Nini Majukumu ya Mbunge kwa wapiga kura wake?

Mbunge kazi yake kutunga sheria, washatunga sheria ya mtandao mengine ndo kama vile mtajuana nyinyi na wajomba zenu ma mashangazi zenu na mama wakubwa na wadogo, yanakuwa hayawahusu tena wanaconcentrate na kuongezwa posho,
 
Ni kweli bora tungejua kazi zao hasa ni zipi zenye kuendana zile posho zao? maana kwa posho zile inaonesha kazi zao ni ngumu.
 
Kama kuna ,makosa ambayo watanzania tunafanya basi ni pamoja kumchagua mtu kuwa mbunge eti tu kwa sababu alitoa milioni mbili mfukoni mwake na kuchangia uchimbaji wa kisima au ujenzi wa darasa.

Kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yetu sio jukumu la mbunge,
Mbunge ana kazi kuu nne zifuatazo;


1. Kuunganisha watu wake na serikali

2. Kukusanya shida za watu wake na kurudisha majibu

3. Kutunga sheria mpya

4. Kuisahihisha serikali ili itie juhudi zake zote kutimiza hoja za watu.


Wajibu wa mbunge

1. Kuangalia na kutambua shida zinazowakabili wananchi wake.

2. Kuwaheshimu wananchi wake. Kushirikiana na wananchi wake katika kazi mbali mbali za kujenga taifa

3. Kushirikiana na viongozi wa sehemu yake, wilaya na mkoa wake.

4. Kuisaidia serikali itawale vizuri.

5. Kuhudhuria mikutano ya bunge.
NAWASILISHA HOJA
 
Binafsi nimeshangazwa na kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ya kuwataka wabunge wa ubungo na kibamba wasifie upatikanaji wa maji na huduma nyingine katika majimbo yao leo wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi wa barabara ya ubungo kwenda kibaha.Labda tumkumbushe Mkuu wa mkoa jukumu la kutoa huduma ni la Serikali kwa kutumia kodi za wananchi na sio hisani ya mtu.Pia Serikali inataka au haitaki ni lazima itoe huduma kwa wananchi wake kwani inachukua kodi zao.Mbunge kazi yake ni kupigania kero za wananchi wake na kuibana serikali ili kuhakikisha serikali kupitia kodi ilizokusanya kwa hao wananchi zinatumika kutoa huduma.Hivyo Mh.Mnyika hakupaswa kusifia chochote zaidi ya kuitaka Serikali itoe kero za hao wananchi vivyo hivyo na mh.Kubenea.
 
Hawa viongoz ni wapumbavu sana

Kodi zetu haf tukushukuru

Kuna haja ya mabebru kurud kutufunza akili

Hawa black colonies washamba sana
 
Back
Top Bottom