Nini Majukumu ya Mbunge kwa wapiga kura wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Majukumu ya Mbunge kwa wapiga kura wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Mar 26, 2009.

 1. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,232
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  Ni wazi tumekuwa tukijiuliza maswali kuwa wabunge wamefanya nini majimboni mwao ili kuweza kuwaletea wananchi waliowachagua maendeleo,nimejaribu sana kufuatilia lakini sijaweza kuona uwajibikaji wa moja kwa moja wa mbunge kwa mwananchi aliyemchagua.

  Napenda kuchukua wasaa huu kujadili na ku brainstorm ili tuweze kuona nini kitafanyika ili wananchi watumikiwe na wawakilishi wao pasipo siasa za utapeli.

  Nimejiuliza swali moja,ukianagalia maisha ya wabunge wakati wakipata ubunge na muda waliokaa bungeni,halafu ukalinganisha maendeleo yao binafsi na yale ya jimbo lake kwa ujumla,then utagundua kuwa ubunge ni maslahi binafasi na kama kuna anayebisha aje na hoja na si vioja.

  Quote hii hapo chini nimeitoa kwenye website ambayo ni ya bunge,kwenye highlight pia palinipa tatizo,wenye uelewa zaidi kuhusu issue hii naomba wanipe msaada....Kwamba Government na Administration ni vitu viwili tofauti?

  Tanzania Parliament like its counterparts, in other countries, is the Supreme Legislature of the country. It consists of the President of the United Republic and the National Assembly. It grants money for running the administration of the country and is a very effective instrument for overseeing Government programs and plans. It can also oversee the action of the Executive by being a watchdog to ensure that government is accountable for its administration. The most important function of Parliament is to make laws. The subjects on which Parliament can legislate have been laid down in the Constitution. Parliament is sovereign in the sphere of Legislation.

  The scheme of our Constitution being a United Republic, the Tanzania parliament that is a Union Parliament exercises autonomous powers in the sphere of both Union and Non union Matters which are not under the purview of Zanzibar Government.

  In view of that parliament can assumes the following roles:
  • To pass laws for the good governance.
  • To provide, by giving legislative sanction to taxation and acquisition
   of means to carrying out the work of the government.
  • To scrutinize government policy and administration, including
   proposal for expenditure; and to debate major issues of the day.
   
 2. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,373
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  What's this form1 civics...lol?
   
 3. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,232
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  Kinyambiss i saw that comming, inabidi tukumbushane.Kwasababu malalamiko ni mengi sana kuhusu wanachofanya wabunge kuwaletea wananchi maendeleo.Naelewa wabunge wanaweza kutumia nafasi zao hata nje ya bunge kuhamasisha shughuli za maendeleo majimboni mwao. Ni kutaka kuona ni kivipi mfumo huu unaweza kurekebishwa ili wananchi waweze kunufaika na kura zao na siyo tofauti kwani inaonekana kama ni wabunge ndiyo wananufaika na kura za wananchi...Nilifurahishwa sana na Dk Slaa juzi pale aliposema wazi kabisa pesa wanazolipwa na hali ya wananchi wenyewe ni vitu tofauti sana,kuna wale wanaosema viongozi ni reflection ya wananchi,ili tafsiri hiyo imake sense,basi viongozi hao wasingekuwa wanajali maslahi yao zaidi ya maendeleo ya wananchi.
  Thread hii nimeianzisha ili kujadili issue zote kuhusu namna bunge linavyoweza kuwatumikia wananchi in a more effective way.


  Pia niligusia kwenye highlights walipotumia maneno mawili ya Government na Administration....Mijadala kadhaa iliyopita tumekuwa tukifikia mahali na kulumbana kuhusu baadhi ya tafsiri ya maneno ya kiingereza kwenda kiswahili,najua alimaanisha serikali inawajibika kwenye utawala wake pale aliposema "Govt to be accountable for its administration.

  Ila nina maswali kuhusiana na mfumo wetu wa utawal..For instance accoding to wikipedia, Administration can be defined as the universal process of organizing people and resources efficiently so as to direct activities toward common goals and objectives, if thats the case inaweza vipi ku function effectivelly na ukweli ni kwamba bunge ni la vyama vingi? Je common objectives ni kama zipi hizo ilhali watu hupiga kura kutokana na itikadi?Sijui hiyo line ya maslahi ya Taifa na ya vyama inapochorwa kwasababu bajeti huwa zinaniacha hoi.
   
 4. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,232
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160


  Kinyambisi ilitakiwa waseme "The Government to be accountable to its people" na si eti its "For it Admistration" Umenipata mkuu?
   
 5. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,232
  Likes Received: 191
  Trophy Points: 160
  Juzi,Regia Mtema alikuja humu na thread ya kushangaa kuwa kuna umasikini wa hali ya juu huko Igunga alipokuwepo RA.However tuli idisscuss hii issue,ama kwa kifupi niliifungulia mjadala.Inaonekana mambo mengine ni hadi watu waone kwa macho.Kusema ukweli nilishajiuliza sana tu kuwa ni kivipi wabunge wako accountable for the development of the people they reperesent.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Wakuu
  Kuna wabunge :-
  • wanasifiwa sababu kipindi cha ubunge wao wanaonekana ndio wamewezesha au wmefanikisha mirai fulani majimboni au wilayani kwao
  • Wanakejeliwa kuwa ubunge wao haujawezesha wilaya au majimbo yao kuwa huduma muhimu za maji, barabara, elimu, nk
  • Wanasifiwa kwa sababu bungeni wanasikika wakihoji, kukosoa au kuomba ufafanuzi wa mambo ya msingi kitaifa
  • Hawasikiki lakini wanakubalika au kupendwa na wapiga kura may be sababu ya uwezo wa kifedha
  • Wanasifiwa na wamechaguliwa sababu ya "usomi" wao wa elimu tu na wananchi wengine wanadharauliwa kuwa hawawezi kuwa wabunge "wazuri" sababu ya elimu yao inayoonekana ndogo.
  Sasa maswali
  • mbunge mahairi /asiyefaa anapimwa kwa vigezo gani?
  • Nini hasa majukumu , wajibu na mipaka ya kazi ya ubunge na bunge kama niliyouliza kwenye kichwa cha uzi?
  • je si kuwanyayapaa wakulima kwa kuwbeza watu wenye elimu za form four wanapogombe ubunge?
  • Je wabunge ni watumishi wa umma?
  Nawasilisha
   
 7. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,283
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tujadili mada hii tafadhali.
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,283
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hizi ndio mada za Great thinkers! Please discuss.
   
 9. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,283
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya yametufanya tusahau majukumu halisi ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.

  Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi (legislative), badala yake wanajitwika majukumu ya serikali (excecutive). Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.

  Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.

  Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.

  Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:

  Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.

  Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.

  Wakati mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.

  Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.

  Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.

  Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.

  Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.

  Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.
   
 10. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2016
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 7,410
  Likes Received: 6,514
  Trophy Points: 280
  Kazi kuu ya mbunge (Major duty) ni kuleta maendeleo kwenye jimbo lake anakotokea na si kuongeaa sana na kuchonga sana mdomo bungeni na kuanika sura sana kwenye kamera za Televisheni akiwa bungeni.
   
 11. J

  JGG JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2016
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 316
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Siyo kosa lako, evolution haijakamilika, you are still in the process of evolving into true Homo sapiens
   
 12. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2016
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Kwa mtazamo wangu wananchi wamekuwa wakiwabebesha wabunge kazi za "executive (serikali)" na kusahau kazi kuu ya mbunge. Ndio maana kuna wabunge wanakaa kimya vikao vyote na wala hawachangii kuwasaidia wananchi kuepukana na sheria kandamizi then wanakimbilia kutoa misaada kadhaa majomboni mwao aidha kwa kutojua wajibu wao mkuu au kwa kuamini kuwa wananchi wao wanaangalia hiyo misaada.
   
Loading...