama siku izi
 
Kazi ya moyo ni kusukuma damu, Kupenda ni kiherehere...
Try to control you lover as you control your business, use your mind not your heart.
 
Back
Top Bottom