Nini Majukumu ya Mbunge kwa wapiga kura wake?

Unazungumzia wabunge wa chama tawala? Kama ndio, wao wana kazi kuu zifatazo:-
1: kuunga hoja mkono kwa 100% kabla hajachangia na hitimisho lake anatoa matatizo ya jimbo lake.
2:- kusinzia mapema kabisa na akistuka anagonga meza kushangilia asichokisikiza!
3:- ni wabadhirifu kupindukia na wanashirikiana na wakurugenzi wa halmashauri watokako kuiba hela za walimu.
4:- ni wanafiki na hawana chembe ya uzalendo kwa nchi yao, mfano kwenye bunge la katiba.
5:- wapo kimaslahi zaidi na wanawaza posho tu mfano leo hii wanajiongezea ili ifike laki 5.
6:- wale wa viti maalumu wapo kupiga vigelegele na mipasho kwa kwenda mbele as if wapo kijiweni.
Ni bunge la aina yake katika sayari yetu kwani haliisimamii serikali kuhudumia wananchi. Nawashauri wawaige wabunge wa upinzani kwa uwezo wao wa kuibua na kujenga hoja current. Kujikomba kwao ccm kutawamaliza kisiasa.
 
teteteteteetetete......teteteteteteetetetete.....tetetetetetetetete...hivi wabunge wana kazi au wana wajibu?.
 
Nadhani kuna dhana potofu kuhusu majukumu ya mbunge kwa wengi tukidhani mbunge kazi yake ni kujenga shule, vituo vya afya na bara bara. dhana hii potofu imetupelekea kuwa na watu wanaogombea ubunge ambao hawafanyi majukumu yao bali kutafuta michango ya shule au kusaidia mabati, vifaa mbalimbali.

Kazi za maendeleo ni jukumu la serikali na mbunge kazi yake ni kuwakilisha wananchi kuhakikisha serikali inatimiza wajibu wake.

Hivyo anayetakiwa kuwajibishwa wa kwanza kwa sehemu kutokuwa na shule, kituo cha afya, barabara na mengine ni raisi. lakini haya yanategemea upatikanaji wa fedha hivyo kama vimepangwa na havikutekelezwa hapo ndipo mhusika awajibishwe au kama mnarukwa kama nyie hamna maana.

Ila kama serikali inafanya madudu kwenye eneo lenu na hayo madudu hakuna wa kuyafuatilia hilo ndilo la kumuwajibisha mbunge. uzembe, kiburi cha watumishi, rushwa, kodi zisizokuwepo na mengine haya mbunge anatakiwa kuyafuatilia.

Miradi ya maendeleo iliyopangwa kwenye eneo lenu imetekelezwa na kwa ubora gani hilo ni jukumu la mbunge.
 
Kivipi kwa kugusa maslahi ya wachache wanaokula fedha ya nchi hawafanyi kazi ya kusimamia serikali bali kujidhania ni watu wa ngo za kutafuta misaada katika jamii?

Kumsimamia anayefanya na kujisema wewe ndiye unayefanya ni vitu viwili tofauti.

Kama una mali unahitaji kuchagua mtu wa kukuwakilisha kulipwa fedha na akatafuta michango ya kuklusaidia ua unatafuta mtu wa kusimamia mali zako ili zitumike vizuri?

Mbona unajikanyaga?
 
HATA sijasoma umeandika nini, ila simply kwa nchi kama yetu kuwa na bunge ni kufuja pesa tu. Kimsingi sioni umuhimu wa hilo bunge lenyewe. lifutwe tu. Nchi kama Ujerumani kipindi cha Hitler ziliendelea kwa sababu hakuona umuhimu wa vitu kama hivo.
 
Nimepitia post mbalimbali zilizokuwa hasa zinawagusa wabunge wa upinzani, nikagundua yafuatayo...

1. wanalaumiwa sana kwa kutokufanya shughuli za kimaendeleo majimbomi kwao... nanuku, mnyika anaiga piga kelele bungeni ila jimboni kwake hajafanya lolote.

NIWAKUMBUSHE TU HAWA WANAOSEMA HIVYO KUWA ISINGEKUWA KUWA NA WABUNGE MAKINI KUTOKA VYAMA PINZANI WANAOUNDA (UKAWA) KUFIKIA SASA KATIKA NCHI HII HADI RAIA WANGEKUWA WAMEBINAFSISHWA AU KUUZWA.

TUTAFANYA KOSA KUBWA KAMA HATUTAWARUDISHA KWA WINGI WAO WABUNGE WENYE NIA YA KUWATETEA WANANCHI SI WAUPINZANI TU BALI HATA WALE WA CHAMA TAWALA WALIIONYESHA MTIZAMO CHANA HASA KATIKA KULITETEA TAIFA NA RASILIMALI ZAKE.

MIAKA YA NYUMA ALIKUWA DR SLAA NA ZITO KABWE AMBAO WALIPIGWA VITA SANA HUKU ZITO AKIFUNGIWA KUTOSHIRIKA VIKAO VYA BUNGE MARA KADHAA. LEO HII TUNAO AKINA KAFULILA, MNYIKA, MACHALI, LISU NA WENGINE WENGI AMBAO WAMESIMAMA KIDETE KUTETEA RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE KIHUNU KUHUNI NA WATU WACHACHE TUWAUNGE MKONO NA KUWAPA NAFASI ILI RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE NA WACHACHE KWA MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO.
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Lakini wasiwe wanaota mapepe kwa umarufu wao,wamefika hapo kwa sababu ya vyama na wala siyo akili zao tu.
 
Ni kweli kabisa mleta mada, siku za nyuma kwa ajili ya kukosa elimu ya uraia ilikuwa ni rahisi kuchomeka wananchi kwani walikuwa hawajui wajibu wa mbunge. Matokeo yake wabunge wakawa wafadhili uchwara kila inapokaribia uchaguzi, na wananchi maskini kwa kutokojua hilo wakawa wanapigwa bao kwa kugawa kura kwa viongozi wahuni. Kazi ama wajibu wa mmbunge ni kama ifuatavyo hapa chini
  1. Kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake bungeni.
  2. Kutunga sheria bungeni
  3. Kuishauri na kuisimamia serekali

Katika majukumu tajwa hapo juu hakuna linaloonyesha kazi ya mbunge ni kuleta maendeleo. Anawajibu wa kuhamasisha shughuli za maendeleo jimboni kwake kama kuomba wafadhili ama kuunganisha wananchi katika shughuli za maendeleo, lakini hatutarajii katika mazingira ya kawaida na kipato cha mbunge ajenge barabara, alete maji, alete umeme, kujenga shule, hospital nk kwa kutumia fedha zake za mfukoni. Huo sio wajibu wa mbunge bali anaweza kuwa muhamisishaji. Kazi ya kuleta maendeleo majimboni/nchini ni kazi ya serekali kupitia kodi inazokusanya kwa wananchi wake. Hivyo wananchi wanaodanganywa na propaganda za kiccm eti mbunge kazi yake ni kuleta maendeleo ni kutumia ufahamu finyu wa wananchi katika kukwepa wajibu wa serekali kuletea wananchi wake maendeleo kupitia kodi zao.
 
Nimepitia post mbalimbali zilizokuwa hasa zinawagusa wabunge wa upinzani, nikagundua yafuatayo...

1. wanalaumiwa sana kwa kutokufanya shughuli za kimaendeleo majimbomi kwao... nanuku, mnyika anaiga piga kelele bungeni ila jimboni kwake hajafanya lolote.

NIWAKUMBUSHE TU HAWA WANAOSEMA HIVYO KUWA ISINGEKUWA KUWA NA WABUNGE MAKINI KUTOKA VYAMA PINZANI WANAOUNDA (UKAWA) KUFIKIA SASA KATIKA NCHI HII HADI RAIA WANGEKUWA WAMEBINAFSISHWA AU KUUZWA.

TUTAFANYA KOSA KUBWA KAMA HATUTAWARUDISHA KWA WINGI WAO WABUNGE WENYE NIA YA KUWATETEA WANANCHI SI WAUPINZANI TU BALI HATA WALE WA CHAMA TAWALA WALIIONYESHA MTIZAMO CHANA HASA KATIKA KULITETEA TAIFA NA RASILIMALI ZAKE.

MIAKA YA NYUMA ALIKUWA DR SLAA NA ZITO KABWE AMBAO WALIPIGWA VITA SANA HUKU ZITO AKIFUNGIWA KUTOSHIRIKA VIKAO VYA BUNGE MARA KADHAA. LEO HII TUNAO AKINA KAFULILA, MNYIKA, MACHALI, LISU NA WENGINE WENGI AMBAO WAMESIMAMA KIDETE KUTETEA RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE KIHUNU KUHUNI NA WATU WACHACHE TUWAUNGE MKONO NA KUWAPA NAFASI ILI RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE NA WACHACHE KWA MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO.

Kuna watu wenye akili ndogo watakuja kuropoka hapa mpaka basi. Ubungo wasipomrudisha jamaa, watakuwa wamefanyakosa kubwa mno. Huyu ni hazina kwa Taifa sio ubungo tu.
 
Nimepitia post mbalimbali zilizokuwa hasa zinawagusa wabunge wa upinzani, nikagundua yafuatayo...

1. wanalaumiwa sana kwa kutokufanya shughuli za kimaendeleo majimbomi kwao... nanuku, mnyika anaiga piga kelele bungeni ila jimboni kwake hajafanya lolote.

NIWAKUMBUSHE TU HAWA WANAOSEMA HIVYO KUWA ISINGEKUWA KUWA NA WABUNGE MAKINI KUTOKA VYAMA PINZANI WANAOUNDA (UKAWA) KUFIKIA SASA KATIKA NCHI HII HADI RAIA WANGEKUWA WAMEBINAFSISHWA AU KUUZWA.

TUTAFANYA KOSA KUBWA KAMA HATUTAWARUDISHA KWA WINGI WAO WABUNGE WENYE NIA YA KUWATETEA WANANCHI SI WAUPINZANI TU BALI HATA WALE WA CHAMA TAWALA WALIIONYESHA MTIZAMO CHANA HASA KATIKA KULITETEA TAIFA NA RASILIMALI ZAKE.

MIAKA YA NYUMA ALIKUWA DR SLAA NA ZITO KABWE AMBAO WALIPIGWA VITA SANA HUKU ZITO AKIFUNGIWA KUTOSHIRIKA VIKAO VYA BUNGE MARA KADHAA. LEO HII TUNAO AKINA KAFULILA, MNYIKA, MACHALI, LISU NA WENGINE WENGI AMBAO WAMESIMAMA KIDETE KUTETEA RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE KIHUNU KUHUNI NA WATU WACHACHE TUWAUNGE MKONO NA KUWAPA NAFASI ILI RASILIMALI ZETU ZISIGAWANYWE NA WACHACHE KWA MASLAHI YAO NA FAMILIA ZAO.
Ni kweli wapinzani wamefanya kazi kubwa sana, vinginevyo wale wezi aliowasema makongoro wangetumaliza watz
 
BUNGEJIPYAA.jpg
bunge-house.jpg

KAZI ZA MBUNGE NA BUNGE:

Tunaweza kuzifahamu kazi za mbunge, kwa kuangalia kazi za Bunge:

  1. Mbunge ni mwakilishi wa jimbo (wananchi) katika Bunge.
  2. Bunge litakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho:kitakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii" Ibara ya 63(2), pia na Ibara ya 64(1) inaelezea kazi za Bunge, juu ya kutunga sheria.

​
Mbunge, ni mwakilishi wa jimbo lake katika chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kina madaraka na kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.

Hivyo basi ni makosa kupima kiwango cha mbunge kwa misaada binafsi na majukumu mengine ambayo hayajaainishwa katika shughuli za bunge na mbunge kisheria. Halali wananchi kujenga hoja kwamba mbunge wao hajafanya utetezi bungeni katika masuala yawahusuyo, lakini suala la amaendeleo sio la mbunge binafsi bali ni la serikali.
 
nashangaa jengo zuri lakini watu waliopo humu wala hawareflect hilo jengo kabisa. wengi ni brainless. sorry kwa kutoka nje ya mada, maana hata sijaisoma, nimeishia kuangalia picha.
 
atatetea vipi kama hajui serikali inakusanya kodi kiasi gani?
acha bangi wewe. sema hujui wewe. serikali inakusanya kodi takriban bil 850 kwa mwezi. kila siku mwigulu na saada wanasema. tatizo lenu misukule mmekeririshwa kupinga kila kitu. wapuuzi kabisa.
 
acha bangi wewe. sema hujui wewe. serikali inakusanya kodi takriban bil 850 kwa mwezi. kila siku mwigulu na saada wanasema. tatizo lenu misukule mmekeririshwa kupinga kila kitu. wapuuzi kabisa.

wewe ndio brainless kabisa haujielewi. hebu rejea post yako ya kwanza hapo juu halafu uilinganishe na hii ya pili.!
 
Ninaamini watia nia wengi hawajui hata tofauti ya majukumu ya
mbunge na mkuu wa wilaya. Tatizo ni kiasi ca malipo cha mbunge
kinachokaribia 11M ndio kinawatoa watu udenda.
Ingewezekana ingefanyika kama kwenye soka,kila mchezaji na mshahara wake
kutokana na anachokifanya. Kumlipa Lissu sawa na Ashumpta ni kama
na kumlipa Ronaldo na Tegete mshahara sawa.
Ukiwa na wabunge kariba ya Lissu/Mnyika/Kafulila unawahitaji wabunge
100 tu na wanapigakazi ya maana. Kuna watu wakiwa wanachangia bungeni
unaona kabisa huyu hata u kaka/dada mkuu Salma Kikwete Sec school hafai.
 
acha bangi wewe. sema hujui wewe. serikali inakusanya kodi takriban bil 850 kwa mwezi. kila siku mwigulu na saada wanasema. tatizo lenu misukule mmekeririshwa kupinga kila kitu. wapuuzi kabisa.

Je matumizi yake ni sahihi na yanawanufaisha wananchi? Ndio mbunge na bunge wanatakiwa kusimamia hayo. Hiyo 850 bilioni ni ndogo sana ukilinganisha na rasilimali.na vitega uchumi vilivyopo. Mbunge ndio anatakiwa asimamie hilo kwa dhati. Takwimu za kodi hazisadii wakati watu wanatubiwa chini ya miti..Abunuas hata kama ni kada wakati mwingine tusimamie ukweli
 
wewe ndio brainless kabisa haujielewi. hebu rejea post yako ya kwanza hapo juu halafu uilinganishe na hii ya pili.!
wala usipate shida na mimi. sio wewe tu ambaye hunielewi, hata mimi mwenyewe sijielewi! hahaaaa!
 
Back
Top Bottom