Nini msimamo wako kama mtanzania. Serikali,mbili au tatu

Moja tu ya Tanganyika wapemba warudi kwao na Watanganyika warudi kwao basi imetosha.
 
Tunachotaka watanzania ni Katina mpya na siyo serikali mpya sasa nashanga hili la serikali ya tatu imefuata nini
 
Nimi nampongeza sama JK lea hotuba yake ya karne ametueleza hasara za serili tátu na faida za serikali mbili. Kwamba mbili changamoto zake zinazungumzika na gharama zake ní nafuu sana ukilinganisha na serikali tátu.
 
1na1 ni 2 pata, 1na2 ni 3 kosa, lipi jibu sahii wajibu ambao elimu yao ni chuo kikuu tuu maana ndio wanaotupotosha.
 
Miaka 50 ya muungano imeshindikana kurekebisha hizo kero ndani ya serikali 2 itawezekanaje ndani ya siku 90? Jibu ni serikali 3 ama kila 1 kivyake.
 
mbona kwenda z'bar mpk kitambulisho ndo muungano gani huo sasa, bora kila mtu kwao kwan tumefaidika nin sasa
 
Naombeni mawazo yenu kwa upande zote,faida zake na hasara zake kwa manufaa ya wananchi

mawazo yangu yapo nje ya swali...!me naona muungano uvunjwee kila mtu akae kivyake

so natamani sana serikali moja ya Tanganyika
 
Hapa mimi naona serikali moja kwa Tanganyika na moja kwa Zanzibar zinatosha kila mtu afe na lwake kwake mizozo ya muungano iishie mbali. Alafu hapo sasa wabara waliopo Zanzibar warudi kwao au waombe uraia wa huko, vivyo hivyo Wazanzibar waioko Bara warudi kwao au waombe uraia wa bara.Maoni yangu haya.
 
Serikali mbili ya Muungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar iko wapi Tanganyika? Kama ndivyo tuwe na serikali moja tu ya Muungano vinginevyo kila upande uwe na serikali yake.
 
Kinachotakiwa ni tanganyika itambulike, maana zanzibar ilishajitoa, ni sawa na ndoa tunayolazimishana, nakumbuka miaka ya nyuma mpk tisini zanzibar tulikuwa tunakwenda kwa pasport lkn wao wakija huku bure, hii ni ndoa ya kikristu watu mmechokana lkn mnaishi tu mpk kifo kiwatenganishe.
 
Mi naona Wazanzibar ni wakorofi sana na wanajiona sana kwahiyo serikali 3 inawatosha. Just imagine mpo nchi za watu alafu mnaulizwa nyie mnatoka nchi gani Mzanzibar anasema am from Zanzibar, me am from Tz wenyeji wanauliza hivi Zanzibar ndo nchi gani jamaa anaanza maelezo ya kudebate na kucriticize na kutetea kua Zanzibar is autonomous state , dah mi hua nachoka kweli hawa wenzetu.
 
TANGANYIKA + ZANZIBAR = 1 au.TANGANYIKA, ZANZIBAR na MUUNGANO =3 BAAAAASI. Serikali mbili ni ZANZIBAR NA IPI??? Tuache ukasuku wa kuabudu "fikra sahihi za mwenyekiti wa ......".Huu sio muungano ni kiini macho.
 
Hapa piga ua... serikali ni mbili tuuu. Makelele ya mlango hayazuii mwenye nyumba kulala. Inabaki kuwa kero tu...!
 
kwanza muungano ufe ndo utamaliza utata huu, kwa sababu kama mke moja kakushinda huwezi waza kuoa wapili serikal nyingi za nini wakati mbili tu matatizo
 
Back
Top Bottom