Kijana leo
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 2,861
- 808
dodoma hawajawah kupata mbunge bora.
dodoma hawajawah kupata mbunge bora.
Hivi ndo huyu wasouth walimpa PhD sawa na zile za baba mwanaisha.
Walau Malolle anajitahidi coz barabara zote za mjini na mitaa ya pembezoni mwa mji zimetengenezwa kwa kiwango cha lami
nadhani katiba mpya iwe open ktk hiliUpo sawasawa huwa namshangaa kusikia heti mbunge kaleta maendeleo kajenga shule barabara zanati ujinga mtupu na majungu ukimuwangalia mbunge hata gorofa hana hiyo barabara atajengaje nyambafu
Remote
Kuna tatizo la kujua majukumu ya Mbunge. Nina uhakika hata wao hawajui majukumu yao. Kwa ufupi Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika ngazi mbali mbali kuanzia jimbo, wilaya au mkoa. Kwa upande mwingine ni mwakilishi wa wananchi katika ngazi ya taifa ambayo ni Bunge.
Mbunge si mtendaji kikazi. Kazi yake ni coordination ya haja za wananchi na maamuzi yatakayoathiri wananchi wa eneo lake. Ni mfuatiliaji wa maamuzi yanayohusu wananchi wake katika ngazi za jimbo hadi taifa.
Si kazi ya mbunge kutoa pesa za shughuli za maendeleo kwasababu hana fungu.
Mbunge anapaswa kuangalia mafungu yaliyopo au kujenga hoja za kutafutwa fungu kwa haja ya kutimiza malengo mengine yenye ulazima na umuhimu.
Fungu la pesa za mbunge linalotolewa sasa hivi ni hongo tu halina maana yoyote.
Ni njia ya kumuongezea mbunge kipato. Fungu hilo halina audit na anayepaswa kuamua nani apate nini ni mbunge, kinyume na utawala bora.
Kujenga shule n.k kwa pesa zao ni hongo tu, hilo si jukumu lao.
Jukumu lao ni pamoja na kuangalia usalama na ustawi wa jamii zao.
Jiulize kuna sababu gani za kujenga shule wakati wafugaji na wakulima wanapigana. Mbunge amefanya nini kuhakikisha usalama wao.
Concern ya mbunge siku zote ni kuhakikisha kunakuwepo na mawasiliano ya uhakika na vyombo vingine akiwa kama go between na si kumwaga pesa.
Kwa nchi za wenzetu imefika mahali ofisi ya mbunge inasikiliza matatizo ya mtu mmoja mmoja ambayo ynahitaji msaada mkubwa (siyo kugawa pesa za chakula )
Mfano, mbunge anafuatilia kwanini mpiga kura wake amenyimwa haki ABCD au hakutendewa EFG na kwamba hilo ni tatizo la mfumo, watu au kitaifa.
Kama ni kitaifa mbunge atalifikisha bungeni kujadiliwa. Endapo ni mfumo wahusika watawajibika n.k.
Endapo kuna anayedhani kazi ya mbunge ni kutoa mipesa au misaada, sasa wale wa kuteuliwa na vyama au Rais wana kazi gani. Watatoa misaada wapi.
Kazi ya mbunge ni uwakilishi kwa ukubwa na upana wake, ngazi ya jimbo hadi taifa
Upo sawasawa huwa namshangaa kusikia heti mbunge kaleta maendeleo kajenga shule barabara zanati ujinga mtupu na majungu ukimuwangalia mbunge hata gorofa hana hiyo barabara atajengaje nyambafu
naskia wengi wanasema ni kuwasilisha matatizo ya wananchi wake bungeni/serikalini ....sasa hebu naomba kujuzwa wabunge wengi wanaishi dar wanajuaje matatizo ya wananchi wao?.,sioni haja ya kua na mbunge na wakuu wa mikoa na wilaya wanatosha
naskia wengi wanasema ni kuwasilisha matatizo ya wananchi wake bungeni/serikalini ....sasa hebu naomba kujuzwa wabunge wengi wanaishi dar wanajuaje matatizo ya wananchi wao?.,sioni haja ya kua na mbunge na wakuu wa mikoa na wilaya wanatosha